Kwaresma 2018 Special thread...

Kwaresma 2018 Special thread...

NAJUA WAJUA LAKINI NATAKA UJUE ZAIDI. *JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!*

*1. Mathayo*
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya Kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

*2. Marko*
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

*3. Luka*
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

*4. Yohana*
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha *"Ufunuo wa Yohana".* Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana, naye ni mtume pekee aliyefariki bila mateso.

*5. Petro*
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Lakini yeye alisulubiwa tofauti na Yesu Kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya *"X"* Petro mwenyewe aliomba asulubiwe kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

*6.Yakobo*
Alikuwa Kiongozi wa Kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu Kristo kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe. Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga mawe mpaka akafa.

*7. Yakobo* (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa Kanisa, Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

*8. Batholomayo*
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

*9. Andrea*
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la *"X"* miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii".

*10. Tomaso*
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko India.

*11. Yuda (Thadei)*
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

*12. Yuda (Iskariote)*
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

*Kumbuka:*
*13. Thadayo (au Mathia)* ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (Msaliti). Huyu alipigwa kwa mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

*14. Paulo*
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 100 A.D.

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika Agano Jipya, kama vile Waraka wa Paulo Mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

Kumbuka: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, *"Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka."* Mathayo Mtakatifu 10:23

*SAMBAZA KWA WENGINE TUJIFUNZE HISTORIA YA KANISA*
 
SOMA MAKALA MAALUM NA MAANA KAMILI YA KWARESMA


Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40)
mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu.



Kwaresma ni kipindi maalum ambacho wakristo wanakumbuka maisha ya Yesu kristo hapa duniani hususan mateso, kufa na kufufuka kwake.


Ni kipindi cha kutafakari maana na umuhimu wa dhabihu ya YESU kristo katika ukombozi wa dunia na kumrudia Mungu. Aidha ni kipindi ambacho wakristo wanakumbushwa kufanya toba na kumrudia Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu.




Ingawa kipindi cha kwaresma ni kipindi cha mafungo kwa wakristo, watu wengi na hasa wa dini nyingine hushindwa kutambua funga inayofanywa na wakristo katika kipindi hiki na hasa kwa sababu wakristo wengi huonekana wakiendelea kula na kunywa wakati wa kwaresma. Wakristo walio wengi pamoja na kufuata kielelezo cha Yesu kristo ambae alifunga siku arobaini (usiku na mchana) huzingatia maagizo ya YESU mwenyewe na nabii Isaya ambao kwa kiasi kikubwa hufafanua aina ya funga ambayo wakristo wanapaswa kuizingatia.

Mwenyezi Mungu alitoa maagizo ya namna ya kufunga kupitia kwa nabii isaya akisema hivi
"Walakini wanitafuta kila siku, hupenda kujua njia zangu ; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao. Hutaka kwangu sheria za haki, humkaribia Mungu. Husema, mbona tumefunga lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. Je, kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je, ni siku ya mtu kujitabisha nafsi yake? je ni kuinamisha kichwa kama unyasi na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? je utasema ni siku ya kufunga na ya kukubaliwa na BWANA? Je, saumu niliyoichagua sio ya namna hii? Kufunguo vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaachia huru walio onewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia, utukufu wa BWANA (Mungu) utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita na BWANA ataitika, utalia nae atasema mimi hapa..." (Isaya 58: 2-9).

Mwenyezi Mungu alitoa maagizo haya baada ya kuona watu wengi wakipoteza muda mwingi na kujitabisha kuacha kula na kujitesa miili yao ili kumpendeza Mungu, huku wakisahau mambo muhimu zaidi ambayo Mungu anawataka wafanye ili kumpendeza. (Katika kipindi hicho wayahudi walikuwa wakifunga kwa kujitesa sana ikiwa ni pamoja na kuacha kula, kuvua nguo zao za thamani na kuvaa magunia, kujipaka majivu na wengine kujipiga na kujikata miili yao ili waone maumivu zaidi.

Aidha, watu walikuwa wakitumia kipindi cha kufunga kuuonesha umma jinsi walivyo wacha Mungu na hivyo kupewa heshima mtaani. Mtu asiyefunga alionekana mjinga, mtenda dhambi na asiyefaa katika jamii. Kufunga ilikuwa sehemu ya maisha na si suala la uhusiano binafsi kati ya mtu na Mungu).

Kwa vile Mwenyezi Mungu wetu ni wa upendo na huruma, alimtuma nabii isaya kuwaambia watu hao kuachana na funga hiyo isiyo na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika mambo muhimu ambayo Mungu anaangalia katika kutathimini utu wa mtu. Mambo hayo ni upendo, huruma na kujitoa kama ilivyoelezwa hapo juu na kuachana uovu wa aina zote.. Kwa msingi huo, mtu mwenye upendo na anaejitoa kusaidia wengine ana thamani kubwa mbele za Mungu kuliko mtu anaeshinda njaa siku 300 za mwaka pasipo kuonesha upendo wa kweli kwa wengine.


Yesu kristo alipokuja ulimwenguni, alisisitiza maneno ya nabii Isaya kwa kutaka watu waache tabia ya funga za kujionesha kwa watu, na badala yake wajitahidi kumpendeza Mugu. Yesu alisema"Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye nyuso za kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amini nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako (Mungu) aliye sirini; na baba yako aonae sirini atakujazi" (Mathayo 6:16)

Kumbe tabia ya kujionesha mbele za watu kwamba tumefunga inamuudhi Mungu na kutufanya tukose thawabu. Mtu anaejionesha au kujisifu kwamba anafunga huambulia kusifiwa na watu wa kidunia ambao wanadhani mtu huyo ni mtakatifu sana, lakini kwa mujibu wa maandiko matakatifu mtu huyo anajisumbua na kupoteza muda wake bure kwani hakuna thawabu anayo pata kwa Mwenyezi Mungu.


Tumuombe Mungu sana atuongoze na kutusaidia katika kipindi hiki cha Kwaresma na baada ya hapo.Ni wajibu wetu kujitahidi kuachana na maovu yote, kufanya toba ya kweli na kumpokea Yesu katika mioyo yetu badala ya kumuabudu kwa midomo tu. Tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu wetu ni yule yule kabla, wakati na baada ya kipindi cha Kwaresma na hivyo kipindi hiki kiwe kipindi cha kutukumbusha na kutuandaa kwa ajili ya wakati mrefu ujao baada ya Kwaresma.

Nawatakia Kwaresma njema waumini wote wa Kristo duniani popote mlipo
 
Habari! Naomba mwenye wimbo huu anitumie WhatsApp 0717246284.

Unihurumie mimi Bwana, nimetenda dhambi mimi Bwana, ninakusihi, ee Mungu wangu, unisamehe, makosa yangu, ( niliyokutendea wewe Mungu wangu na jirani zangu ) x 2
 
Kwa Neema na baraka zake muumba tumeweza kufika Kwaresma ya Mwaka 2023.

Ni kwa Neema tu👼🤗☺️
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Ashe to ashe...Dust to dust
Tu wamavumbi ba mavumbini tutarudi
1677046971710.png
 
Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma. Ni kipindi kinachotualika kumwilisha ndani mwetu utamaduni wa upendo, kwa kufunga na kutenda matendo ya huruma, kama vile kuwasaidia wahitaji hasa maskini, kuwatembelea wagonjwa na hata wafungwa. Ni kipindi cha toba, kipindi cha kujipatanisha na Mungu, kujipatanisha na Kanisa, ndugu katika familia, marafiki zaidi sana ni kujipatanisha mtu na nafsi yake.

Kwaresima ni safari ya maishaya kiroho ambayo kilele chake ni adhimisho la fumbo la ukombozi wetu - mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo tunaloliadhimisha katika juma kuu, kuanzia alhamisi kuu, ijumaa kuu na jumamosi kuu,kilele chake ni domenika ya Pasaka. Kusali, kujitoa sadaka kwa ukarimu kwa wahitaji na kufunga, ndizo nguzo kuu tatu za kipindi cha Kwaresima, kipindi cha toba.

Siku ya kwanza ya kipindi hiki cha Kwarema huitwa Jumatano ya Majivukutokana na tendo la kupakwa majivu katika paji la uso na wakati huo mhudumu wa tendo hili takatifu la kiroho akisema; Mwanadamu kumbuka, u mavumbi wewe na mavumbini utarudi.

Jina hili la Jumatano ya majivu, lilianza kutumika rasmi mwaka 1099 na Papa Urbano II. Mwanzoni iliitwa “Mwanzo wa Mfungo”.
Majivu yanayotumika siku hii ya Jumatano ya majivu ni ya matawi ya mitende yaliyotumika Jumapili ya Matawi ya mwaka uliopita ambayo yanaashiria ushindi dhidi ya dhambi na mauti kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Kwanini kupakwa majivu? Majivu ni alama au ishara tu ya nje inayoashiria toba ya ndani ya mioyo yetu kama ilivyo rangi ya kijivu ambayo ni rangi ya toba na matumaini. Kupakwa majivu ni ishara ya toba yetu ya ndani ya nafsi zetu tunayoifanya ambayo inatutakasa na kutusafisha na uovu wote, kama Majivu yanavyotumika kusafisha vyombo.

Kumbe kupakwa majivu ni kukubali kwetu kuwa tu wachafu, tu wadhambi, tunahitaji kusafishwa, tunahitaji kutakaswa. Majivu ni mbolea na mbolea hutumika kukuza mimea na kuifanya izae matunda mema, mengi na bora. Toba ya kweli tunayoifanya ndani mwetu ikiashiriwa na alama ya majivu hutusaidia kukua na kuzaa matunda mema ya kiroho. Majivu haya yanapakwa kwenye paji la uso, kama vile siku ya ubatizo tulipopakwa mafuta ya Krisma takatifu, tukaondolewa dhambi ya asili na adhabu zake zote, kwa ishara ya msalaba, alama ya ushindi tuliyokombolewa nayo.

Kumbe majivu yanatukumbusha kufanya toba na kuungama dhambi tulizotenda baada ya ubatizo. Kupakwa majivu katika paji la uso ni kukiri hadharani bila kujificha kuwa tu wadhambi na tunahitaji huruma ya Mungu Baba, tunahitaji msamaha, tunahitaji kutakaswa na kufanywa upya watoto wa Mungu na wa Kanisa.

Asili ya kujipaka majivu kama alama ya toba:
Tendo hili la kiroho la kupakwa majivu katika paji la uso ni ishara ya toba ya kweli, ishara ambayo imekuwa ikitumika kwa maelfu ya miaka iliyopita hata kabla ya kuja Kristo. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10).

Baadaye utamaduni huu wa kupakwa majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba. Mwaka 600 hivi, Gregory Mkuu aliifanya siku ya Jumatano ya majivu kuwa siku ya kwanza ya Kwaresma na kufanya kipindi hiki cha toba kuwa ni cha siku arobaini. Miaka ya 800 hivi, baadhi ya makanisa yaliadhimisha ibada ya Jumatano ya majivu kwa ajili ya wadhambi waliokubuhu katika dhambi na waliojulikana. Wadhambi hawa waliojulikana walipoamua kufanya toba na kubadili maisha yao walipakwa majivu.

Hivi wakati huu si wote walipakwa majivu ila tu wale waliokuwa wadhambi waliojulikana wazi, kama vile makahaba, wauaji na waasi. Kuanzia karne ya 11, Kanisa kwa kutambua kuwa mbele za Mungu hakuna asiye na dhambi, liliamuru tendo hili liwe kwa waamini wote likiambatana na kufunga, kusali, kutoa sadaka na kufanya matendo ya huruma.

Katika Somo la kwanza la kitabu cha Nabii Yoeli (2:12-18);
Mungu anatuita tumrudie Yeye kwa mioyo yetu yote, na kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza. Tunaambiwa tuirarue mioyo yetu, na siyo mavazi yetu. Katika siku za Agano la Kale, watu walikuwa na desturi ya kurarua mavazi yao kama ishara ya kufanya toba.

Hata hivyo, walikuwepo wengine waliokuwa wakiyararua mavazi yao kama ishara ya nje tu, lakini ndani ya mioyo yao hawakuwa na nia ya kufanya toba ya kweli. Mioyo yao ya “jiwe” haikuweza kubadilika! Watu hawa hawakuwa wameyaacha mambo ya kiulimwengu na kuanza kuyaishi maisha mapya, maisha ya kumcha Mungu.

Nabii Yoeli, anatuita kumrudia Mungu sio kama mtu mmoja mmoja, bali ni wito kwa watu wote; “Pigeni tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyikeni kusanyiko kuu; kusanyikeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyikeni wazee kusanyeni watoto na hao wanyonyao maziwa” (Yoe 2:15). Mtume Paulo, katika somo la pili la Waraka wake wa pili kwa Wakorintho (2Kor 5:20-6:2); anatusihi tupatanishwe na Mungu kwa ajili ya Kristo.

Mungu Baba alimtuma Mwanawe wa pekee, Yesu Kristo, aje kutukomboa kwa kuteswa na hata kufa msalabani. Mungu asiyejua dhambi alimfanya Yesu Kristo kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye (2Kor 5:21). Yesu Kristo hakujua dhambi, lakini alifanywa kuwa dhambi; vivyo hivyo sisi tusio haki tunafanywa kuwa haki katika Yeye. Sisi wadhambi tulistahili kifo hiki cha kutisha, kifo alichokufa Yesu kutokana na Upendo wa Mungu.

Katika Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo (Mt 6:1-6;16-18); Yesu anatufundisha namna tunavyopaswa kukiishi kipindi hiki cha Kwaresima.
Yesu anatuonya tusiwe wanafiki, tusifanye matendo mema ili tuonekane machoni pa watu wengine, kwani kwa kufanya hivyo tunakuwa tumepokea thawabu yetu kwa njia ya watu wanaotutazama, kutustaajabia, na kutusifia.

Kumbe, matendo yetu mema yasilenge kujionesha kwa watu wengine, bali yawe ni mawasiliano binafsi kati yetu na Mungu yaani kujenga muungano na Mungu wetu aliyemtakatifu kwa sala, sadaka na kufunga. Matumaini ya mafungo yetu hayana budi kujengeka katika njaa na kiu ya muungano na Mungu wetu mtakatifu.

Muungano huu unawezekana tukiwafungulia mlango wenzetu hasa wahitaji na kuwapatia yale tutakayojinyima. Ni katika mfungo ndipo tunaweza kuiga mfano wa Msamaria mwema, anayejitolea kumsaidia mhitaji bila kuangalia tofauti zao kama inavyokaziwa katika Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko "Fratelli tutti": Yaani “Wote ni Ndugu”: Kuhusu Udugu na Urafiki wa Kijamii. » Mfungo unaoambatana na huduma kwa wahitaji ni njia ya kushinda tofauti zetu na vishawishi vinavyoambatana na tofauti hizo.

Kwa hiyo, tunaalikwa katika kila hali tuliyonayo tushiriki mfungo huu wa Kwaresima kwa malengo ya kuhuisha maisha yetu ya kiroho na kujiweka karibu zaidi na Mungu.

Hatua za kuchukua ili tuweze kufanya vema mapinduzi ya kiroho, toba na wongofu wa ndani.
Tukubali kwamba sisi ni wadhambi. Tusipokubali kuwa tu wadhambi hatutaona hitaji la kufanya toba na kubadilika. Ndiyo maana kwaresima lazima ianze kwa tendo la kupakwa majivu hadharani ili kukubali na kukiri hadharani kuwa tu wadhambi na tunahitaji kufanya toba.

Sala, kufunga na matendo ya huruma ni mambo matatu ambayo tunahimizwa kuyafanya katika kipindi hiki cha Kwaresma. Yesu anatuangalisha kuwa, ili tuweze kufaidika kutokana na sala, matendo yetu ya huruma, na kufunga kwetu, tuondokane na unafiki. Mnafiki ndiye mdhambi pekee ambaye Yesu alimkemea hadharani bila kusita; huu ndio ufarisayo.

Tusianze kipindi hiki cha Kwaresima kwa mazoea. Tukiingie kipindi hiki kama vile ni cha kwanza na cha mwisho katika maisha yetu. Tuitumie kwaresma hii kana kwamba hakuna tena Kwaresma nyingine. Kwa hakika hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kuiona Kwaresma nyingine.

Mtume Paulo anatukumbusha kwamba kipindi cha Kwaresma ndio wakati uliokubalika, siku ya wokovu ndiyo sasa. Tusisubiri wakati mwingine. Tukitumie vema kipindi hiki. Nawatakieni nyote mwanzo mwema wa kipindi cha Kwaresma
 
Kwaresma Countdown 🕜
2nd Day 👼

FB_IMG_16770484051035477.jpg
 
Siku ya Ijumapili. Leo ni mapumziko hua hatufungi Kwaresma.
Why??
Tunaadhimisha ufufuko na kufufuka kwa Bwana yetu Yesu kristo kila Ijumapili.

#Kwa wasiofahamu.
 
Back
Top Bottom