Labda na Mimi nitajaribu kugusia maeneo matatu
1.Mwili.mwili wa binadamu ni kama nguo/vazi la roho yake na pindi Mungu anapoangalia mwili wa binadamu anauona kwa kuwa msafi au umechafuka na vyote viwili vitampa mtu kuwa karibu au mbali na Mungu.
2.Dhambi ni uchafu kama mfano wa vumbi,,tope au namna yoyote ya kitu kinachochafua.Kwa hio kama unavyokuwa na mtoto mwenye nguo safi ukamkataza asikae mazingira ya tope,,vumbi,grease au oil chafu ni kama vile unavyokatazwa ukae mbali na dhambi kwa uhusiano wa mwili wako kwamba dhambi inauchafua mwili.
3.Zinaa.zinaa ni dhambi kwa sababu kadhaa,,mtu akizini na chochote hata mnyama ameungana nae kiroho,,mtu akizini na wanawake 10 ameungana nao kiroho na wanashare dhambi na milango ya kifamily,,zinaa haihusishi mwili TU ila inahusisha Hadi roho na ndio maana wanandoa/waliozaa watoto wao Huwa na viashiria na tabia na baraka au mikosi ya pande zote mbili.
Zinaa ni mkataba wa kiroho ndio maana baadhi ya watu hupewa sharti la kuzini na viumbe,,waganga nk kwa ajili ya kufanikiwa katika biashara maisha na mipango Yao..Kwa hio katika kufanikiwa atafanikiwa under control ya kile alichoingiziwa au alichojisajili kama mkataba.Zinaa ni mkataba uliotakiwa Uwe kwa ajili ya kuzaliana katika mazingira yalio rasmi ya ndoa..Nje ya hapo ni kujifunga na wanawake/wanaume mikataba isio rasmi inayopelekea kuzaa wanaharamu,,kutoa mimba na mambo mengine yatokanayo na kutokurasimisha.
Zinaa inajumuisha manii ya mwanaume ambayo yenyewe yanapomwagika bila mpangilio ni najisi na uchi wa mwanamke ambao ni kama chemchem isiotakiwa kuchafuliwa hasa kutokana na matunda yanayotoka ndani yake.Kwamba mwanamke anaweza kuwa hata Malaya kwa kule kuzini TU,,na akatoka katika lengo lake hasa kutokana na zinaa kufungua milango ya kiroho ya mtu ambapo roho chafu kama majini huweza kupitia mlango huo na kumchafua zaidi alozini.