Kwanini zile karatasi za vipimo vya mgonjwa zahanati binafsi huwa hairuhusiwi kuondoka nazo? Ni utaratibu sahihi wa tiba au ni uhuni?

Hujaelewa jamaa anachozungumzia....anamaanisha kama umepimwa ukakutwa na malaria labda dokta huwa anaandika karatasi ya dawa unayopaswa kutumia ila hawezi kukupa kama hutonunua dawa kwao ila kama utanunua utaondoka na ile karatasi
 
Madhara mojawapo ya kutoka na karatasi ni kuambukizana ujinga, ukweli ni kwamba raia kama dmkali mna ujinga mwingi sana.

Leo ukiumwa ukaandikwa dawa fulani basi unakariri, kesho ukiumwa unataka dawa ile ile.

Mwingine anaambia wajinga wenzie eti mimi niliandikiwa dawa fulani nzuri sana, ilinifaa sana... nao wanaitaka.

Ulisikia wapi!!
 
Hujaelewa jamaa anachozungumzia....anamaanisha kama umepimwa ukakutwa na malaria labda dokta huwa anaandika karatasi ya dawa unayopaswa kutumia ila hawezi kukupa kama hutonunua dawa kwao ila kama utanunua utaondoka na ile karatasi

Huenda anamaanisha hivyo lakini huo ni ujinga zaidi, kwamba kama hununui kwangu sikupi karatasi ila kama unanunua nakupa!!

Ni daktari gani anaweza kujadili na mgonjwa kwa lugha ya kijinga namna hii?

Ooh enewei ameongelea dispensaries ambazo nyingi ni uchwara za magumashi, wanachojaribu ni kumshawishi ili wauze dawa.

Hiyo lugha tu inatosha kuonesha kuwa upo mikono ya biashara na sio huduma iliyo bora.

Angetaka pesa yako isitoke, kama ni maelekezo ya ofisi... kuna namna nzuri ya kufanikisha hilo bila kutia hofu kwa mteja (mgonjwa).
 
Kwani spital ya muhimbili ni ya serekali au ni spital ya TRA ya kukushanya mapato
 
Sijui, lakini nadhani ungenza kutozwa stationery costs hospitalini nadhani ungekuja na swali jingine ?, next time jaribu kwenda na carbon copy wakati anaandika upate copy yako ......, Just trying to help, though sidhani kama nimefaulu....
 
Unafikiri iliwekwa na copy yake kwa sababu gani? Ile ni kama risiti. Ushahidi kwamba dawa alizonazo ana haki ya kuwa nazo na yule wa duka la dawa naye ushahidi kwamba alitoa dawa baada ya mgonjwa kuandikiwa.
Kwa hiyo siyo sahihi kusema mgonjwa hana haki ya kuwa na psrecription au ile copy yake.
 
Ukirnda kunywa dawa zikakudhuru angalau wapate reference ya dawa
 
Zahanati za serikali mgonjwa anaenda na daftari halafu anarudi nalo nyumbani
 
Kwa hospital ambazo wanafaili lako huwa wanabaki nacho for references, ila kuna baadhi ya hospitali ambazo hazina ulazima wa kuwa na faili wanaruhusu uondoke na majibu ya vipimo ila sio prescription kama hizo dawa zipo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…