Kiini macho na kihoja kuliko vyote ndani ya nchi ya Zanzibar ni kuwa miaka 56 iliyopita tarehe kama ya leo walipata uhuru wao kutoka kwa mkoloni Muingereza. Sijui ni kutokana na mila walizowekewa na yule anayeandaliwa kuwa mwenye heri ila hawajawahi kuadhimisha siku hii.
Mwezi mmoja baadaye ASP wakaipindua serikali iliyowapatia wazanzibar uhuru na wao wakajitwalia madaraka na ndicho wanachosherehekea hadi leo. Wanakiita mapinduzi matukufu.
Halafu tulikuwa tunaaminishwa kuwa Sultani aliyeitawala Zanzibar alikuwa dhalimu. Udhalimu gani alioufanya ndani ya mwezi mmoja tangia apate uhuru?
Mkuu Mohamed Said hebu tusaidie kwanza ni kwanini nyie wazanziberi hamuadhimishi siku ya uhuru wenu mlioupata tarehe 10 December 1963? Kwanini muadhimishe mapinduzi ambayo mpaka leo hayajulikani hasa lengo lake la halali? Pascal Mayalla unaweza pia kutusaidia
Bendera ya Zanzibar ambayo ilipandishwa baada ya uhuru
Mapinduzi ya zanzibar yaliongozwa na John Okelo au Karume?Zanzibar ya leo ilipatikana kwa mapinduzi ya kufukuza Serkali ya kisultan na kuweka Serkali ya kiraia
Sasa Nyie vijana kila kitu mnaweka siasa
Usione Zanzibar imetulia kwa Amani kuna watu walijitoa muhanga maisha yao kuikomboa Nchi
Kwa mawazo haya ya wipinzani Hawastahili hata kuongoza Nchi maana mawazo yao hayaakisi historia ya Nchi yetu
Wao wanatuletea kitu wanachokiita mapinduzi daima..Naona Nyerere aliogopa kupakana na serikali ya kiarabu. Aisee yule mzee alikuwa muoga balaa.Dunia nzima inatambua uhuru wa Zanzibar kuwa ni 10 December 1963 isipokuwa CCM na wafuwasi wake 😝😝😝
Zanzibar ya leo ilipatikana kwa mapinduzi ya kufukuza Serkali ya kisultan na kuweka Serkali ya kiraia
Sasa Nyie vijana kila kitu mnaweka siasa
Usione Zanzibar imetulia kwa Amani kuna watu walijitoa muhanga maisha yao kuikomboa Nchi
Kwa mawazo haya ya wipinzani Hawastahili hata kuongoza Nchi maana mawazo yao hayaakisi historia ya Nchi yetu
Sultani hakuwa na serikali. Serikali ikiongozwa na Muhammed Shamte ,Mpemba kutoka Ole. Alichaguliwa kwa kura. Nyerere akaivamia nchi na kumkamata yeye na baraza lake la mawaziri na kuwafunga katika jela za Tanganyika kabla hata huo uvamizi haujapewa jina la muungano hapo Aprili 26 ,1964
Sultani hakuwa na mamlaka waZanzibar waikuwa chini muingereza,baada ya uhuru muungano zppp na znp ukaunda serikali iliyokuja kupinduliwa na mwezi mmoja baadae Nyerere akapinduliwa ni waingereza ndo walozima maasi swali linabaki kwanini hawakuzima ya Zanzibar?Zanzibar ya leo ilipatikana kwa mapinduzi ya kufukuza Serkali ya kisultan na kuweka Serkali ya kiraia
Sasa Nyie vijana kila kitu mnaweka siasa
Usione Zanzibar imetulia kwa Amani kuna watu walijitoa muhanga maisha yao kuikomboa Nchi
Kwa mawazo haya ya wipinzani Hawastahili hata kuongoza Nchi maana mawazo yao hayaakisi historia ya Nchi yetu
Kama wangeongoza kwa ubaguzi mbona waziri mkuu alikuwa mpemba?Kwanini kila siku tunamsingizia Nyerere?
Mnatakiwa muwalaumu Wazee wenu wa ZPP kwa kuongoza kwa ubaguzi
Ndio chanzo cha Wazanzibar kuikataa serkali hadi ikapelekea mapinduzi
Kwanini kila siku tunamsingizia Nyerere?
Mnatakiwa muwalaumu Wazee wenu wa ZPP kwa kuongoza kwa ubaguzi
Ndio chanzo cha Wazanzibar kuikataa serkali hadi ikapelekea mapinduzi
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P