Kwanza Ijue Maana Halisi Ya Kutongoza, Ili Usipate Shida Kujiuliza Unamtongozaje Mwanamke

Kwanza Ijue Maana Halisi Ya Kutongoza, Ili Usipate Shida Kujiuliza Unamtongozaje Mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Kutongoza sio kusifia tu au kujionesha kiasi gani unaweza kumtunza mwanamke.

Wengi huanza kuonesha kumjali mwanamke kwa pesa. Ubaya wake ni kwamba unamfundisha mwanamke ajali pesa yako tu. Na wanawake wengi skuizi wamezoeshwa hivi.
Wanawafundusha wanawake uchunaji.

Wengine wanakesha mtandaoni kutafuta maneno mazuri ya kumwambia mwanamke. Wakikutana na mwanamke wanaongea mno kwa kumwaga sera. Sio vibaya. Lakini huwezi kumshawishi mwanamke akupende bila ya kumjua.
Wanajikuta wanatumia muda mrefu kumshawishi mwanamke kuliko kufurahi na mwanamke.

Lakini, kabla hujamfata mwanamke;
Kutongoza isikupe mawazo. Ukiona kunakupa mawazo kuna sehemu unakosea.
Kutongoza isikufanye ujisikie mdongo/ mnyonge kwa mwanamke.
Kutongoza isikufanye uhisi utamkosa mwanamke ukikosea kidogo.
Kutongoza isikufanye uache mambo yako ya msingi kwa ajili ya mwanamke.
Kutongoza isikufanye ukakosa furaha na kujiamini.
Kutongoza isikulazimu ubebe mzigo wa mahusiano mwenyewe.
Kutongoza isikufanye uvunje mipaka yako kwa ajili ya mwanamke.
Kutongoza isikuharibie bajeti zako.

Bali uchukulie kutongoza ni kama unampa mwanamke zawadi ya muda wako. Ili ajithibitishe kuwa anastahili muda wako na nguvu zako.

Maana ya kutongoza.
Kutongoza ni mchakato wa kujuana baina yako na mwanamke.
Kutongoza ni wewe kumfata mwanamke na kumuonesha kuwa unataka muwe pamoja na mjuane lakini naye pia ajithibitishe kwako kama yupo tayari na anastahili. Unampa zawadi ya muda wako.

Unamfata ukiwa unajiamini, una furaha, mambo yako yapo sawa na unajitegemea kihisia (hautegemei mtu ili wewe uwe na furaha).
Maana yake haumfati mwanamke ili uombe penzi.
Maana yake haumfati mwanamke huku unaogopa atakukataa.
Maana yake haumfati mwanamke ili upate furaha toka kwake.
Maana yake haumfati mwanamke ili awe mwanga maishani mwako.
Maana yake haumfati mwanamke ukiamini yupo juu yako.
Hivyo usijizuie kutaka kumjua mwanamke yoyote umtakaye. Kwa kisingizio chochote. Hauna kisingizio cha maana cha kukufanya usitake kumjua mwanamke umtakaye.
Sio pesa, sio cheo, sio chochote.
Lakini akikataa we chukulia amekosa zawadi ya muda wako.
Wala usilie lie. We sio wa kwanza kukataliwa.

Kwenye mchakato huo wa kujuana kuna;
Kumsifia inapostahili,
Kumrudisha kwenye mstari inapostahili,
Kwenda naye sehemu nzuri inapostahili,
Kumchunguza kama ni wako anayekustahili,
Kufanya naye mapenzi inavyostahili.
Kumtunza inavyostahili.
Kwa kifupi, mfate mwanamke uliyemkubali. Mwambie ungependa kujuana naye. Mtoe out/ kukutana kwako. Muulize maswali yatakayokusaidia kujuana zaidi. Kama unaona anafaa mpeleke kitandani. Kisha mtunze kama mwanamke wako.

Wanawake wanapendelea zaidi kujuana kwanza kabla ya kumwagiana sera za mapenzi.
Ndio maana kuna muda ukimtongoza mwanamke anakuambia, “yaani hata hatujuani unataka …”

Lakini ni muhimu ujue kwamba sio kila mwanamke atataka ujuane naye. Kama ilivyo kwako, sio kila mtu utataka ujuane naye.

Kumwambia mwanamke unampenda na utamuoa hata kabla ya kujuana naye, na wewe mwenyewe hujajua kama kweli utaendana naye uongo.

Hata ukiwa naye kwenye mahusiano endelea kumtongoza.

Usimwache akabaki kukumbukia enzi zenu mlikua hivi mlikua vile. Hapana. Usiache mpaka akajiona wa kawaida na kuacha kujipamba kwa ajili yako, au akaanza kunenepeana sababu haumwoneshi kumtaka au mbaya, akabweteka kwenye mahusiano yenu.

Ona kila siku ni kama siku mpya na umchumbie upya, atazidi kukupenda.

Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
JamiiForums302272342.gif
 
Kuna vijana watakuja kusema andiko
Zuri akimaliza hapo anaenda kwenye sehemu ya muamala na kuthibitisha kutuma vocha ya 10k kwa mwajuma aliyekutana nae jana kwenye daladala ili tu amtumie picha whatsApp

Vijana huwaga hawaskii wala kuambilika juu ya wanawake😅😅🚮
 
Kuna vijana watakuja kusema andiko
Zuri akimaliza hapo anaenda kwenye sehemu ya muamala na kuthibitisha kutuma vocha ya 10k kwa mwajuma aliyekutana nae jana kwenye daladala ili tu amtumie picha whatsApp

Vijana huwaga hawaskii wala kuambilika juu ya wanawake😅😅🚮
Haha! Dah nimecheka sana. Ila acha tuwakumbushe.
 
Mwanamke either akupende au umshawishi aone anaweza kuwa salama na wewe , full stop , hayo mengine ni mbwebwe , note: Mwanamke hana mapenzi ya kudumu hyo haipo....!!! Kama mwanaume usipoteze mda sana na mwanamke ni unpredictable , kuwa naye kama paka wa nyumbani , anazunguka wee anarud home maisha yanaendelea
 
Mwanamke either akupende au umshawishi aone anaweza kuwa salama na wewe , full stop , hayo mengine ni mbwebwe , note: Mwanamke hana mapenzi ya kudumu hyo haipo....!!! Kama mwanaume usipoteze mda sana na mwanamke ni unpredictable , kuwa naye kama paka wa nyumbani , anazunguka wee anarud home maisha yanaendelea
Umenikumbusha kitu....enzi hizo nakua kuna mzee mmoja alikuwa ananiambia "Women are unpredictable"....nimefahamu ukubwani neno hilo
 
Back
Top Bottom