Kwaresma na Pasaka Special Thread

Kwaresma na Pasaka Special Thread

View attachment 3259835

IFANYE KWARESMA 2025 KUWA YA TOFAUTI KIROHO

πŸŸͺπŸŸͺ Kwaresma ni kipindi maalum sana kiroho, ni safari ya kwenda nyikani na Bwana Yesu kwa muda siku 40.

πŸŸͺπŸŸͺ Kipokee kipindi hiki kama fursa ya Kiroho kwani ni kipindi cha kufunga, Kusali, Kutubu, na Kufanya matendo ya Huruma kwa wahitaji.

πŸŸͺπŸŸͺ Jiandae kiroho kwa kufanya toba halisi.

πŸŸͺπŸŸͺ Usiingie kwenye mfungo huu maalum ukiwa moyo wako una makwazo ama manung'uniko yeyote achilia kila jambo lililo gumu na ubaki huru.

πŸŸͺπŸŸͺ Weka nia maalum ya mfungo kwa kutenga na kumwambia Mungu akupe msaada hasa changamoto nzito na ngumu ambazo kwa upande wako unaziona huziwezi.

πŸŸͺπŸŸͺ Kama huna changamoto yeyote ya kiafya mfano kama si mjamzito ama husumbuliwi na ugonjwa wowote tafadhari jinyime kwa kutokula chakula.

πŸŸͺπŸŸͺ Usifunge kwa kujionyesha kwa watu kwamba na wewe umefunga, funga kwa kusudi ama nia uliyoikusudia ili Mungu akupe msaada wake.

πŸŸͺπŸŸͺ Kumbuka kipindi hiki hutokea mara moja tuu kwa mwaka hivyo ifanye kama fursa ya kiroho ambayo mara tuu baada ya kumaliza mfungo utavuna na kujiwekea akiba kubwa ya kiroho.

πŸŸͺπŸŸͺ Uwapo kwenye mfungo waombee na watu wengine kwani ukifanya hivyo Mungu atapokea maombi yako haraka na kwa urahisi.

πŸŸͺπŸŸͺ Saidia wahitaji hasa kwenye kipindi hiki cha Kwaresma, watu wote Mungu amewaumba kwa mfano wake hivyo unavyowasaidia tambua kwamba unagusa mboni yake.

πŸŸͺπŸŸͺ Omba kwa imani na Mungu ataisikia sauti yako

πŸŸͺπŸŸͺ Omba kwa kumaanisha na Mungu ataenda kukutendea sawa sawa na mapenzi yake

πŸŸͺπŸŸͺ Safari hii ya siku 40 itakuwa ni historia kwenye maisha yako kwani ukifunga na kuomba kwa imani Mungu ataenda kuruhusu mambo makuu mnoo yatendeke maishani mwako.

πŸŸͺπŸŸͺ Nakutakia Mfungo mwema wa Kwaresma na Mungu akubariki sana πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
AMINA ila Mimi najuaga kuwa wewe ni msabato
 
AMINA ila Mimi najuaga kuwa wewe ni msabato
Nilizaliwa na kulelewa katika Ukatoliki. Ujana nikaupitishia katika Usabato. Utu uzima niliokoka na kuwa mlokole pyua. Na sasa uzeeni (78) nimerudi tena kuumalizia mwendo katika Usabato.

Yote kwa yote Mungu ni yule yule ati!

Kwaresma njema! πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Tusali rozary takatifu ya mama wa Fatma
Jumatano matendo ya utukufu

Tendo la kwanza
YESU anafufuka,(Luka 25:5-7) tumuombe MUNGU atujalie kugeuka watakatifu
Tendo la pili
YESU anapaa mbingun,(matendo ya mitume 1:8-9)tumuombe MUNGU atujalie kwenda mbingun
Tendo la tatu,
ROHO mtakatifu ana washukia mitume, (matendo ya mitume 2:1-4)tumuombe MUNGU atujalie bidii katika dini yetu
Tendo la nne,
Bikira Maria anapalizwa mbingun, (ufunuo 12:1)tumuombe MUNGU atujalie kufa vizuri
Tendo la Tano,
Bikira Maria anawekwa malikia mbingun, (ufunuo 3:21) tumuombe MUNGU atujalie kudumu katika njia njema
 
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
1, kufariji (mfariji) ROHO MTAKATIFU ni nafsi ya tatu ya MUNGU lakin ROHO huyu hupelekwa kwa ajili ya kuwafariji wamtumainia BWANA

Hakuna mfariji wa kweli kama ROHO MTAKATIFU

Namtuma ROHO huyo akawe nawe akakufariji katika maisha yako ya sasa na yajayo akawe chanzo cha furaha katika maisha yako sasa na hata milele
AMINA
 
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
2, ni ufunuo wa MUNGU kwa watakatifu wake (hutufunulia yajayo)waefeso 3:4-5 , 1 wakorintho 2:14
Ukimtumia ROHO MTAKATIFU ipasavyo huwezi tembea gizani kamwe, utakuwa nuruni milele, atakuonesha ufanye nini na usifanye nini, atakuonesha utembee na yupi na usitembee na yupi, atakuonesha uende wapi na lini na atakuonesha usipende wapi na kwanini usiende

Basi tujitakase ROHO MTAKATIFU akae nasi akatufunulie kesho yetu ijayo

Namtuma ROHO huyo
Pokea ROHO MTAKATIFU kwa jina la YESU KRISTO
 
KAZI YA NENO LA MUNGU
1, ni upanga hupiga adui (waefeso 6:17)
Mtumish wa MUNGU, ukiwa na adui yako ana kusumbua hata usihangaike naye, ishi tu katika NENO sawa sawa hakika utamwona adui yako akipigwa kwa macho yako

Tuendelee kulitumia NENO sawa sawa ili BWANA YESU KRISTO akae nasi
Nami nautuma upanga huo ukapiga adui zako(zaburi 91), zaburi 37
 
Sisi ni mavumbi
 

Attachments

  • Screenshot_20250306_085809_Instagram.jpg
    Screenshot_20250306_085809_Instagram.jpg
    195.1 KB · Views: 1
Nilizaliwa na kulelewa katika Ukatoliki. Ujana nikaupitishia katika Usabato. Utu uzima niliokoka na kuwa mlokole pyua. Na sasa uzeeni (78) nimerudi tena kuumalizia mwendo katika Usabato.

Yote kwa yote Mungu ni yule yule ati!

Kwaresma njema! πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
Kuna kipindi flan nilipitia huko kwenye usabato, nyakati flani bado sijaweza kujipambanua na kupambanua Mambo
Nilikuwa nikikutana na hawa wasabato wanatema mbovu sana juu ya kanisa hadi nikawa naogopa, lakin baada ya kukua nikagundua ukweli mpaka leo niko huku kwetu

Yote kwa yote ubalikiwe sana ndugu yangu

Lakin hiyo miaka 78 umeifikisha lini?
 
KANUNI YA IMANI

Nasadiki kwa MUNGU baba MWENYEZI, muumba wa mbingu na Dunia, na kwa yesu KRISTO mwanawe wa pekee, BWANA wetu, aliyetungwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU, akazaliwa na bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya ponsyo pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu, siku ya tatu akafufuka katika wafu, akaa paa mbingun, amekaa kuume kwa MUNGU BABA MWENYEZI, toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu, nasadiki kwa ROHO MTAKATIFU, kanisa takatifu mkatoliki la mitume, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miwili na uzima wa milele. AMINA
 
Back
Top Bottom