Kwaresma 2018 Special thread...

Kwaresma 2018 Special thread...

Toka nizaliwe sijawahi kuona Mkristo alofunga kwaresma hata mmoja, hapa ofisini nilipo wapo kama 10 hivi cha ajabu tumegonga chai pamoja asb na saiz tumegonga lunch. Huko mtaani washkaji zangu (wakristo) wananiuliza wkend tukanywe wapi. 🙁🙁
 
Asante Da'Vinc kwa makala yako nzuri.

Kwa maelezo yako ni kuwa kipindi hiki tunapaswa kukumbuka viapo vya ubatizo pamoja na kuukumbuka mshumaa uliowashwa siku ya ubatizo.

Kwa ufaham wangu, asilimia kubwa ubatizo hufanywa kwa watu chini ya umri wa mika 5, ambapo hawajawa hata na uwezo wa kutambua viapo vya ubatizo.

Je watu hawa wanakumbuka nini kipindi hiki wakati walibatizwa wangali wadogo.?

Nadhani ubatizo wa ukubwani ni muhimu sana katika imani kuliko kumbatiza mtu ambaye hajielewi labda iwe ubatizo wa hatari.

Tujadiliane hii imekaaje
 
Hivi mbona kama kuna mistari katika Bible ikimuonyeshe yesu alisherehekea pasaka je inakuwaje tena pasaka inamuhusu yeye tena ilihali nayeye alisherehekea, halafu nasikia ilikuwa sikukuu ya mavuno.
Mkuu naomba jibu.
 
Kwaresma ni nini......?

Kwaresma ni kipindi ambacho waamini wakatoliki tunajiandaa kwa ajili ya kuadhimisha mafumbo ya pasaka. (Kifo mateso na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo) Katika kipindi hiki sisi waamini tunaalikwa kutazama tulikotoka yaani kuanzia siku ya ubatizo wetu na kujihoji kwa kina kabisa kama bado vile viapo vyetu tulivyo apa siku ya ubatizo wetu tuna vishika bado ama la! Siku ya ubatizo tunapewa nguo nyeupe na mshumaa unaowaka sasa ni wakati wakujiuliza, Je! Ule mshumaa bado unawaka au umezima kutokana na mapungufu yetu? Kama umezima niwakati sasa wa kuuwasha mshumaa tena, pia kama nguo ile nyeupe tuliyo pewa siku ya ubatizo imechafuka ni wakati sasa wa kuifua kwa kiti cha kitubio. Kwa ujumla ni wakati wa kuingia ndani ya moyo wako na kutazama kama kweli bado tunashika sheria na maagizo ya Mungu. Kwa hakika kwaresma ni muda wa kujitakasa, na kujuta na si hivyo tu bali kuwa jirani zaidi na Mungu kwa kutenda matendo mema kama vile kuwasaidia watu, kufunga na kusali.

Reference..
1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
Mathayo 4 :1

2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
Mathayo 4 :2

Why wakatoliki tu na si wakristo wote?
 
Wakirustu mpate lakujifunza wenzenu hawajaja hapa kwenye uzi na kebehi na matusi ambayo ni vice versa huu ungekuwa uzi unaohusu Uislamu mubadilike mujiunze kuheshimu dini za wenzenu

Note; yesu alifung siku 40 usiku na mchana???! [emoji107]sound fishy here
 
Asante Da'Vinc kwa makala yako nzuri.

Kwa maelezo yako ni kuwa kipindi hiki tunapaswa kukumbuka viapo vya ubatizo pamoja na kuukumbuka mshumaa uliowashwa siku ya ubatizo.

Kwa ufaham wangu, asilimia kubwa ubatizo hufanywa kwa watu chini ya umri wa mika 5, ambapo hawajawa hata na uwezo wa kutambua viapo vya ubatizo.

Je watu hawa wanakumbuka nini kipindi hiki wakati walibatizwa wangali wadogo.?

Nadhani ubatizo wa ukubwani ni muhimu sana katika imani kuliko kumbatiza mtu ambaye hajielewi labda iwe ubatizo wa hatari.

Tujadiliane hii imekaaje

Ubatizo ni moja kati ya sakramenti saba alizotuachia Bwana wetu Yesu kristo. Sakramenti nyingine ni pamoja na Kipaimara, Ekaristi Kitubio,Mpako wa Wagonjwa,Daraja Takatifu na Ndoa. Sakramenti zote 7 zinagusa hatua zote na nyakati zote muhimu za maisha ya mkristo. Zinayajalia maisha ya imani ya mkristo, kuzaliwa kukua,kupona na utume.Sakramenti ya Ubatizo ni msingi wa maisha yote ya kikristo, lango la kuingilia uzima katika roho na mlango unaowezesha kupata sakramenti zingine. Kwa njia ya ubatizo tunafanywa huru katoka dhambi na kuzaliwa upya kama watoto wa Mungu. Sakramenti hii huitwa ubatizo kutokana na madhehebu ya msingi ambayo kwayo hufanyika. Kubatiza kwa Kigiriki (Baptaizein) humaanisha “kutumbukiza” au “kuzamisha” ndani ya maji alama ya kuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo ili uwe kiumbe kipya.

Yeyote anayepokea ubatizo bila kuwa na imani hapati neema za sakramenti hiyo. Ndiyo maana Yesu alipowatuma wanafunzi wake kwenda duniani alisema “aaminiye na kuokoka atabatizwa na asiyeamini atahukumiwa” Mk16:16. Pia anawaeleza mitume wajibu wa kuhakikisha watu wote wanahubiriwa na neno la Mungu na kubatizwa akisema “nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Mt 28:19. Swali la kujiuliza na kuangaliwa hapa ni lini ubatizo ufanyike, je, mtoto mdogo asiyeweza kuamini anaweza kubatizwa au tusubiri hadi awe mkubwa?
Katika suala hili ni kweli kwamba ubatizo ni sakramenti ya imani lakini lazima tukumbuke kuwa imani ina lazima ya jumuia ya waamini, ni katika imani ya kanisa tu kila mwamini aweze kusadiki. Imani inayodaiwa kwa ubatizo si imani kamili na komavu bali ni mwanzo tu ambao lazima ukue. Ndiyo maana mwenye kubatizwa huulizwa “unataka nini katika kanisa la Mungu?” naye hujibu “Imani”. Kwa hiyo iwe amebatizwa akiwa mtoto au mkubwa imani lazima ikue baada ya ubatizo. Na ili neema ya ubatizo iweze kukua, msaada wa mzazi ni wa lazima. Hapo pia ni kazi ya wasimamizi wa kiume na wa kike ambao lazima wawe waamini imara, wenye uwezo na walio tayari kumsaidia mbatizwa katika safari ya maisha ya kikristo. Wajibu wao ni kweli kazi ya kanisa. Jamii yote ya kanisa ina sehemu na wajibu katika maendeleo na katika kutunza neema iliyopokewa kwa ubatizo.
 
Wakirustu mpate lakujifunza wenzenu hawajaja hapa kwenye uzi na kebehi na matusi ambayo ni vice versa huu ungekuwa uzi unaohusu Uislamu mubadilike mujiunze kuheshimu dini za wenzenu
Ni kweli mkuu itabidi tujirekebishe[/QUOTE]

Note; yesu alifung siku 40 usiku na mchana???! [emoji107]sound fishy here[/QUOTE]
Ndio alifunga siku zote usiku na mchana bila kula..
Kama unajua Yesu ni nani huwez doubt kwa hilo
 
Wapendwa katika Kristo
Tumsifu yesu Kristo...

Nawakaribisha waumini wote wa kanisa Catholic na wengine wote wanaoshiriki mateso ya bwana Yesu kristo kwa kufunga na kujielekeza mbele zake MUNGU kipindi hichi cha KWARESMA.
Nawaalika sasa tuweze kutiana moyo, kukumbushana, kufundishana kupitia uzi huu.
Kama una document za kidini weka hapa, nyimbo, picha, sala, miatari ya biblia weka hapa...

Wako katika kristo Da'Vinci..

Tunakimbilia..........
asante kwa ujumbe pia ule waraka wa baraza la maaskofu wote utasomwa nchini kote
 
Toka nizaliwe sijawahi kuona Mkristo alofunga kwaresma hata mmoja, hapa ofisini nilipo wapo kama 10 hivi cha ajabu tumegonga chai pamoja asb na saiz tumegonga lunch. Huko mtaani washkaji zangu (wakristo) wananiuliza wkend tukanywe wapi. 🙁🙁
Umejuaje kama hawajafunga? Kufunga kwa wakristu siyo kama ramadhani bali kujinyima kile kitu ukipendacho kwa siku arobaini na kama ulikua unapenda kunua nguo moya kila wiki unaacha kufanya hivyo kwa siku arobaini na ile hela uliyoiokoa unatoa kama sadaka yako kwa wale wasiokuwa na uwezo. Pili umaweza kufunga baada ya kula milo miwili unakula mulo moja iwe mchana ama usiku lakini zile gharama za lazima ukazitoe kama sadaka. Kufunga kwa wakristu siyo kupiga mbiu bali ni juu yako mfungaji na Mungu wako aliyesirini.

Matthew 16: 16-18
“And when you fast, do not look gloomy like the hypocrites, for they disfigure their faces that their fasting may be seen by others. Truly, I say to you, they have received their reward. But when you fast, anoint your head and wash your face, that your fasting may not be seen by others but by your Father who is in secret. And your Father who sees in secret will reward you.
 
Duh na yesu naye alifunga kwa staili hii?
 
Duh na yesu naye alifunga kwa staili hii?
Ijulikane kwamba hizi zilikua mila za kiyahudi halafu zaidi ya mwanzo wa utumishi wake alupofunga kwa siku 40 hakuna mahali popote ktk biblia panaonyeha alifunga. Na hiyo sura hapo juu kutoka katika injili ya Matayo ni maneno yake yeye Yesu. Soma hapo chini upate uelewa wa siku ya majivu na maana nzima yy kwaresma.
E

What is the significance of the ashes on Ash Wednesday?

Ash Wednesday, the day many Christians mark as the first day of Lent, the time of reflection and penitence leading up to Easter Sunday. ... As they “impose” or “dispense” the ashes, the pastor or priest reminds each Christian of Genesis 3:19: “For dust you are and to dust you shall return.”1
 
Mbona hujajibu swali unazunguka zunguka kama feni.

Swali limeulizwa je na Yesu alifunga kama mnavyofunga nyie wakristo nyakati hizi?

Yaani Yesu nae katika zile siku zake 40 za kufunga alikua anakula kwa kujinyima kama nyie?
 
Why wengine hawalichukulii uzito? Au wanaona ni mambo ya kutunga I need to know?
Wakatoliki,walokole, wasabato nk hwanamisingi yao ya imani wanayofuata. Vipo vingi wakatolic tunafanya wengine hawafanyi ajili ya misingi hiyo
 
Mbona hujajibu swali unazunguka zunguka kama feni.

Swali limeulizwa je na Yesu alifunga kama mnavyofunga nyie wakristo nyakati hizi?

Yaani Yesu nae katika zile siku zake 40 za kufunga alikua anakula kwa kujinyima kama nyie?
Ndugu yangu huu uzi sio kwa ajili ya mabishano
 
Back
Top Bottom