Kwanini zile karatasi za vipimo vya mgonjwa zahanati binafsi huwa hairuhusiwi kuondoka nazo? Ni utaratibu sahihi wa tiba au ni uhuni?

Kwanini zile karatasi za vipimo vya mgonjwa zahanati binafsi huwa hairuhusiwi kuondoka nazo? Ni utaratibu sahihi wa tiba au ni uhuni?

Kwani hospitali za serikali unaruhusiwa kuondoka nazo?

Wengi mnapotoshwa na mawazo kuwa 'unazuiliwa' ili ununue dawa hapo hapo.

La hasha!
Kinachoandikwa pale sio dawa pekee, ni pamoja na taarifa za mgonjwa. Una haki ya kupewa taarifa, lakini huwezi kusoma mwenyewe ukaelewa.

Kama unahitaji omba utapatiwa, lakini hawawezi kuziachia wazi kwa kila mtu kwa maana haijulikani nani ni nani.

Hii ni kwa usalama/usiri wa taarifa zako.
Hujaelewa jamaa anachozungumzia....anamaanisha kama umepimwa ukakutwa na malaria labda dokta huwa anaandika karatasi ya dawa unayopaswa kutumia ila hawezi kukupa kama hutonunua dawa kwao ila kama utanunua utaondoka na ile karatasi
 
Madhara mojawapo ya kutoka na karatasi ni kuambukizana ujinga, ukweli ni kwamba raia kama dmkali mna ujinga mwingi sana.

Leo ukiumwa ukaandikwa dawa fulani basi unakariri, kesho ukiumwa unataka dawa ile ile.

Mwingine anaambia wajinga wenzie eti mimi niliandikiwa dawa fulani nzuri sana, ilinifaa sana... nao wanaitaka.

Ulisikia wapi!!
 
Hujaelewa jamaa anachozungumzia....anamaanisha kama umepimwa ukakutwa na malaria labda dokta huwa anaandika karatasi ya dawa unayopaswa kutumia ila hawezi kukupa kama hutonunua dawa kwao ila kama utanunua utaondoka na ile karatasi

Huenda anamaanisha hivyo lakini huo ni ujinga zaidi, kwamba kama hununui kwangu sikupi karatasi ila kama unanunua nakupa!!

Ni daktari gani anaweza kujadili na mgonjwa kwa lugha ya kijinga namna hii?

Ooh enewei ameongelea dispensaries ambazo nyingi ni uchwara za magumashi, wanachojaribu ni kumshawishi ili wauze dawa.

Hiyo lugha tu inatosha kuonesha kuwa upo mikono ya biashara na sio huduma iliyo bora.

Angetaka pesa yako isitoke, kama ni maelekezo ya ofisi... kuna namna nzuri ya kufanikisha hilo bila kutia hofu kwa mteja (mgonjwa).
 
Nenda pale Muhimbili ukaombe kuondoka na file lako nyumbani.

File kubaki hispitali ni record management ili ukirudi next time ijulikane ulifanyiwa vipimo gani na kuandikiwa dawa gani, je tatizo la sasa linamahusiano na lile la mwanzo au ni tafauti? Kama unazihitaji sana piga photocopy au picha kwa siku yako.
Kwani spital ya muhimbili ni ya serekali au ni spital ya TRA ya kukushanya mapato
 
Sijui, lakini nadhani ungenza kutozwa stationery costs hospitalini nadhani ungekuja na swali jingine ?, next time jaribu kwenda na carbon copy wakati anaandika upate copy yako ......, Just trying to help, though sidhani kama nimefaulu....
 
Unazoita dispensary pengine ni za magumashi, umesema lengo ununue dawa zao... au kama ni za serikali pengine ni utaratibu rasmi.

Hiyo unayoita karatasi ni 'prescription', wala sio kwajili yako... inaandikwa dawa na maelekezo ya matumizi.

Ile unaandikiwa ili ukachukue dawa FAMASI, sasa kama dawa umepata unaihitaji ya kazi gani?

Siku hizi mifumo imeboreshwa, hakuna cha karatasi ni electronics unapewa namba tu nenda famasi chukua dawa anza kutumia kwa kuzingatia maelekezo.

Utapewa uende nayo ikiwa tu dawa hazipatikani hapo hospitali, na inategemea na aina ya dawa.
Unafikiri iliwekwa na copy yake kwa sababu gani? Ile ni kama risiti. Ushahidi kwamba dawa alizonazo ana haki ya kuwa nazo na yule wa duka la dawa naye ushahidi kwamba alitoa dawa baada ya mgonjwa kuandikiwa.
Kwa hiyo siyo sahihi kusema mgonjwa hana haki ya kuwa na psrecription au ile copy yake.
 
Ukirnda kunywa dawa zikakudhuru angalau wapate reference ya dawa
 
Zahanati za serikali mgonjwa anaenda na daftari halafu anarudi nalo nyumbani
 
Kwa hospital ambazo wanafaili lako huwa wanabaki nacho for references, ila kuna baadhi ya hospitali ambazo hazina ulazima wa kuwa na faili wanaruhusu uondoke na majibu ya vipimo ila sio prescription kama hizo dawa zipo hapo.
 
Back
Top Bottom