Kwa kifupi si vizuri kutoa lifti, kwa mtu usiemjua awe mwanamke au mwanaume, ni kwa kuhofia usalama tu. Unaweza mpa lift mtu then ajali ikitokea hutaamini kesi itakavyo kutesa. Pia unaweza mpa lift mtu kumbe jambazi, kuna jamaa mmoja alikwenda kuwashusha wenzie home usiku wakitokea kula raha wakiwa njiani walikuta dada anaomba lift wakambeba USIKU WA MANANE, wengine wote walivyoshuka dereva alimuomba huyo dada ahamie siti ya mbele, lakini alikataa na ilikua sanane za usiku, wemekwenda hatua kidogo yule dada alimshuti yule kaka kwa nyuma kichwani. Baada ya hapo alishuka na akaondoka bila kuchukua kitu, mshikaji alikutwa kwa VX yake amekufa. Kwa hiyo wasio toa lift hawana roho mbaya wengine wanafanya kwa nia nzuri tu na kuepa matatizo.