Kwaresma 2018 Special thread...

Kwaresma 2018 Special thread...

*MUNGU YUKO TAYARI KUTUPONYA*

“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima” [HASHTAG]#2Nyakati[/HASHTAG] 7:14-16

Nakusalimu mpendwa wangu katika jina lipitalo majina yote, jina la Yesu Kristo aliye hai.

Tunapoanza kumbukumbu muhimu ya kuakisi kipindi cha Pasaka, kwa hiari kabisa tutaenda kutembea katika maombi ya kufunga kwa siku 40 kuanzia leo hadi siku ya kumbukumbu ya kufufuka Bwana wetu Yesu Kristo. Kama hukuwahi kufunga maishani mwako kwa ajili ya kipindi cha pasaka chukua hatua ya kiimani kufunga mwaka huu kwa kadri ya neema ya Mungu utakavyojaliwa. Kama ni siku zote au baadhi ya siku sawa. Ntajitahidi kukuletea mwongozo wa maombi kila siku alfajiri. Kila siku tutajitoa kufunga kwa masaa 12 tangu asbh saa 12 hadi jioni saa 12. Kuna wengine siku za jumapili watapumzika lakini wenye pumzi tutasonga mbele pamoja nao. Kwa wale watakaofunga kwa muda mrefu inashauriwa sana unywe maji kwa ajili ya kuufanya mwili kuwa na maji maji.

Pamoja na kukumbuka mateso ambayo Kristo aliyapata na kutukomboa pale msalabani, maombi haya tunataka tukamtafute Mungu akaachilie uponyaji kwenye maisha yetu. Tunataka tukasimame kwenye nafasi zetu kumwomba Bwana aliponye Taifa letu, alihuishe na kuliponya kanisa lake, aponye na kuhuisha familia zetu na maisha yetu binafsi binafsi ya kimwili na ya kiroho. Tunataka tukakitumie kipindi hiki kumwomba Mungu aingilie kati mambo ambayo yametutinga kwenye maisha yetu. Kama liko jambo ambalo umekuwa ukiliona ni gumu mbele ya uso wako basi nakuomba sana ungana pamoja nasi kwenye madhabahu hii kumtafuta Mungu. Yasiyowezekana kwa wanadamu, kwa Mungu yote yanawezekana. “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?” [HASHTAG]#Yeremia[/HASHTAG] 32:27. Hakika hakuna la kumshinda Bwana.

Neno la Mungu kutoka [HASHTAG]#2Nyakati[/HASHTAG] 7:14-16 ndilo litakalotuongoza kwenye maombi yetu kwa siku zote kwa ajili ya maombi ya rehema. Na nikuombe tu kama kweli umekuwa ukibarikiwa na kupendezwa na kazi tunayoifanya kwenye madhabahu hii uwe mwaminifu kuniombea kwamba Bwana akanipe nami nguvu na kunifunulia yanipasayo kutembea pamoja kwenye maombi haya. Kuna maeneo mengi tutaenda kumlilia Mungu akatuponye. Kwenye ngazi za Taifa, Kanisa, Familia na mtu binafsi tunataka Bwana akatuponye pia kwenye uchumi, kazi zetu, ndoa zetu, kwenye siasa za Taifa letu, miili, roho na nafsi zetu, watoto na wazazi wetu. Kila eneo kwa neema ya Mungu tutaligusa kwenye maombi yetu. “Hamna kitu kwa kuwa hamwombi!” [HASHTAG]#Yakobo[/HASHTAG] 4:2

Kuomba rehema juu ya Taifa, Kanisa na familia na wewe binafsi liwe jambo la msingi la kila siku kwenye maombi yetu haya kwa siku zote.

Sasa nakuomba mpendwa wangu leo simama kwenye nafasi yako kwa ajili ya kujenga msingi wa maombi ya rehema. Mungu ameahidi kutuponya kama tutarudi mikononi mwake kwa kutubu. “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake?” [HASHTAG]#Yoeli[/HASHTAG] 2:12-17

Hatutamani kuona Taifa letu likiingia kwenye aibu, hatutamani kuona kanisa la Kristo likiingia kwenye aibu, hatutamani familia zetu zikiaibika, hatutamani kama mtu binafsi binafsi unayemtumaini BWANA uaibike. Hapana maana hata maandiko yanasema ‘Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa’ [HASHTAG]#Yoeli[/HASHTAG] 2:32 . Ndugu Mungu yuko tayari kukuponya.

Uko uovu mwingi mpendwa tumeufanya kama Taifa. Watoto, vijana, watu wazima, wanawake kwa wanaume, wageni kwa wenyeji tumemtenda dhambi Mungu wetu kama Taifa. Wajua wewe mwenyewe kwa sababu unayaona vizuri mambo yalivyo mitaani kwetu. Kuwa wazi mbele za Mungu kuomba toba maovu ambayo tunayafanya. Omba rehema kwa ajili ya Serikali yetu. Viongozi wetu ni wanadamu tu wanafanya makosa, wao sio malaika.

Simama kwenye nafasi yako kuomba rehema kwa ajili ya Kanisa la Kristo. Omba rehema kwa ajili ya viongozi wa kanisa watumishi wote waliojitoa kumtumikia Mungu na omba rehema kwa ajili ya kanisa kwa ujumla. Oooh ndugu yangu, yako maovu mengi tumetenda kama kanisa tunahitaji rehema za Mungu. “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” [HASHTAG]#1Yohana[/HASHTAG] 1:8-9

Lakini pia simama kwenye nafasi yako wewe binafsi au na familia yako kuomba rehema mbele za Mungu. Wajua we mwenyewe mapito yako au na ya familia yako. Wajua namna gani mmeanguka na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake” [HASHTAG]#Warumi[/HASHTAG] 3:23-25

Na kila umalizpo kuomba rehema mwambie sasa Bwana atutakase kwa damu ya Yesu. Imeandikwa “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo” [HASHTAG]#1Thes[/HASHTAG]. 5:23

Mungu aliye hai na mwaminifu akubariki na ikiwa umebarikiwa basi share ujumbe huu kwa mwingine naye abarikiwe

“YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU, YAWEZEKANA KWA MUNGU” [HASHTAG]#LUKA[/HASHTAG] 18:27

Kwa maombezi, unataka kupokea uponyaji au kufunguliwa kwenye kifungo chochote kile, ushauri au unatamani ujitoe kikamilifu kumtumikia MUNGU na UNATAKA KUMPOKEA BWANA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO NA AKUSAMEHE DHAMBI ABADILISHE MAISHA YAKO NA TABIA MBAYA ZILIZOKUSHINDA basi wasiliana nasi kwa msaada wa Roho Mtakatifu tukusaidie +255 758 443 873.

MPENDWA WANGU UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. UNASUBIRI NINI KUMRUDIA BWANA YESU NA KUMTUMIKIA?
 
*Nakutakia Kwaresma njema* *Mungu atubariki sote



*Alhamisi baada ya Majivu*
*Mtakatifu Wilfried ,Abate*
*Alhamisi 15 Februari 2018*

*Somo la 1*
*Kum. 30:15-20*

Musa aliwaambia watu akisema: Aangalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki. Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia; nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yoradani, uingie kuimiliki. Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti Baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kupenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.

*Wimbo wa katikati*
*Zab. 1:1-4, 6 (K) Zab. 39:5*

Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
*(K) Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.*

Naye atakuwa kama mti ulipopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
*(K) Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.*

Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushayo na upepo.
Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea.
*(K) Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.*

*Shangilio*
*Zab. 130:5*

Nimemgoja Bwana, roho yangu imengoja, na neno lake nimelitumaini. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, naam, walinzi waingojao asubuhi.

*Injili*
*Lk. 9:22-25*

Siku ile: Yesu aliwaambia wafuasi wake kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.
Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, na kujipoteza mwenyewe?

NENO LA BWANA.....
 
Ufafanuzi wako ni mzuri mkuu. Wengi wanadhani na wamekaririshwa kuwa kufunga ni kula tuu. Bali kufunga ni kujizuia kufanya kile kitu unakipenda au umekua ukikifanya mara kwa mara. Kufunga ni sala na toba na kujitahidi kumrudia mungu.

Huu uzi udumu unatupa elimu kubwa sana.
Kristu.. Tumaini letu !!
Tumaini letu mkuu Pasm..
NI KWELI WAKATOLIKI WANAABUDU SANAMU ?


Utangulizi
Kati ya dhambi ambazo kwa wakatoliki ndiyo wazi kwa watu ni dhambi ya kuabudu sanamu. Dhambi hii imewafanya wakatoliki waonekane au hawasomi Biblia au wanasoma ila hawaelewi au wanasoma na kuelewa lakini wamekuwa wakipuuza maandiko Matakatifu. Ubayana wa dhambi hii kwa wakatoliki ni kile wanachokifanya siku ya Ijumaa Kuu na mambo yanayoonekana katika nyumba za kuabudia kama makanisa ambapo sanamu lukuki zinaonekana, toka zile za vitu vya duniani hadi vile za mbinguni.

Tuhuma kwa wakatoliki haitoki hewani, bali ni kutokana na mambo hayo kwenda kinyume na baadhi ya aya katika maandiko matakatifu. Law. 19:4; 1Yoh. 5:21; Zab.115:1 – 9)
Kifupi ni wazi kabisa kuwa kuziabudu sanamu ni kosa; na hata katika baadhi ya nukuu kuzichonga pia imeoneshwa kuwa ni kosa. (Kumb. 20:3 – 5 na Kumb. 5:7 – 10). Sisi wakatoliki tonazo sehemu nyingi tu tulikoweka hizo sanamu ndiyo maana tunatuhumiwa kuwa kinyume cha Maandiko Matakatifu.

Kwa nini wakatoliki wamechonga sanamu ingawa imekatazwa (Kumb. 20:3 – 5 na Kumb. 5:7 – 10)?
Wakatoliki wameangalia roho ya katazo la kuchonga sanamu na si katazo lenyewe tu. Roho ya katazo la kutochonga sanamu haikuwa Mungu kuamua kuzichukia tu sanamu, la hasha! Bali Mungu aliwakataza waisrael wasichonge sanamu za vitu wala vya duniani wala vya mbinguni kwa sababu alijua kuwa waisrael ambao wakati ule walizungukwa na makabila ya kipagani ambayo yalikuwa na kawaida ya kuabudu sanamu. Ili kuwaepusha Waisraeli, ambao imani yao kwa Mungu mmoja ilikuwa bado kukomaa, aliwakataza wasichonge. Kwa hiyo roho ya katazo hilo lilikuwa ni hatari ya kuanza kuziabudu – kama walivyokuwa wanafanya wenzao wapagani.

Tunasema hivyo kwa sababu Mungu huyo huyo aliyewakataza Waisraeli kuchonga sanamu katika Kumb. 20:3 – 5, mbele kidogo anamwagiza Musa huyo huyo kuchonga sanamu ya makerubi katika sanduku la Agano (makerubi ni vitu vya mbinguni) ( Kumb. 25:18 – 20, Ebr. 9:5). Hapa Mungu ameonekana kutengua kile ambacho alisema pale mwanzoni kuwa wasichonge sanamu yoyote. Utenguzi huo si wakimaana; si wa kiroho ya sheria, bali ni wa kidhana ya katazo. Maana yake, Mungu anamruhusu Musa kuchonga sasa sanamu akijua kwamba Waisrael sasa wamekomaa kiimani kiasi kwamba hata wakichonga sanamu hawataweza kuiabuni ikichukua nafasi ya Mungu. Kwa hiyo roho ya katazo ilikuwa ni kutoabudu sanamu.

Kama haitoshi, ukienda mbele kidogo ya kitabu hicho cha Kumbukumbu la Torati Mungua anafanya mchezo wa hatari zaidi wa kumwambia Musa achonge nyoka wa shaba (kitu cha duniani) na kumweka kwenye mti na kila amtazamaye angepona. (Hes. 21: 8-9, Yoh. 3:14 – 15). Musa alitekeleza agizo hilo naye Mungu alimuhesabu kama mtiifu kwake. Hata hapa pia Mungu ameona kuwa waisraeli sasa imani yao kwa Mungu mmoja ni thabiti kiasi kwamba hata kama wakiona sanamu wasingeweza kuziabudu wakamsahamu Mungu wao. Si kwamba Mungu ana chuki na sanamu, hata kidogo. Kama Mungu angekuwa na chuki na sanamu tusingeweza kuziona nukuu zifuatazo: Kut. 29:37, 1Fal. 7:29, Hek. 16:7.
Kifupi, imani ya mwanadamu hukua kama vile akili ya mtu inavyokua kutoka utoto, ujana hadi utu uzima. Mwanzoni kabisa waisraeli walikuwa kama watoto kiimani. Kumbuka Abrahamu alitoka kwenye nchi ya kipagani baadaye taratibu Mungu anamtoa kutoka katika utamaduni huo wa kuabudu miungu hadi kwenye kumwabudu Mungu mmoja. Kilele cha kumwabudu Mungu mmoja kinafikia pale mlimani sinai wanapopewa sheria. Kukua taratibu huko kwa imani ya waisrael ndiyo sababu inayofanya kuwepo tofauti ya nukuu za Mungu kukataza au kuruhusu kutengeneza sanamu. Hii ni sawa na mtoto anayekatazwa kushika kisu na mama yake lakini anapofikia umri wa kupevuka anaruhusiwa kushika kisu. Sisi wakatoliki siyo watoto wadogo kiimani hata tuogope kuchonga sanamu tusijeziabudu. Tunazichonga tukijua kwamba hata siku moja hazitaweza kutudhuru kwa sisi kuanza kuziabudu. Wale wote wanaogopa kuzichonga sanamu, wajue kuwa wao ni wachanga kiimani.

Kama Mungu hakatazi kuchonga sanamu ila anakataza kuzifanyia ibada, je, sisi wakatoliki hatufanyi hivyo?
Kujibu swali hilo, ndiyo nitakuwa nimegusa kiini cha swali lack Sr. Gracia. Nakuomba fuatilia maelezo yangu, huu ulikuwa kama utangulazi tu.

KUABUDT MSALABA
Kama wakristo, hatuna budi kujisifu kwa vile tumekomboleva kwa fjia ya msalaba ambapo Bwana wetu Yesu Kristo alatundikwa na `kafa juu yake. Lengo la Yesu ni kutuletea wokovt. Mimi na wewe tulistahili kupata adhabu hii ambayo yeye ameipata badala yetu. Kwetu msalaba ni ukombozi, msalaba ni sehemu ya maisha yetu na msalaba ni haki yetu. Hivyo msalaba ni lazima uheshimiwe na si kuabudiwa. Anayepaswa kuabudiwa ni Mungu peke yake. Zipo heshima za viwango tofauti:
Mungu kwanza (latria) – tunamwabudu.
Bikira Maria (Hyperdulia)
Watakatifu wengine na vitu wanavyohusika navyo (dulia)
Picha na sanamu pia hupewa heshima isiyoizidi ile ya watakatifu na Bikira Maria.
Hayo ndiyo madaraja ya heshima ambayo tunazitoa, 2 hadi 4 ni heshima tu.

Mpendwa Sr.Gracia,sijafikia ufundi wa kufafanua yote unayopenda kuyajua ila nataka nijaribu kadiri nitakavyoweza japo kwa kifupi kiha upitie.Yaliyo ya kizushi yafumbie macho na usiniseme nikatengwa na Kanisa. Nianze kwa kueleza maana ya neno sanamu kisha nitaendelea:

Sanamu
Ni kitu kilichochongwa au kutengenezwa kikiwakilisha kitu halisi,mtu,mnyama,mchoro au chochote kile kilicho halisi.Kwa hiyo ili kukiita sanamu,hicho ambacho kimetengenezwa,lazima kikiwakilishe kitu halisi,ndiyo maana ukitembelea sehemu za makumbusho utakuta sanamu za maraisi,nenda Butiama utaikuta sanamu ya Baba wa Taifa letu au kule Zanzibar utakuta sanamu ya mzee Karume n.k.Pamoja na hayo,kitu sanamu,kinaweza kikachukua mtindo wa picha.Mtu aliye na photo albam zile zote zilizomo iwe ni sura za watu,wanyama,miti au vitabu ni sanamu za hao au hicho kilichowakilishwa kwa njia ya hizo picha.Mtu akiandika kitabu cha historia kwa mfano,alichoandika si historia yenyewe kwa kuwa historia huwezi ukaiandika bali ataandika kiwakilishi cha historia ambacho amekiweka katika maandishi.Maandishi hayo{zile herufi} ni sanamu. Kwa maneno mengine,ukiwa huko shuleni unafundisha,herufi zote zilizomo kichwani mwako,ukiziandika tu ubaoni tayari elewa kuwa unaandika sanamu na wote watakayoyasoma hayo maandishi,wanasoma sanamu.Kwa kifupi,sanamu ya kila kitu inaanzia kichwani au akilini mwa mtu,anapoichonga au kuiandika au kuichora basi anaiumba kadili aijuavyo.Kitu halisi kinakuwepo lakini mwandishi au mchongaji amekiwakilisha kwa mtindo wake.

KUABUDU
Hiki daima ni kitendo cha kumtukuza mtu, kitu au chochote ambacho si mungu [herufi ndogo} kama vile unavyomtukuza Mungu {herufi kubwa}mwenyewe.Lazima kila mmoja atambue kuwa anayestahili kutukuzwa ni Mungu tu kama tunavyosoma katika Biblia Takatifu rej.Mdo 17:28 KWA KUWA NDIYE ANATUWEZESHA KWENDA NA KUFANYA CHOCHOTE, au rej Kumb 4:15/28,15:42ff sehemu ambazo Mungu ametukataza kuabudu kitu kingine chochote tofauti na yeye.

Je, tunapotuhumiwa kuwa tunaabudu sanamu wanatusingizia?Sanamu hutusaidiaje?
Lengo la kutumia sanamu ni pamoja na kutukumbusha kitu kilichokuwepo kwani ukufuatilia maelezo yangu juu ya neno sanamu utagundua kuwa huwezi kuitengeneza ya mtu ambaye bado hujamwona.Kwa hiyo zinatumika kama nyenzo ya kutukumbusha yaliyotokea zamani za kale. Ndivyo kwa mfano matumizi ya picha yaliyopoUkienda Nairobi kwenye malezi na huko ukaamua kupiga picha ukiwa katika barabara nzuri utaitunza kama ukumbusho wako na hiyo itakufanya ulikumbuke kwa urahisi tukio hilo kuliko kama ukisimulia tu.
Kuhusu suala la kuabudu ili mtu aambiwe kuwa ameabudu lazima awe ametimiza mambo makuu mawili yaani:
Kuwa na nia kamili ya kuabudu ile sanamu ikichukua nafasi ya Mungu
Kufanya ibaada ya dhati ya kuiabudu hiyo/hizo sanamu.
Kuna mambo kama tisa hivi ambayo mmoja anaweza kuyafanya akiwa katika ibada ya sanamu. Mambo hayo yametajwa katika Biblia Takatifu.
Utoe sadaka Hos 4:13
Uitolee sanamu yako ubani 1 Fal 11:8
Ufanye tambiko mbele ya sanamu yako Isa 57:6
Uitolee zaka Hes 2:8
Uweke sanamu yako juu ya meza au tuseme iwepo meza Isa 65:11
Usujudie sanamu yako 1Fal 19:18
Uiinulie mikono sanamu yako Isa 44:20
Uichezee ngoma sanamu yako 1Fal 18:26
Ulale kifudifudi na kuipigia makofi sanamu yako (1Fal. 18:26).

Nini wafanyacho wakatoliki?
Kwanza, wakatoliki hawaamini juu ya miungu mingi kama walivyofanya watu wa kale.Hakuna mkatoliki anayedai kuwa Maria na Watakatifu ni miungu wala hawasemi kuwa msalaba una nguvu kuliko Mungu.Haya ni mashtaka ya watu wasiojua nini wakatoliki wanakifanya.Wayahudi kwa asili waliabudu miungu mingi hadi pale Mungu alipojifunua kwao na kuwataka waache kuiabudu miungu isiyo ya kweli.Pamoja na hayo katika safari yao ya maisha hawakuonesha kutii agizo la Mungu na matokeo yake waliweza kuiabudu hata miungu ya uongo.

Pili, Wakatoliki wanatambua kuwa Mungu ajua yote na hafungwi na muda.Kwa hekima kubwa aliyonayo,hawezi kuikasirikia sanamu ambayo inaheshimiwa tu kama ukumbusho wala haichukui nafasi yake.Mungu alikuwa akiwaadhibu vikali Wayahudi kwa kuwa kila walipohisi kuwa amewaacha,waliacha kumwamini wala kumwabudu yeye bali wakajitengenezea sanamu za kuchonga na hizo wakasemezana na kukubaliana kuwa ndo Mungu mwenyewe.Mungu alichukia na kuwaadhibu kwa vile waliziabudu na zikachukua hadhi kama ya Mungu wa kweli.

Tatu, Mungu kwa kutambua kuwa si kila sanamu imetengenezwa ili ichukue nafasi yake,aliweza kumruhusu hata Musa kutengeneza sanamu kwa lengo maalumSehemu ambazo Mungu karuhusu sanamu ni nyingi sana katika Biblia rej. Hes 21:8f,Ebr 9:5, Yn 3:14f,Kut 16:31,2 Nyak 3:10, 4:4, Eze 41: 17 ff,n.k Kwanini anaruhusu?Kwa kuwa hazina madhara,zimetengenezwa kwa lengo lisilo la kuziabudu.

Je, tuseme nini juu ya kile tufanyacho Ijumaa Kuu?
Kitu cha msingi ni kusikiliza maneno ya Padre au shemasi anapowaalika watu kuja kuanza kuabudu.Padre au shemasi husema,
“Huu ndio mti wa msalaba, ambao wokovu wa dunia
umetundikwa juu yake, njooni tuuabudu”.
Ukifuatilia kwa makini kiswahili sanifu na bahati njema wewe mwalimu japo sijui wa somo lipi, utagundua kuwa, Padre hufanya mambo haya yafuatayo katika mwaliko huo:
Hutuonesha mti wa msalaba.
Hutuambia kuwa juu ya mti huo,wokovu umetundikwa
Kisha hutualika tukauabudu.

Ningekuwa naongea nawe,ningekuuliza hivi hutualika tukauabudu mti wa msalaba au wokovu ambao umetundikwa juu ya huo mti au tukauabudu mti na msalaba au tukauabudu nini? Hebu fikiri kisha uone kama mawazo yako ni sawa na nitakachokisema hapa chini kabla hujaangalizia!

Wakatoliki hualikwa kufanya nini?
Kwa mwaliko huo,wakatoliki hualikwa kwenda kuuabudu WOKOVU ulio juu ya msalaba.WOKOVU NI NINI? WOKOVU ni jina lililoandikwa kwa kiswahili.Jina wokovu kibiblia na kwa lugha asili ya Biblia ni sawa na jina YESHUA kwa kiebrania au YOSHUA. Mwanangu,wewe unamfahamu Yoshua katika Biblia kuwa alichukua jukumu la kuwaingiza Waisrael katika nchi ya ahadi baada ya Musa kufa kwani huyu ndiye aliyekuwa msaidizi wa Musa.Yoshua aliwachukua watu hawa wakiwa ng`ambo ya mto Yordan wakisubilia tu kuiingia nchi ya ahadi.Kumbe kwa Waisrael Yoshua ni mtu wa muhimu sana kwao kwani baada ya Musa kuwatoka,wanamtumainia Yoshua na kumwona kuwa ni Mwokozi wao kwa kitendo cha kuwafikisha salama katika nchi ya ahadi ambayo kwa miaka karibu 40 wamesafiri kuifikia.Tendo la Yoshua la kuyapiga maji ya mto yakagawanyika na kuacha nchi kavu nao wakavuka bila shida,ndilo wanaloliona kuwa la kuwaletea ukombozi kama alivyofanya Musa pale alipoyapiga maji ya bahari ya Sham yakaacha njia wakapita kwa usalama kutoka Misri.

Kristo ndiyo WOKOVU wetu tunayepaswa kumwabudu kwani alipokuja aliamua kuanzia kazi yake ya kutuletea wokovu katika mto Yordan pale ambapo Yoshua kahitimishia kazi yake.Yoshua aliwavusha watu toka ng`ambo ya mto kuwaingiza katika nchi ya ahadi ambayo ni Kanaan ya duniani na Yesu anapokuja,kama mwokozi,anataka awatoe watu wake kutoka katika nchi ya ahadi ya kidunia,kuwapeleka katika nchi ya ahadi ya mbinguni.Kumbe Yesu ni mwokozi wetu anayetutoa kutoka katika dunia kwenda mbinguni wakati Yoshua anaitwa mwokozi kwa kuwa aliwatoa Misri akawaleta Kanaan nchi ya ahadi.Yesu na Yoshua kwa mantiki hii ni hilo jina WOKOVU kama nomino wakati kazi waliyotenda ni ya kutuokoa na kikitamkwa kama kitendo,Yesu au Yoshua,anaitwa Mwokozi.

Labda nikupeleke kidogo darasani juu ya mambo ya viambishi katika lugha ya kiswahili kwani hapa ndipo wengi wanaposhindwa kueleza kile tunachokiabudu ile Ijumaa Kuu.
Padre au Shemasi husema ,
Huu ndiyo MTI wa msalaba ambao WOKOVU wa dunia Umetundikwa juu yake, njooni tuUabudu.
Katika sarufi ya kiswali hasa tunaposema juu ya upatanisho wa kisarufi, bahati mbaya ni kwamba nomino MTI na nomino WOKOVU zote zimechukua viambishi ngeli U, ili kuwa na upatanisho wa kisarufi. Tunasema kwa mfano, mti umaanguka, wokovu umetujia. Katika sentensi hiyo anayotamka padre au shemasi, ina maneno yote mawili, yaani mti na wokovu yenye kiambishi kimoja tu U kinachotuletea shida kuwa kimaresha nini, wokovu au mti. Kiambishi U, hakirejerei mti bali kinarejea wokovu yaani Yesu.
Kwa hiyo tunaposema njooni tuuabudu, hatumaanishi tuuabudu mti la hasha! Bali tuuabudu Wokovu uliotundikwa juu ya mti wa msalaba katika akili zetu. Ndiyo kusema, ibada hii kama mtu hawezi kutoka nje ya pale na kupeleka mawazo yake kwa Yesu, aliye Wokovu wetu , bila shaka anaweza kuwa anaabudu sanamu au mti wa msalaba.

Mpendwa sista, Kristo Bwana wetu ndiye sanamu ya kwanza kabisa ya Mungu. Ndiyo maana Kristo anasema aliyemwona Yesu kamwona Baba Yn 14:8f. Kama Yesu ni sanamu,hata binadamu ni sanamu za Mungu kwa vile tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.Kama mtu anaziogopa sanamu,ashakumu si matusi,aogope hata kuzaa watoto kwa vile kuzaa mtoto ni kuongeza sanamu duniani kwa kuwa licha ya kufanana na Mungu,zinafanana na mzazi mwenyewe.Kama hatuziabudu,yanini kuziogopa? Kama maandishi ni sanamu lakini hatuyaabudu,kwa nini uogope kusoma herufi? Mungu si mjinga wa kutuhukumu kwa mambo kama hayo yasiyochukua sifa yake.

Pamoja na hayo,tukumbuke kuwa sanamu huanzia kichwani mwa mtu kama nilivyokwishasema.Kama mtu akibuni kichwani kutengeneza gari nzuri sana,hatuwezi kumzuia kwa sababu atakapotengeneza kile alichonacho kichwani kikawa gari,hatakiabudu.La sivyo,hata kupanda gari ili kusafiri tuache kwani tunapanda
Ndani ya sanamu walizotengeneza watu.Ukiwa na picha zako,kwa jinsi zilivyotoka vizuri,ukafurahi na kuzibusu,haina maana kuwa unaziabudu.Au,kwa vile sasa unajua kuwa mtu ni sanamu ya Mungu,je ukienda mahali ukamsalimu mkubwa wako au anayekulea wakati unampa kitu ukampatia huku ukipiga goti, utakuwa unamwabudu?

Hatimaye, Kanisa katika sheria yake no.1159 linafundisha kuwa,sanamu ya Mungu haipo kwani tangu mwanzo Mungu baba hajawahi kuonwa na mtu isipokuwa kupitia kwa mwanae ambaye watu walimwona na waliishi naye wakamfahamu na kumbe kuchonga sanamu ya kufanana naye Isingeliwezekana.Sanamu za Yesu zafanana naye kwa vile watu walimfahamu alivyofanana lakini zimeletwa kwetu kama ukumbusho wa jinsi alivyokuwa si kwa lengo la kuziabudu. Kwa kuziona,hatuna mashaka kuwa alikuwepo kuliko kama tungekuta masimlizi tu.Hivyo hivyo kizazi kijacho kikiambiwa juu ya Nyerere kitaelewa zaidi kikioneshwa picha na sanamu zake lakini hizo picha na sanamu zake hawatasema ndo Nyerere mwenyewe labda kama ni vichaa.

HITIMISHO.
Mungu si mjinga wa kukasirikia kitu kisicho na madhara. Aliwaadhibu wote waliochonga sanamu na kusema hizo zafanana na Mungu lakini sisi hatusemi zinafanana naye bali tunajua kuwa yeye yupo na hizo zipo kama ukumbusho wa sura ya Yesu mwanae ambaye tunamfahamu kupitia waliomwona wakazitengeza. Akili zetu zinapata kutufanya tumtambue Kristo tunapoziona sanamu lakini kwa zenyewe si Kristo wala Mungu wetu
Ukiona sanamu ya B.Maria au Mtakatifu Fulani, ni uthibitisho kuwa, wapo watu waliomwona wakamchonga alivyo na sanamu yake inatukumbusha alivyokuwa nasi tunahizwa kuishi kwa mfano wake. Hakuna aliyewahi kumwona Mungu Baba hivyo hakuna awezaye kuchonga sanamu ya kufanana na Mungu, atachemka tu. Ndiyo maana waisraeli waliadhibiwa, walikuwa wanachonga ndama wanajidai eti Mungu anafanana na Ndama,hayuko hivyo wala hakuna aliyekwisha kumwona ni kutwanga maji kwenye kinu.Mwishowe umeanza kusinzia,naishia hapo pole kwa kukuchosha.

Kifupi, hapo mwanzo Mungu aliwakataza waisraeli kuchonga sanamu kwa sababu aliona imani yao kuwa ni changa wangeweza kuanza kuziabudu, baadaye aliwaruhusu akijua kuwa walikuwa wamekua kiimani kwake, hata wangechonga wasingeweza kuziabudu. Sisi tunachonga kwa sababu imani yetu kwa Mungu imekomaa na hivyo sanamu haziwezi kutufanya sisi tuanze kuziabudu. Juu ya siku ya Ijumaa kuu kinachoabudiwa ni WOKOVU ambao ni Yesu mwenyewe aliye Mungu na hivyo anapaswa kuabudiwa. Hatuabudu mti wa msalaba kwani ni kinyume na Maandiko Matakatifu na kinyume na amri ya kwanza ya Mungu.
 
Milele Amina[emoji120]
JIBU LA JUMLA KWA MASWALI MBALIMBALI YANAYOHUSU SABATO


Baadhi ya maswali yaliyotufanya tutoe jibu la jumla ni haya yafuatayo:

Kulingana na Maandiko Matakatifu Mungu anapaswa kuabudiwa siku ya Sabato. Kwa nini Kanisa Katoliki husali siku ya kwanza ya juma? Kama kuna vifungu vya Biblia vinavyohusu kusali siku ya kwanza ya juma naomba nipatiwe.
Viongozi wa Kanisa Katoliki hawaoni kuwa Sabato ni Agano la milele na wala siyo jumapili?
Katika Maandiko Matakatifu Mungu anasema ikumbukwe siku ya sabato na kanisa katoliki linasema shika kitaklatifu siku ya Bwana yaani Jumapili,hamuoni kuwa mnapingana na Mungu mkuu?
Hamuoni kuwa kusali Jumapili ni amri ya binadamu na wala siyo ya Mungu?
Yesu anasema tufundishe watu yale tu aliyofundisha, kama tusomavyo Mt. 28:19-20, 2Timotheo 3:16, Kumb. 4:2. Inakuwaje mnafundisha kuwa Jumapili ni siku ya Sabato? Je, kufuatana na Maandiko Jumapili ni siku ya ngapi? Je, Mungu alisema tusali Jumapili badala ya Jumamosi? N.K.


Neno “sabato” hutokana na neno la kiyahudi “shabbath” lenye maana ya kukoma, kuacha au kupumzika kufanya kazi. Hii ndiyo maana ya msingi wa neno sabato. Katika matumizi ya baadaye neno hili lilichukua maana ya siku ya saba ya juma ambayo ilikuwa siku ya mapumziko. Hii ni maana ndogo tu ya neno sabato.

Kwa nini wayahudi walishika na wanaishika sabato. Wayahudi huishika sabato kwa sababu tatu kama ndiyo msingi wa amri ya kupumzika:

Sababu ya kwanza ni kukumbuka kitendo cha kuondolewa toka utumwani Misri, kama tusomavyo katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:12-15 “Ishike siku ya sabato uitakase-siku hiyo usifanye kazi yoyote-Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri-Mungu wako alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu- Kwa sababu hiyo Bwan Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.”

Sababu ya pili ni kukumbuka siku alipopumzika Mungu baada ya kumaliza kazi ya uumbaji; kama tusomavyo katika kitabu cha Kutoka 20:9-11 “Siku sita fanya kazi lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana-usifanye kazi yoyote, maana kwa siku sita bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe siku ya saba.” Vile vile tunaweza kusoma kitabu cha Mwanzo 2:3.

Sababu ya tatu na mwisho ni kwamba sabato ni alama ya kwamba Mungu aliliteua taifa la Israeli kuwa mali yake. Kama tunavyosoma katika kitabu cha Kutoka 13:13 “Hakika mtazishika sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote, ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.”
Hizo ndizo sababu tatu za msingi ambazo huwasukuma wayahudi kuishika sabato.

Sabato ilikuwa ni sikukuu ya kila juma kwa wayahudi wote. Sasa tuangalie jinsi wayahudi walivyoisherehekea sabato.

Sabato ilianza siku ya sita (yaani Ijumaa) jioni jua lilipozama. Kabla yake watu walijiandaa kwa kuipamba nyumba, kutayarisha chakula litakacholiwa siku ya sabato, watu walivaa vizuri, na mama wa nyumba aliwasha mishumaa miwili ya sabato. Walifanya hivi kwa sababu waliiheshimu sabato kama bibi harusi ambaye inabidi apokelewe kisikukuu. Baada ya maandalizi, jioni ile ya Ijumaa wakati wa kuzama jua, mtumishi wa sunagogi alipiga baragumu mara tatu kuashiria kuanza kwa sabato. Jioni hiyo sabato ilisherehekewa katika sunagogi na nyumbani. Basi jioni watu walikusanyika katika sunagogi kusali. Sala kwa nafasi hii zilikuwa ni za kumshukuru na kumsifu Mungu aliyewapa watu siku ya sabato. Baada ya sala walirudi nyumbani ambako walikula mlo wa sabato. Kabla ya mlo baba wa nyumba alitamka sala ya sifa na baraka ijulikanayo kama “Kiddush”, kwaajili ya kuwabariki watoto na mama yao, na kumshukuru Mungu aliyewapa mkate na divai. Kwa myahudi kula bila kubariki chakula ni wizi, ni kumwibia Mungu chakula (ni sawa na kula takataka)- kwani vitu vyote ni mali ya Mungu. Wakati wa kula waliweka vituo mbalimbali na kuimba nyimbo za kumsifu na kumshukuru Mungu. Siku ya sabato yenyewe, asubuhi, ilifanyika ibada rasmi katika sunagogi au hekelu.

Kushika sabato:sheria za namna ya kuishika sabato zilikaziwa sana.Wayahudi walitakiwa kuitumia sabato vema, siyo tu waliacha kufanya kazi bali pia hawakuruhusiwa kufanya mipango au kuzungumzia kazi zijazo au zilizopita. Hiyo nayo ilihesabiwa kuwa ni kazi. Haikuiruhusiwa kufanya kazi yoyote wala na mtumwa au mgeni wala hata na mnyama. Mazungumzo yote yalitakiwa yawe ni mambo ya dini tu.
Kazi zilizokatazwa kufanyika siku ya sabato: Kazi za wayahudi zilipangwa katika aina 39 na kukatazwa zote. Baadhi ya kazi hizo ni:-
Kupika na kuoka (Kut. 16:23)
Kutembea siku ya sabato kuliruhusiwa kwa kiasi cha mwendo wa sabato tu, yaani mita 938 au futi 3000 tu (Kut. 16:29)
Kuwasha moto (Kut. 35:3)
Kukusanya kuni (Hes. 15:32)
Kulima na kuvuna(Kut.34:21)
Kuchukua mzigo iwe ni kutoa au kuingiza ndani ya nyumba(Yer.17:21-23)

Kazi nyingine zilizokatazwa ni pamoja na kuwafunga watumwa, kupepeta, kusafisha,kasaga, kukanda unga, kufua viatu, kusokota uzi, kufuma, kufanya vifundo viwili, kukunja nyuzi mbili, kutenganisha nyuzi mbili, kuandika herufi mbili, kuzima moto, kuwasha moto, kugonga kwa nyundo na kubeba kitu kutoka eneo moja hadi jingine. aidha siku ya sabato hakuna kupigana labda kwa kujitetea tu baada ya kushambuliwa au kuvamiwa. Kuponya magonjwa yasiyonyeti na dharura kama vile kupooza, ukoma au upofu zilikatazwa. Pale palipo na hatari ya kifo, msaada ulihimizwa utolewe kwa haraka ili kifo kiepukwe. hIyo ndiyo ilikuwa sabato na kimsingi ndivyo ilivyo hadi leo hii kati ya waumini wa dini ya kiyahudi.

Kwa upande wa Yesu kama myahudi mwngine yeyote mwenye kuithamini dini yake, aliiheshimu siku ya sabato. Alijumuika na wenzake kuhudhuria ibada mbalimbali katika sunagogi. Hata hivyo Yesu hakuipokea tafsiri nzima juu ya taratibu za mapumziko ya siku hiyo. Mafarisayo waligongana na Yesu mara nyingi kwa sababu walimwona Yesu anakiuka sheria za kushika siku ya sabato.

Katika nafasi nyingi Yesu aliwaponya watu siku ya sabato. Sheria ilisema mgonjwa asipate matibabu kamili siku ya sabato iwapo ugonjwa huo haukuhatarisha maisha. Kwa mfano, mtu amepatwa na ajali ya kuvunjika mguu, sheria ilisema mtu huyu ashughulikiwe kiasi cha kuufanya mguu wake usiharibike zaidi, lakini kazi ya kuutengeneza kikamilifu na kuutibu lazima isubiri siku ya pili yake. Matatizo ya ugonjwa aliyoyashughulikia Yesu kadiri ya wayahudi, hayakuwa ya haraka wala muhimu kufanyika hata siku ya sabato. Ni sababu hiyo ilimfanya mkuu wa sunagogi akasirike na kusema, “mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msifike kwaajili hiyo siku ya sabato.” (Rej. Lk. 13:14) Jibu la Yesu kwa wapinzani wake ni kwamba, kumponya mtu siku ya sabato ni tendo jema na hilo halina kizuizi cha wakati. Kila wakati ni wakati wa kutenda mema. Kama wanyama wanasaidiwa siku ya sabato sembuse binadamu! Muhtasari wa mafundisho ya Yesu kuhusu sabato ni huu, “Sabato iliwekwa kwa faida ya binadamu na siyo binadamu kwa faida ya sabato” haya tunayasoma kutoka Injili ya Marko 2:27.
Hiyo ndiyo sabato kati ya wayahudi na mtazamo wa Yesu juu ya sabato.


Sababu yinayotufanya sisi wakatoliki na mathehebu mengine ya kikristo tupumzike siku ya Jumapili na kuitakasa ambayo ni siku ya kwanza ya juma badala ya Jumamosi ambayo ni siku ya saba ya juma.

Utamaduni wa kusali siku ya jumapili unapatikana tangu karne ya kwanza, yaani katika kipindi cha mitume wa Yesu. Kanisa Katoliki na madhehebu yanayosali Jumapili yanafuata nyayo za wafuasi wa kwanza wa Yesu Kristo. Yesu alipokufa mitume waliendelea na utaratibu huo wa kushika sabato, wakati huohuo waliokutana siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili, kwa lengo la kuumega Mkate, ikiwa ndiyo siku ile Yesu alipofufuka. Polepole mambo yalianza kubadilika. Wayahudi walikuwa hawapendi kuona kuwa wakristo nao wanashiriki nao katika Sinagogi au Hekaluni. Kwa sababu walionekana kuwa na ajenda ya siri kwa kushiriki ibada mbili, yaani ile ya Jumamosi (sabato}na ile ya Jumapili-siku ya kwanza ya juma. Wayahudi walitunga ombi la kumi na mbili ambalo lilikuwa kwaajili ya kuwalaani wakristo. Ombi hilo lilikuwa ni kuwalaani wakristo ili majina yao yafutwe kwenye kitabu cha uzima.


Uadui uliupoongezeka kati ya wayahudi washika sabato na wayahudi waliomwamini Kristo, waamini wa Yesu walifukuzwa kutoka katika sinagogi, kama tusomavyo katika kitabu cha Matendo ya Mitume 18:16-18. Baada ya kufikia hatua hiyo, waamini wa Yesu walikutana mahali pao pa sala napo palikuwa nyumbani kwa watu binafsi. Tunayapata haya katika kitabu cha Matendo ya Mitume 18:7, pia 1Kor.16 na Rum. 16: 3-5. Humo waamini walisali,walipata mafundisho kuhusu njia yao mpya na waliadhimisha Ekaristi Takatifu, tendo lililoitwa wakati wa kumega Mkate. Hayo yote yalifanyika siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili. (Rej. Mdo. 20:7). Kipindi ambacho haya yalifanyika ni karne ya kwanza na wala siyo karne ya nne. Hivi, ieleweke kuwa kusali Jumapili ni tendo lililoanza karne ya kwanza na wala siyo karne ya nne kama baadhi ya watu wanavyotushutumu.

Hapa tunaweza kuanza kuulizana kwa nini wafuasi wa Yesu walianza kufanya ibada siku ya Jumapili badala ya sabato ambayo Bwana wetu Yesu Kristo aliiheshimu? Je, walifanya hivyo kwa uhalali gani? Uhalali wa kufanya mabadiliko hayo, ulitokana na tukio kubwa na la msingi kwa wanafunzi wa Yesu, yaani ufufuko wa Yesu siku ya kwanza ya juma(Mt. 28:1; Lk. 24: 1; na Yoh. 20:1). Umuhimu wa siku hiyo ni pamoja na ushindi wa Bwana wetu Yesu Kristo dhidi ya maadui wawili yaani dhambi na mauti. Ilikuwa pia siku ya kuleta matumaini makubwa kwa watu wote waliomwamini Yesu Kristo. Uzito wa tukio hili unaelezwa vizuri sana na mtume Paulo “…kama Kristo hakufufuka, basi, mahubiri yetu hayana maana na imani yetu haina maana”(Rej.1Kor.15: 14). Kwa sababu ya umuhimu wa tukio la ufufuko wa Yesu, siku ya ufufuko iliitwa siku ya Bwana (Ufu.1: 10). Katika lugha ya kilatini siku ya Bwana huitwa Dominika. Wafuasi wa Yesu waliona umuhimu wa kuienzi siku ya Bwana- yaani Dominika au Jumapili wakaifanya kuwa siku ya kumega Mkate kama kumbukumbu ya siku ile ya karamu ya mwisho.
Siku ya kwanza ya juma ilikuwa pia ni siku ya kwanza ya enzi mpya ya maisha; kumsubiri Bwana wetu Yesu Kristo kwa ujio wa pili wa kuwahukumu wazima na wafu.
Utamaduni huu wa kusali Jumapili uliendelea miongoni mwa wakristo hadi karne ya nne, ulipopata nguvu zaidi baada ya Kaisari Konstantino kuitangaza Jumapili kuwa siku ya mapumziko katika dola yake. Kaisari Konstantino katika vita na mpinzani wake Maxentius. Usiku mmoja Kaisari Konstantino aliota ndoto, akiwa katika ndoto aliona maono mfano wa msalaba halafu akasikia maneno haya “katika ishara hiyo utashinda”. Hapo aliamua kubandika ushara ya msalaba katika ngao za askari wake, hatimaye mwaka 312 aliweza kumshinda vitani mpinzani wake katika daraja la Milvia karibu na Roma. Tangu hapo ishara ya msalaba (ambayo ni ishara ya ushindi dhidi ya mauti na kifo kutokana na kifo cha Kristo msalabani) ilipata heshima ikawa ishara ya uzima. Kaisari Konstantino alizidi kuimarisha uhuru wa watoto wa Mungu, pale alipotangaza Jumapili iwe siku ya mapumziko kutokana na ufufuko wa Yesu; siku iliyokuwa na uzito zaidi kuliko siku ile ya sabato, yaani siku ya saba ya juma, ile ya Agano la kale. Konstantino alifanya haya katika karne ya nne, wakati zoezi la kupumzika siku ya Jumapili lilikuwa linafanywa na wafuasi wa Yesu tangu karne ya kwanza. Hivyo tusichanganye mambo hapa kwa kusema kuwa kupumzika Jumapili kulianzishwa na Konstantino. Yeye alichokifanya ni kutoa ruhusa rasmi katika dola yake katika tendo ambalo wakristo walikuwa wakilifanya tangu karne ya kwanza.

Historia ya kupumzika Jumapili si ndogo. Jinsi muda ulivyosonga mbele, miongoni mwa wakristo wakatokea watu walioamua kurudi nyuma kwenda mpaka kwenye Agano la Kale, yaani kupumzika na kuabudu katika siku ya kwanza ya juma, yaani Jumamosi. Kwa maana hiyo utakuta baadhi ya madhehebu ya kikristo yanaendelea kufuata maendeleo ya historia yaliyohamishia sabato siku ya kwanza ya juma iliyo siku ya ufufuko wa Bwana, ambayo ni sabato mpya na wapo wale walioamua kurudi nyuma kwenye sabato ya kiyahudi yaani sabato ya Agano la Kale.

Maelezo ya jumla kufuatia maswali tunayoulizwa juu ya sabato

Sababu zinazotufanya sisi wakatoliki tusali Jumapili ni hizi:
Sababu ya kwanza kubwa na ya msingi ni ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alifufuka siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili. Hili tunalipata katika vifungu vifuatavyo: -Mt.28: 1; Lk. 24:1; Yn. 20:1. Hivi kufuatia umuhimu wa tendo hili la kufufuka Yesu kristo, mitume na wakristo wa kwanza waliifanya siku ya kwanza ya juma kuwa ndiyo siku ya mapumziko. Siku hiyo walipata mafundisho kuhusu njia yao mpya na waliadhimisha Ekaristi Takatifu, tendo lililoitwa kuumega Mkate, Rej. Mdo. 20:7. Tena kwa sababu ya umuhimu wa tukio la ufufuko wa Yesu, siku hiyo ya kwanza ya juma iliitwa “siku ya Bwana” Rej. Ufu. 1:10.
Pili, Yesu mwenyewe baada ya ufufuko wake alikuwa akiwatokea wanafunzi wake katika siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili, Rej.
Tatu, Roho Mtakatifu aliwashukia mitume na watu waliokuwepo nao siku ya kwanza ya juma, Rej.
Nne, siku ya kwanza ya juma ndiyo siku ambayo Mungu alianza kazi yake ya kuumba ulimwengu, Rej.Mwa.

Maana ya msingi ya sabato ni kukoma, kuacha au kupumzika kufanya kazi. Hivi sabato si Agano kama wengine wasemavyo. Zaidi sana sabato si jina la siku fulani katika wiki. Sabato ni kitendo cha kutenga siku fulani moja katika juma ili kumwabudu Mingu. Kwa wenzetu wayahudi siku waliyokuwa wamemtengea Mungu, ilikuwa ni siku ya saba ya juma na walikuwa na sababu zao za msingi. Vigezo walivyotumia kuichagua siku ya saba ni:
Kukumbuka kitendo cha kuondolewa kutoka utumwani Misri.
Sabato ilikuwa ni alama kuwa Mungu aliliteua taifa la Isreli kuwa mali yake.
Kuiga kile alichokifanya Mungu, kwamba alipumzika siku ya saba, baada ya kumaliza kazi ya uumbaji.
Hivyo ndiyo vigezo walivyotumia wayahudi katika uchaguzi wao wa siku ya saba ya juma.

Kanisa Katoliki limeiga utamaduni huo wa kusali Jumapili au siku ya kwanza ya juma toka kwa mitume waliofanya hivyo siku hiyo. Mmoja asifikiri kwamba ni viongozi wa Kanisa ndio waliojitungia utaratibu au utamaduni huu katika kipindi fulani baada ya mitume kufa, la hasha. Kanisa Katoliki linaushika utamaduni huu tangu nyakati za mitume wa Yesu. Wengine wanadhani kulikuwa na mkutano fulani wa Kanisa Katoliki uliojipitishia uamuzi wa kusali Jumapili, la hasha. Kwani Maandiko Matakatifu yanaweka bayana kabisa jambo hili. Watu wa kwanza kupumzika siku ya Jumapili ni wafuasi wa kwanza wa Yesu, katika karne ya kwanza. Kigezo kikubwa walichotumia ni ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ufufuko wa Kristo ndiyo kilele cha ushindi dhidi ya dhambi na mauti. Ufufuko wa Yesu ndio unaoleta maana hata katika kulisoma Agano la Kale. Yesu alipofufuka ndipo watu walianza kusoma upya Agano la Kale na kupata maana sahihi ya ujumbe wa Mungu kwaq wanadamu. Hivi kwa yeyote anayetaka kusoma Biblia na kuielewa vizuri, kiini cha yote ni ufufuko wa Yesu. Yesu mwenyewe anasema, “mwana wa mtu anauwezo hata juu ya sabato”, (Rej. Mk. 2:28). Bila shaka wale wanaosali siku ya kwanza ya juma wamechagua kilichobora zaidi, yaani Bwana Yesu, ambaye ni Bwana wa sabato. Yeyote asiyeipokea siku ya ufufuko wa Yesu kwa namna ya juu sana, huyo si mkristo. (Rej.1Kor.15:14). Siku ya ufufuko ndiyo inayotufanya sisi sote leo tumfuate Kristo. Kama Kristo asingelifufuka bila shaka dini ya kikristo isingekuwepo.



Katika Maandiko Matakatifu Mungu anasema ikumbuke siku ya sabato na Kanisa linasema shika kitakatifu siku ya Bwana yaani Jumapili. Kusali Jumapili ni amri ya Mungu au ya binadamu!
Ni kweli kabisa, Kanisa Katoliki katika amri yake ya sita, linawaalika waamini wake kushiriki Misa Takatifu siku ya Bwana na sikukuu zilizoamriwa. Ufufuko wa Yesu siku ya kwanza ya juma-Jumapili ni uumbaji mpya. Mungu amependa kuumba upya ulimwengu katika mwanae Yesu Kristo baada ya kuharibiwa na dhambi ya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Eva. Kama Mungu baba alivyoanza kuumba siku ya kwanza naye Yesu Kristo ameumba ulimwengu upya siku ya kwanza ya juma ya ufufuko wake. Maana yake nini? Maana yake ni kwamba siku ya kwanza ya juma, imekuwa siku yenye umuhimu zaidi kuliko sherehe na sikukuu zote zinazofahamika hapa duniani.
Zaidi ya hayo, Jumapili (siku ya kwanza ya juma) ndiyo inayoikamilisha maana nzima ya siku ya sabato na kututangazia sisi wanadamu pumziko la milele katika Mungu. Kristo mwenyewe alisema, “msidhani kuwa nimekuja kutengua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutengua bali kukamilisha”(Mt. 5: 17). Vile vile sabato ni kivuli tu, ukweli wenyewe ni ufufuko wa Yesu siku ya kwanza ya Juma- yaani Jumapili. Mtume Paulo anaeleza vizuri sana juu ya ukweli huu, “Kwa hiyo basi msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku ya sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au sabato. Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu ya yale yatakayokuja, ukweli wenyewe ndiye Kristo”
Kufuatia maelezo haya, unaweza kuona kuwa kamwe \Kanisa Katoliki halipingani na Mungu, bali lipo upande wa Mungu na kutangaza ukweli huu kwamba, Kristo alifufuka na ufufuko wa Kristo ni ukamilifu wa Mungu katika kumkomboa binadamu dhid ya dhambi na mauti.kumpinga Mungu ni kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Ili kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu, vitu viwili ni lazima vifanyike:
Cc
Otorong'ong'o jiwe la majiwe Che mittoga[/QUOTE]
 
Wakirustu mpate lakujifunza wenzenu hawajaja hapa kwenye uzi na kebehi na matusi ambayo ni vice versa huu ungekuwa uzi unaohusu Uislamu mubadilike mujiunze kuheshimu dini za wenzenu


Asante mkuu.

Kuhusu Yesu kufungu halina ubishi kwenye Imani ya kikristo.


Note; yesu alifung siku 40 usiku na mchana???! [emoji107]sound fishy here
 
Milele Amina


Bikira Maria aliwatokea watoto watatu wa Fatima. Je, kwa sasa watoto hao wako wapi?

Kweli kwamba Bikira Maria aliwahi kuwatokea watoto watatu katika kitongoji cha Aljuster katika mji wa Fatima huko nchini Ureno barani Ulaya, mnamo mwaka 1917. Hao watoto watatu ni Lucia ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 10 na binamu zake Fransisko alikuwa na umri wa miaka 9 na Yacinta pia alikuwa na umri wa miaka 7. Mpaka sasa watoto hao watatu wote wamekwishafariki dunia. Fransisko alifariki mwaka 1919 na Yasinta mwaka 1920 wakati Lucia, ndiye aliyekuwa mkubwa kuliko wanzake alifariki dunia mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 97.

Tukio la Fatima ni moja ya matukio muhimu kabisa kwa wale wenye imani na upendo kwa Bikira Maria. Kutokea kwa Bikira Maria huko Fatima Ureno matunda yeke ndiyo uimara na uwepo wa vyama vya kitume katika kanisa, Chama cha Fatima na kwa namna fulani chama Lejio Maria. Tukio hilo vile vile ndiyo asili ya Kanisa Katoliki kuifanya miezi miwili katika mwaka iwekwe rasmi kwa heshima ya Bikira Maria. Mwezi wa Mei ambapo Bikira Maria huheshimiwa kwa namna ya pekee katika Kanisa Katoliki kwa sababu ndiyo mwezi ambao Bikira Maria aliwatokea hao watoto kwa mara ya kwanza tarehe 13. Kisha akaendelea kuwatokea kila tarehe 13 ya miezi iliyofuata hadi tarehe 13 Oktoba - ambao pia mwezi wa bikira maria wa Rozari.

Kifupi hilo tukio lilikuwa hivi,
Hawa watoto watatu yaani Fransisko, Yasinta na Lucia walikuwa wanachunga kondoo. Tarehe 13 ya mwezi Mei mwaka 1917 Bikira Maria aliwatokea hao watoto watatu akiwa na mavazi ya kung’aa. Katika tukio hili la kwanza aliwaambia mambo mawili:
Kwanza aliwaambia wasiogope, kuwa yeye ni Bikira Maria ametoka Mbinguni na hivyo wawe wanafika mahali pale kila tarehe 13 ya mwezi kwa muda wa miezi sita mfululizo.
Pili aliwahimiza kusali Rozari kila siku ili kuleta amani duniani.

Mwezi uliofuata yaani mwezi Juni tarehe 13 aliwatokea tena na kusisitiza juu ya kusali Rozari na kuwa kila tarehe ile wafike pale mahali lakini la zaidi aliwaambia kuwa angewachukua Yasinta na Fransisko kwenda mbinguni na kumwacha Lucia ili azidi kueneza ujumbe wake. Taarifa hii ilifuatia swali la Lucia aliyetaka wachukuliwe naye kwenda Mbinguni.

Mwezi uliofuata yaani mwezi Julai 13, aliwatokea tena. Mara hii alisisitiza tena juu ya Rozari na kuahidi kuwa mwezi Oktoba angetoa muujiza mkubwa hata watu wapate kushuhudia. Zaidi alisisitiza sana kufanya toba.

Mwezi Agosti hawakuweza kwenda mahali pale pa kutokea kwa Bikira Maria kwa tarehe ile 13 kwa sababu walikuwa wamekamatwa na kuwekwa ndani na mtawala wa wakati ule eti kwa sababu walisababisha fujo. Hata hivyo, mtawala huyo aliyeitwa Arthur Santos aliwaachia mmoja mmoja akiwatisha kwamba kila aliyemtoa mle kifungoni aliwenda kuchomwa kwa mafuta akiwataka watoe siri ya tokeo hilo. Kwa hiyo mwezi huo wa nane (Agosti) walikutana tarehe 19 badala ya tarehe 13. Mara hii alisema tena juu ya muujiza wa mwezi Oktoba, akisisitiza kusali kwa ajili ya roho zinazoteseka toharani na aliwaambia pia kuwa mahali pale kijengwe kikanisa.
Mwezi Septermba tarehe 13 kama kawaida alitokea tena mbele ya walioshuhudia wapatao watu 25,000. Mara hii hakukukuwa na ujumbe mgeni isipokuwa alisisitiza tu kusali rozari na kuwa mwezi Oktoba angetoa muujiza kama alivyosema hapo awali.

Tarehe 13 Oktoba mwaka 1917, walikusanyika watu wapatao 70,000. Mvua ilianza kunyesha kuanzia tarehe 11 mwezi ule; watu walikuwa wamelowa si kawaida. Waliokusanyika walikuwa wa imani mbalimbali. Hapo mambo yaliyotokea ni haya. Hapo walitokea Yosefu, mtoto Yesu na Mama Maria na huyo mtoto Yesu akiwa ameshikilia skapulari. Walioona haya si wote waliokuwa pale isipokuwa wale watoto watatu yaani Lucia, Fransisco na Yacinta. Watu walichoweza kuona ni jua lililokuwa linajigeuzageuza na kutoa cheche kali za rangi tofauti kama linakaribia kutua chini na kurudi tena juu. Watu walioshuhudia walishangaa sana na mara nguo zao zikakauka.

Pamoja na kuona hayo, mama huyu alitoa ule ujumbe alioutoa katika miezi iliyotangulia. Alisisitiza kusali Rozari na kutubu dhambi. Tukio hilo lilishuhudiwa na watu zaidi ya 70,000 (kama nilivyoseama pale awali) wakiwemo waandishi wa habari na wapiga picha.

Wote mnaonisikia sasa, swali lilikuwa kwamba hao watoto watatu kwa sasa wapo wapi? Baada ya tokeo hilo la mwisho, yaani tarehe 13 mwezi Oktoba mwaka 1917, watoto hao watatu yaani Lucia, Fransisko na Yasinta walirudi makwao na kuendelea na maisha yao ya kawaida. Bahati mbaya mwaka 1919 yaani miaka miwili baadaye Fransisko alifariki dunia. Hii ilikuwa tarehe 4/4/1919. Na, mwaka uliofuata Yasinta naye aliaga dunia katika hospitali ya Lisboni kule Ureno. Ilikuwa tarehe 20/02/1920. Huu ndiyo ukawa mwisho wa maisha ya Fransisko na Yasinta hapa duniani.

Mwaka 1921, Lucia aliamua kujiunga na utawa na mwaka 1928 akawa amefunga nadhiri katika shirika la wa Dorothea la huko Uhispania. Na, ilipofika mwaka 1947 Lucia alihama shirika la Wadorothea na kwenda Shirika la Wakarmeli kulekule Ureno na hapo akawa mlezi wa shirika hilo. Makao makuu ya shirika yalikuwa katika mji wa Koimbra.

Labda la muhimu ambalo unapaswa pia kufahamu ni kwamba, hata baada ya tokeo la mwisho la tarehe 13. 10. 1917, yasemekana Lucia alikuwa mara nyingi anatokewa na Bikira Maria. Mwisho wa maisha yake hapa duniani ulikuwa ni mwaka 2005. kwa hiyo mwaka 2005 tarehe 13. 02 Lucia alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 97.

Nilisema pale awali kuwa Fransisko alifariki mwaka 1917 na Yasinta mwaka 1920. baada ya kifo chao, mwaka 1989 tarehe 13. 05 Papa Yohane Paulo II aliwatangaza kuwa watumishi wa Mungu na mwaka 2000 akawatangaza kuwa wenye heri(maana yake wamebaki tu kutangazwa kuwa watakatifu). Katika historia ya Kanisa Yasinta atakuwa na umri mdogo zaidi kutangazwa mtakatifu asiye shahidi kwani Yasinta alikufa akiwa na miaka 11 na Fransisko miaka 12.

Wote mnaonisikia sasa, kabla ya kuhitimisha jibu la swali tuliloulizwa juu ya hatma ya watoto watatu wa Fatima, napenda kusema yafutayo: kwanza tufahamu kwamba tukio la kutokea kwa Bikira Maria kule Fatima, ni moja ya matokeo mengi ya Bikira Maria. Mengine ni lile la Ludi kule Ufaransa na sehemu nyingine nyingi zilizo maarufu na zisizo maarufu. Baada ya kujua hilo, la pili la kujua ni kwamba matukio kama haya hayatengenezi au hayajengi ufunuo wa pili zaidi ya ule wa Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini matukio haya yanatusaidia sisi katika kukomaza imani yetu katika ufunuo wa Yesu Kristo. Ndiyo, Mungu bado anajifunua kwetu kupitia watu mbalimbali, lakini ufunuo huo hauwezi kujenga historia mpya ya ukombozi zaidi ya kuthitisha zaidi ile iliyohitimishwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa maneno hayo, ndiyo ninasema neno la tatu kwamba, matukio hayo hatulazimishwi kuyaamini, lakini, yanastahili kuaminiwa. Kwa maneno mengine, asiyeamini hawezi kuhukumiwa wala kulaumiwa lakini anayeamini hapotezi chochote; hapati hasara bali anapata faida ya kukomaza imani yake kwa Mungu.


Bikira Maria aliwatokea watoto watatu wa Fatima. Je, kwa sasa watoto hao wako wapi?

Kweli kwamba Bikira Maria aliwahi kuwatokea watoto watatu katika kitongoji cha Aljuster katika mji wa Fatima huko nchini Ureno barani Ulaya, mnamo mwaka 1917. Hao watoto watatu ni Lucia ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 10 na binamu zake Fransisko alikuwa na umri wa miaka 9 na Yacinta pia alikuwa na umri wa miaka 7. Mpaka sasa watoto hao watatu wote wamekwishafariki dunia. Fransisko alifariki mwaka 1919 na Yasinta mwaka 1920 wakati Lucia, ndiye aliyekuwa mkubwa kuliko wanzake alifariki dunia mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 97.

Tukio la Fatima ni moja ya matukio muhimu kabisa kwa wale wenye imani na upendo kwa Bikira Maria. Kutokea kwa Bikira Maria huko Fatima Ureno matunda yeke ndiyo uimara na uwepo wa vyama vya kitume katika kanisa, Chama cha Fatima na kwa namna fulani chama Lejio Maria. Tukio hilo vile vile ndiyo asili ya Kanisa Katoliki kuifanya miezi miwili katika mwaka iwekwe rasmi kwa heshima ya Bikira Maria. Mwezi wa Mei ambapo Bikira Maria huheshimiwa kwa namna ya pekee katika Kanisa Katoliki kwa sababu ndiyo mwezi ambao Bikira Maria aliwatokea hao watoto kwa mara ya kwanza tarehe 13. Kisha akaendelea kuwatokea kila tarehe 13 ya miezi iliyofuata hadi tarehe 13 Oktoba - ambao pia mwezi wa bikira maria wa Rozari.

Kifupi hilo tukio lilikuwa hivi,
Hawa watoto watatu yaani Fransisko, Yasinta na Lucia walikuwa wanachunga kondoo. Tarehe 13 ya mwezi Mei mwaka 1917 Bikira Maria aliwatokea hao watoto watatu akiwa na mavazi ya kung’aa. Katika tukio hili la kwanza aliwaambia mambo mawili:
Kwanza aliwaambia wasiogope, kuwa yeye ni Bikira Maria ametoka Mbinguni na hivyo wawe wanafika mahali pale kila tarehe 13 ya mwezi kwa muda wa miezi sita mfululizo.
Pili aliwahimiza kusali Rozari kila siku ili kuleta amani duniani.

Mwezi uliofuata yaani mwezi Juni tarehe 13 aliwatokea tena na kusisitiza juu ya kusali Rozari na kuwa kila tarehe ile wafike pale mahali lakini la zaidi aliwaambia kuwa angewachukua Yasinta na Fransisko kwenda mbinguni na kumwacha Lucia ili azidi kueneza ujumbe wake. Taarifa hii ilifuatia swali la Lucia aliyetaka wachukuliwe naye kwenda Mbinguni.

Mwezi uliofuata yaani mwezi Julai 13, aliwatokea tena. Mara hii alisisitiza tena juu ya Rozari na kuahidi kuwa mwezi Oktoba angetoa muujiza mkubwa hata watu wapate kushuhudia. Zaidi alisisitiza sana kufanya toba.

Mwezi Agosti hawakuweza kwenda mahali pale pa kutokea kwa Bikira Maria kwa tarehe ile 13 kwa sababu walikuwa wamekamatwa na kuwekwa ndani na mtawala wa wakati ule eti kwa sababu walisababisha fujo. Hata hivyo, mtawala huyo aliyeitwa Arthur Santos aliwaachia mmoja mmoja akiwatisha kwamba kila aliyemtoa mle kifungoni aliwenda kuchomwa kwa mafuta akiwataka watoe siri ya tokeo hilo. Kwa hiyo mwezi huo wa nane (Agosti) walikutana tarehe 19 badala ya tarehe 13. Mara hii alisema tena juu ya muujiza wa mwezi Oktoba, akisisitiza kusali kwa ajili ya roho zinazoteseka toharani na aliwaambia pia kuwa mahali pale kijengwe kikanisa.
Mwezi Septermba tarehe 13 kama kawaida alitokea tena mbele ya walioshuhudia wapatao watu 25,000. Mara hii hakukukuwa na ujumbe mgeni isipokuwa alisisitiza tu kusali rozari na kuwa mwezi Oktoba angetoa muujiza kama alivyosema hapo awali.

Tarehe 13 Oktoba mwaka 1917, walikusanyika watu wapatao 70,000. Mvua ilianza kunyesha kuanzia tarehe 11 mwezi ule; watu walikuwa wamelowa si kawaida. Waliokusanyika walikuwa wa imani mbalimbali. Hapo mambo yaliyotokea ni haya. Hapo walitokea Yosefu, mtoto Yesu na Mama Maria na huyo mtoto Yesu akiwa ameshikilia skapulari. Walioona haya si wote waliokuwa pale isipokuwa wale watoto watatu yaani Lucia, Fransisco na Yacinta. Watu walichoweza kuona ni jua lililokuwa linajigeuzageuza na kutoa cheche kali za rangi tofauti kama linakaribia kutua chini na kurudi tena juu. Watu walioshuhudia walishangaa sana na mara nguo zao zikakauka.

Pamoja na kuona hayo, mama huyu alitoa ule ujumbe alioutoa katika miezi iliyotangulia. Alisisitiza kusali Rozari na kutubu dhambi. Tukio hilo lilishuhudiwa na watu zaidi ya 70,000 (kama nilivyoseama pale awali) wakiwemo waandishi wa habari na wapiga picha.

Wote mnaonisikia sasa, swali lilikuwa kwamba hao watoto watatu kwa sasa wapo wapi? Baada ya tokeo hilo la mwisho, yaani tarehe 13 mwezi Oktoba mwaka 1917, watoto hao watatu yaani Lucia, Fransisko na Yasinta walirudi makwao na kuendelea na maisha yao ya kawaida. Bahati mbaya mwaka 1919 yaani miaka miwili baadaye Fransisko alifariki dunia. Hii ilikuwa tarehe 4/4/1919. Na, mwaka uliofuata Yasinta naye aliaga dunia katika hospitali ya Lisboni kule Ureno. Ilikuwa tarehe 20/02/1920. Huu ndiyo ukawa mwisho wa maisha ya Fransisko na Yasinta hapa duniani.

Mwaka 1921, Lucia aliamua kujiunga na utawa na mwaka 1928 akawa amefunga nadhiri katika shirika la wa Dorothea la huko Uhispania. Na, ilipofika mwaka 1947 Lucia alihama shirika la Wadorothea na kwenda Shirika la Wakarmeli kulekule Ureno na hapo akawa mlezi wa shirika hilo. Makao makuu ya shirika yalikuwa katika mji wa Koimbra.

Labda la muhimu ambalo unapaswa pia kufahamu ni kwamba, hata baada ya tokeo la mwisho la tarehe 13. 10. 1917, yasemekana Lucia alikuwa mara nyingi anatokewa na Bikira Maria. Mwisho wa maisha yake hapa duniani ulikuwa ni mwaka 2005. kwa hiyo mwaka 2005 tarehe 13. 02 Lucia alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 97.

Nilisema pale awali kuwa Fransisko alifariki mwaka 1917 na Yasinta mwaka 1920. baada ya kifo chao, mwaka 1989 tarehe 13. 05 Papa Yohane Paulo II aliwatangaza kuwa watumishi wa Mungu na mwaka 2000 akawatangaza kuwa wenye heri(maana yake wamebaki tu kutangazwa kuwa watakatifu). Katika historia ya Kanisa Yasinta atakuwa na umri mdogo zaidi kutangazwa mtakatifu asiye shahidi kwani Yasinta alikufa akiwa na miaka 11 na Fransisko miaka 12.

Wote mnaonisikia sasa, kabla ya kuhitimisha jibu la swali tuliloulizwa juu ya hatma ya watoto watatu wa Fatima, napenda kusema yafutayo: kwanza tufahamu kwamba tukio la kutokea kwa Bikira Maria kule Fatima, ni moja ya matokeo mengi ya Bikira Maria. Mengine ni lile la Ludi kule Ufaransa na sehemu nyingine nyingi zilizo maarufu na zisizo maarufu. Baada ya kujua hilo, la pili la kujua ni kwamba matukio kama haya hayatengenezi au hayajengi ufunuo wa pili zaidi ya ule wa Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini matukio haya yanatusaidia sisi katika kukomaza imani yetu katika ufunuo wa Yesu Kristo. Ndiyo, Mungu bado anajifunua kwetu kupitia watu mbalimbali, lakini ufunuo huo hauwezi kujenga historia mpya ya ukombozi zaidi ya kuthitisha zaidi ile iliyohitimishwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa maneno hayo, ndiyo ninasema neno la tatu kwamba, matukio hayo hatulazimishwi kuyaamini, lakini, yanastahili kuaminiwa. Kwa maneno mengine, asiyeamini hawezi kuhukumiwa wala kulaumiwa lakini anayeamini hapotezi chochote; hapati hasara bali anapata faida ya kukomaza imani yake kwa Mungu.
 
Toka nizaliwe sijawahi kuona Mkristo alofunga kwaresma hata mmoja, hapa ofisini nilipo wapo kama 10 hivi cha ajabu tumegonga chai pamoja asb na saiz tumegonga lunch. Huko mtaani washkaji zangu (wakristo) wananiuliza wkend tukanywe wapi. 🙁🙁
Mkuu kufunga kipindi cha Kwaresima,inatokana na Imani ya mtu na Uelewa pamoja na hali ya Kiafya ya mhusika. Hivyo usishangae sana.
 
Asante Da'Vinc kwa makala yako nzuri.

Kwa maelezo yako ni kuwa kipindi hiki tunapaswa kukumbuka viapo vya ubatizo pamoja na kuukumbuka mshumaa uliowashwa siku ya ubatizo.

Kwa ufaham wangu, asilimia kubwa ubatizo hufanywa kwa watu chini ya umri wa mika 5, ambapo hawajawa hata na uwezo wa kutambua viapo vya ubatizo.

Je watu hawa wanakumbuka nini kipindi hiki wakati walibatizwa wangali wadogo.?

Nadhani ubatizo wa ukubwani ni muhimu sana katika imani kuliko kumbatiza mtu ambaye hajielewi labda iwe ubatizo wa hatari.

Tujadiliane hii imekaaje
Mkuu sio lazima mtu abatizwe Ukubwani, anaweza kubatizwa akiwa mdogo then wazazi au Walezi watapaswa kuwafundisha Misingi ya Imani, wanapofika utu uzima, wanaimarishwa kwa Mafundisho ya Komunio ya kwanza.
 
Mkuu sio lazima mtu abatizwe Ukubwani, anaweza kubatizwa akiwa mdogo then wazazi au Walezi watapaswa kuwafundisha Misingi ya Imani, wanapofika utu uzima, wanaimarishwa kwa Mafundisho ya Komunio ya kwanza.
Amina amina Kristo aibariki familia yako..
 
Ubatizo ni moja kati ya sakramenti saba alizotuachia Bwana wetu Yesu kristo. Sakramenti nyingine ni pamoja na Kipaimara, Ekaristi Kitubio,Mpako wa Wagonjwa,Daraja Takatifu na Ndoa. Sakramenti zote 7 zinagusa hatua zote na nyakati zote muhimu za maisha ya mkristo. Zinayajalia maisha ya imani ya mkristo, kuzaliwa kukua,kupona na utume.Sakramenti ya Ubatizo ni msingi wa maisha yote ya kikristo, lango la kuingilia uzima katika roho na mlango unaowezesha kupata sakramenti zingine. Kwa njia ya ubatizo tunafanywa huru katoka dhambi na kuzaliwa upya kama watoto wa Mungu. Sakramenti hii huitwa ubatizo kutokana na madhehebu ya msingi ambayo kwayo hufanyika. Kubatiza kwa Kigiriki (Baptaizein) humaanisha “kutumbukiza” au “kuzamisha” ndani ya maji alama ya kuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo ili uwe kiumbe kipya.

Yeyote anayepokea ubatizo bila kuwa na imani hapati neema za sakramenti hiyo. Ndiyo maana Yesu alipowatuma wanafunzi wake kwenda duniani alisema “aaminiye na kuokoka atabatizwa na asiyeamini atahukumiwa” Mk16:16. Pia anawaeleza mitume wajibu wa kuhakikisha watu wote wanahubiriwa na neno la Mungu na kubatizwa akisema “nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Mt 28:19. Swali la kujiuliza na kuangaliwa hapa ni lini ubatizo ufanyike, je, mtoto mdogo asiyeweza kuamini anaweza kubatizwa au tusubiri hadi awe mkubwa?
Katika suala hili ni kweli kwamba ubatizo ni sakramenti ya imani lakini lazima tukumbuke kuwa imani ina lazima ya jumuia ya waamini, ni katika imani ya kanisa tu kila mwamini aweze kusadiki. Imani inayodaiwa kwa ubatizo si imani kamili na komavu bali ni mwanzo tu ambao lazima ukue. Ndiyo maana mwenye kubatizwa huulizwa “unataka nini katika kanisa la Mungu?” naye hujibu “Imani”. Kwa hiyo iwe amebatizwa akiwa mtoto au mkubwa imani lazima ikue baada ya ubatizo. Na ili neema ya ubatizo iweze kukua, msaada wa mzazi ni wa lazima. Hapo pia ni kazi ya wasimamizi wa kiume na wa kike ambao lazima wawe waamini imara, wenye uwezo na walio tayari kumsaidia mbatizwa katika safari ya maisha ya kikristo. Wajibu wao ni kweli kazi ya kanisa. Jamii yote ya kanisa ina sehemu na wajibu katika maendeleo na katika kutunza neema iliyopokewa kwa ubatizo.
Kwa kuongezea, hua katika kila vigilia ya pasaka tunajikumbusha ubatizo kwa kurudia viapo vyetu hivyo ukubwani viapo vinaendelea kukaziwa hadi mwisho wa maisha ya mtu
 
Kwa kuongezea, hua katika kila vigilia ya pasaka tunajikumbusha ubatizo kwa kurudia viapo vyetu hivyo ukubwani viapo vinaendelea kukaziwa hadi mwisho wa maisha ya mtu
Amina sana...
 
Ndivyo tunapaswa kuenenda wakristo kuirarua mioyo yetu na kupata toba na msamaha pamoja na kuishi utakatifu... Maisha duniani ni mafupi na safari kurejea kwa Muumba ni muda wowote hivyo tujiandae sio wakati wa Kwaresma tu bali kipindi chote cha mwaka
 
Back
Top Bottom