Nisamehe kaka lakini historia hii hujaelewa bado. Vita kuu ya kwanza ilianza kama mapigano kati ya mataifa ya Ulaya (si makabila) lakini iliendelea haraka kuwa vita kati ya mataifa ya Ulaya, Asia ya Magharibi (Milki ya Osmani) na Amerika.
Usidhani Waafrika, kadri walivyoshiriki, kwa jumla hawakuelewa kitu. Hawakuwa wajinga. Walikuwepo sehemu walioona faida yao kupanda ngazi ya kijamii kwa kujiunga na jeshi la wakoloni, wengine walilazimishwa tu.
Umewahi kuwaangalia? Walikuwepo pande tatu: hao wa Schutztruppe wa Kijerumani, hao wa Kings African Rifles , hao wa Force Publique wa Kongo. Naona mfano wa hao upande wa Schutztruppe, walikuwepo wengine walioendelea kukutana kama wazee wa vikosi vyao miaka mingi baada ya vita. Wengine waliamua kuhamia upande wa Kings African Rifles.
Picha yako Waafrika "walitendewa tu" si kweli. Unataja biashara ya watumwa - basi isingeanza wala kuendelea bila kuendeshwa na watawala Waafrika. Wazungu (isipokuwa mifano michache ya kinyume) hawakuja Afrika Magharibi kukamata watu. Walikuja kununua watumwa kutoka watawala Waafrika walioendelea kukamata watumwa wengi zaidi baada ya kupata soko la nje.
Unasema kweli hasara upande wa Waafrika ilikuwa kiwango cha elimu, pia hali ya kuwaganyika kati yao.
Wakati wa vita kuu ya pili, Waafrika walijitolea kuwa wanajeshi wa UIngereza kwa sababu waliona faida - pia waliambiwa wanapigana na watu wabaya. Naona azimio lao lilitokana zaida na faida walizoona.
Mkuu baba uko sawa kuiita Vita ya Dunia kwa mtizamo wa kimagharibi, za kuambiwa mimi nilichanganya na zangu kifupi sababu kubwa ya vita ilikuwa ni km ifuatavyo uone sasa Africa imesimamia wapi,;
1. Utaifa-Nationalism, huu utaifa haukuwa kwa watu weusi, bali weupe tupu, ile kuamini kuwa Taifa langu ni Bora kuliko la mwingine, mfano kabila la kijermani Aryan walijiona bora sana kwa maguvu ya kijeshi, kiuchumi,kisiasa kuliko Makabila yeyote ya Ulaya, na waliamini wao ndiyo wameleta Maendeleo Ulaya, hawawezi kuwa Dhalili, wanastahiri kutawala Duniani.
siyo Africa hkn taifa lolote la africa lilikuwa tishio kwa Ulaya wakti huo.bali vijiji/ mashamba yao ya kulimia mazao, na malighafi, yaani tuliitwa Protectorate Land of Tanganyika. siyo Country!
2. Kuimarisha na kukita mizizi ya Ubepari na Ubwanyeye-Imperialism ktk Bara la Africa, Tamaa ya kuwa na Makoloni mengi Africa ilipaa, ambapo Ufaransa na UK walikuwa tayari wanatamba kuwa wamemiliki robo tatu ya Africa kutoka Cairo mpaka Cape of G/Hope. sasa unapigana ili mtu akunyonye? na ambaye bado anakunyonya, hakuheshimu tena unajua? Dharau iliyoje?
kumbuka hapo AFRICA watemi km kina mkwawa wamepigana kumpinga kwelikweli, na kibanga alisha mpiga Mkoloni ina maana waliwachukia walikuwa maadui wao, sasa unapigana kumsaidia adui yako? hiyo ni akili au Matope? hata wao watakuamini vipi kuwa una moyo kabla ya siraha?
Hiyo KAR ni ya humuhumu tu kulinda vijiji PROTECTRATE LAND. na Jerman anatamani Land yake mpaka kesho, ndiyo imeandikwa kwenye hati huko Vatican, Tanzania haiko Vatican, najua kuna wazee walikuwa na ofisi yao palee karibu na Fire! haihararishi kuwa walishiriki kwa uhuru!
Siraha kubwa waliyo tumia Wakoloni ni kuwanyima wa-Africa Elimu. na vita lazima uelimishwe tu! ina maana walibebwa tu bila kuhoji? kama watumwa tu walihoji Uhalali wao wa kupelekwa Utumwani! na kupigana wakiwa na Minyororo Miguuni, KM Kunta Kinte sembuse hao waliokuwa hawana Minyororo?
3. sababu nyingine Millitarism (army race) kupimana maguvu ya kijeshi kuwa nani ana nguvu kubwa kuliko mwingine. Mjermani alijiamini sana kwa hili. Africa haikufikiriwa kuwa na nguvu yeyote! Africa alikuwa km Mrembo anayepiganiwa anasubiri tu nani atashinda achukuliwe akalale naye! uongo?
4. Washirika -alliance, nchi za Ulaya zilijiunga katika ushirika mdogomdogo wa kulindana kijeshi, kisiasa na kiuchumi pia kibiashara mwaka 1882, kupitia umoja wao mfano Triple Alliance, kinara akiwa Mjermani
Usharika huu uliwaumiza sana na kuonekana tishio la wazi kwa UK, na Ufaransa na kujiona kama wametengwa, na wao wakaona ngoja waanzishe usharika wao maarufu kama Tripple Entente, Ushirika huu wa aina mbili tofauti ulisababisha misuguano ya kimasrahi mikali Barani Ulaya. Ma boss wako wanasuguana kwa mzozo ambao huujui. ivo Ulaya kukawepo Makundi mawili mahasimu
Nakuuliza Africa hapo ilikuwa na faida gani? Koloni la Ufaransa ndiyo ilikuwa na Askari wengi vitani kama 20000 tu, kati ya watu laki 2 waliokufa Bara la Afrika robo tatu ni njaa na magonjwa.
Ukweli ni kuwa utumwa tulianza sisi Africa, lkn kwa kujaliana na kuheshimiana, wengine walitunukiwa hata Utemi, Babu yake Mamangu yangu alikuwa Mtumwa na akapewa mke na kumiliki mali na Ngombe wengi mpaka leo wapo!
Wazungu wao walivuruga na kuwafanya km wanyama, walitoa ufadhiri wa siraha kwa watemi ili kukamata zaidi, na mwishowe hizo tawala nazo zika dhoofika vibaya, kiuchumi kwa sababu watu wenye nguvu wazalishaji walipelekwa utumwani, wengine wakatoroka Milki wote! wengine wakawapinga watemi wakorofi!
Wazungu sababu ya tamaa wakaanza kuwakamata watu wa Milki ya Watemi, hapo ndo sekeseke lilipoanza kuwa tata. hata watemi kutoaminiwa na wanoa walinda.
Kifupi Mkuu vita ya 1 na ya 2 ni genge la kikabila la Wahuni wa Ulaya Khazarians, waliokuwa wanatafuta Faida, na kulinda Masrahi yao binafsi Kupitia Population control, Propaganda za kijeshi, na
kweli mpaka leo hao waheshimiwa wako juu ya Sheria Duniani. vizazi mpaka vizazi, wana hati Milki ya Unyonyaji Duniani, wanachimba ardhini kila kitu chenye Thamani Duniani kote! Madini, Mafuta, thamani ya Fedha, Mabenki nk, hakuna wa kuhoji! kwanza hamuwajui! mtahoji nini? Wanaamua nani aongoze nchi gani Duniani na nani asiongoze, Mkuu ni familia kumi na tatu tuu!
Haiwezekani mpigane vita halafu uibe wataalamu mahasimu wakatengeneze siraha kwa adui! halafu mjishambulie tena! kwani hao wataalamu wa Adui unawaamini vipi kuwa chukua kirahisi ivo? rejea OPP.Paper Clip! huwaga nacheeeka sana mtu akisema www1 or 2.
hao sijui wa schutzetruppe mkuu siwajui labda unifungue kidogo!