Kwaresma na Pasaka Special Thread

Kwaresma na Pasaka Special Thread

SALA YAKUJIOMBEA ILI KUACHA MATENDO MAOVU
Mungu Mwenyezi, asante kwa kunipenda ingawa sijakamilika. Ninapambana na hali hii (itaje) na kadiri ninavyotaka kuacha, ninaendelea kurudi nyuma. Ninahisi aibu na uchovu. Ni Wewe pekee unayeweza kunisaidia kupambana na hali hii ili niweze kuacha. Niponye ndani na nje. Ikiwa kuna kitu chochote moyoni mwangu kinachonizuia kusonga mbele, nifunulie na unioneshe jinsi ya kukabiliana nacho. Ondoa hofu moyoni mwangu na unijaze nguvu ili niendelee kutembea katika roho na kweli. Amina.
Watakatifu Mikaeli, Gabrieli na Rafaeli malaika wakuu. Mtuombee.
 
Tusali malaika wa BWANA

Malaika wa BWANA alimpasha habari Maria naye akapata mimba kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU, salaam maria................
Ndimi mtumish wa BWANA nitendewe ulivyonena, salaam maria.................
Neno la MUNGU akatwaa mwili akakaa kwetu , salaam maria..........
Utuombee mzazi mtakatifu wa MUNGU tujaliwe ahadi za KRISTO
Tuombe...... Tunakuomba ee BWANA utie neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika kwamba kristo mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe utukufu na ufufuko wako. Tunaomba yote hayo kwa njia ya kristo BWANA wetu. AMINA
 
Rozary takatifu matendo ya uchungu

Siku ijumaa
Tendo la kwanza.
YESU anatoka jasho la damu, (Mariko 14:36) tumuombe MUNGU atujalie sikitiko la dhambi

Tendo la pili,
YESU anapigwa mijeledi, (Mariko 15:14-15)
Tumuombe MUNGU atujalie kuacha dhambi za uchafu

Tendo la tatu,
YESU anatiwa taji la miiba kichwani,(Mariko 15:16-17)
Tumuombe MUNGU atujalie kushinda kiburi

Tendo la nne,
YESU anachukua msalaba wake, (YOHANA 19:17-18)
Tumuombe MUNGU atujalie kuvumilia taabu

Tendo la Tano,
YESU anakufa msalabani, (yohana 19:30)
Tumuombe MUNGU atujalie kuwapenda YESU na maria
 
Hongera sana chief,pepo unayo mkononi kwa kujua kwako kufunga kwa imani yako but kama unadhani Mungu anapima kwa mzani mdogo kama huu wewe ndiye unayeshinda njaa.
Huyu anataka atuweke kwenye mashindano ya kufuturu
 
View attachment 3259835

IFANYE KWARESMA 2025 KUWA YA TOFAUTI KIROHO

🟪🟪 Kwaresma ni kipindi maalum sana kiroho, ni safari ya kwenda nyikani na Bwana Yesu kwa muda siku 40.

🟪🟪 Kipokee kipindi hiki kama fursa ya Kiroho kwani ni kipindi cha kufunga, Kusali, Kutubu, na Kufanya matendo ya Huruma kwa wahitaji.

🟪🟪 Jiandae kiroho kwa kufanya toba halisi.

🟪🟪 Usiingie kwenye mfungo huu maalum ukiwa moyo wako una makwazo ama manung'uniko yeyote achilia kila jambo lililo gumu na ubaki huru.

🟪🟪 Weka nia maalum ya mfungo kwa kutenga na kumwambia Mungu akupe msaada hasa changamoto nzito na ngumu ambazo kwa upande wako unaziona huziwezi.

🟪🟪 Kama huna changamoto yeyote ya kiafya mfano kama si mjamzito ama husumbuliwi na ugonjwa wowote tafadhari jinyime kwa kutokula chakula.

🟪🟪 Usifunge kwa kujionyesha kwa watu kwamba na wewe umefunga, funga kwa kusudi ama nia uliyoikusudia ili Mungu akupe msaada wake.

🟪🟪 Kumbuka kipindi hiki hutokea mara moja tuu kwa mwaka hivyo ifanye kama fursa ya kiroho ambayo mara tuu baada ya kumaliza mfungo utavuna na kujiwekea akiba kubwa ya kiroho.

🟪🟪 Uwapo kwenye mfungo waombee na watu wengine kwani ukifanya hivyo Mungu atapokea maombi yako haraka na kwa urahisi.

🟪🟪 Saidia wahitaji hasa kwenye kipindi hiki cha Kwaresma, watu wote Mungu amewaumba kwa mfano wake hivyo unavyowasaidia tambua kwamba unagusa mboni yake.

🟪🟪 Omba kwa imani na Mungu ataisikia sauti yako

🟪🟪 Omba kwa kumaanisha na Mungu ataenda kukutendea sawa sawa na mapenzi yake

🟪🟪 Safari hii ya siku 40 itakuwa ni historia kwenye maisha yako kwani ukifunga na kuomba kwa imani Mungu ataenda kuruhusu mambo makuu mnoo yatendeke maishani mwako.

🟪🟪 Nakutakia Mfungo mwema wa Kwaresma na Mungu akubariki sana 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Tunaomba mafundisho zaid

Achen kukata tamaa tunaosoma ni wengi sana
 
Kesho mapema ibada ya majivu.

Tuombeane kwa Mungu azipokee toba zetu madhaifu na tabia mbovu tulizozoea kuziishi huko nyuma Kwaresma hii ikaziondoshe kwetu tubaki wasafi hata milele.
Tubun na kuiamin injili
 
Amani iwe kwenu watumishi wa MUNGU katika kristo YESU

Tumsifu YESU KRISTO. AMINA

Tumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo hasa kwa kumtuma mwanae aje atukomboe . AMINA

PASAKA ni nini pasaka ni kuteseka/mateso/ kifo/kufa/na kufufuka kwa YESU KRISTO

PASAKA ilianzia misiri lakini badae wana wa Israel MWENYEZI MUNGU aliwaagiza waadhimishe pasaka kama kumbukumbu la kwamba wao walikuwa watumwa wa mateso huko misiri

Hivyo wakristo kwa sasa huadhimisha pasaka kama kumbukumbu la kwamba TULIKUWA WATUMWA/ WAFUNGWA WA MINYORORO YA SHETANI mpaka pale BWANA wetu YESU KRISTO alipokuja kutukomboa kwa mateso yake makali pale msalani

Je kwaresma ni nini, kwaresma ni ibada ni ibada ambayo husindikizwa na mfungo wa siku 46 kutoa Dominika 6 hivyo siku hubaki 40

Kufunga kwaresma ni kufanya nini, kufunga ni kuyakalibisha mateso ya YESU KRISTO ambaye ni mfufua wa ulimwengu wote

Hivyo wewe uliyefunga unapaswa kuwapikia wengine ambao hawajafunga na kutoa pesa yako iliyopaswa kula ili uwalishe ndugu na watu Baki

Lakin ndugu zangu kufunga bila sala huko ni kushinda NJAA kabisa
Kufunga bila kunuia jambo flani huko nako ni kushinda NJAA kabisa

Lakin pia kwaresma huanza na jumatano ya MAJIVU

MAJIVU ni nini, MAJIVU hutukumbusha kwamba sisi wanadamu ni mavumbi na mavumbini hakika tutarudi

Masomo husika yoel 2:12-18
Injili husika mathayo 6:1-6,16-18

Moderate tafdhari nawaomba uzi huu msiuunganishe maana uzi utakuwa wa milele kwa update za kila siku juu ya neno la MUNGU la kipindi cha kwaresma

Basi nawakaribisha tufunge na tumuombe MUNGU wetu aliye mwema sana

SAYUNI BOY

Naomba kuuliza kama ifuatavyo!:!.
1️⃣ Je kwaresma ipo kwa madhehebu yote ya kikristo / kikristu au ni special kwa wakatoliki peke yao?
2️⃣ Je makanisa au madhehebu yote yanayoadhimisha kwaresma ni lazima kujichora misalaba myeusi kwenye mapaji ya uso au hili ni kwa wakatoliki peke yao?
Nauliza hivi kwa sababu siku moja nilikuwa naongea na dada mmoja msabato akasema kwenye usabato hawana sikukuu ya krismas wala pasaka ila sikukumbuka kumuuliza kuhusu kwaresma kama kwenye usababato ipo au haipo?!
 
Naomba kuuliza kama ifuatavyo!:!.
1️⃣ Je kwaresma ipo kwa madhehebu yote ya kikristo / kikristu au ni special kwa wakatoliki peke yao?
2️⃣ Je makanisa au madhehebu yote yanayoadhimisha kwaresma ni lazima kujichora misalaba myeusi kwenye mapaji ya uso au hili ni kwa wakatoliki peke yao?
Nauliza hivi kwa sababu siku moja nilikuwa naongea na dada mmoja msabato akasema kwenye usabato hawana sikukuu ya krismas wala pasaka ila sikukumbuka kumuuliza kuhusu kwaresma kama kwenye usababato ipo au haipo?!
Asante sana kwa swali zuri

Kwaresma ipo kwa ajili ya watu wote lakini si kwa kila mtu

Baadhi ya madhehebu huamisha kwaresma kwa ukubwa kama Lutheran, Anglican, catholic, Moravian na mengine mengi lakini siyo yote, madhehebu mengine hupinga kwaresma kwa sababu ambazo wanazijua wao

Kupaka MAJIVU usoni ni thehebu ya Catholic pekee ndo hupaka MAJIVU uson, Sina uhakika kama na Lutheran nao hupaka majivu

Hao watu wanaoitwa wasabato achana nao wao ni wapinga KRISTO na wako wazi wala hawajifichi
 
Asante sana kwa swali zuri

Kwaresma ipo kwa ajili ya watu wote lakini si kwa kila mtu

Baadhi ya madhehebu huamisha kwaresma kwa ukubwa kama Lutheran, Anglican, catholic, Moravian na mengine mengi lakini siyo yote, madhehebu mengine hupinga kwaresma kwa sababu ambazo wanazijua wao

Kupaka MAJIVU usoni ni thehebu ya Catholic pekee ndo hupaka MAJIVU uson, Sina uhakika kama na Lutheran nao hupaka majivu

Hao watu wanaoitwa wasabato achana nao wao ni wapinga KRISTO na wako wazi wala hawajifichi
Mh! aisee!
Kipengele kinachosema " kwaresma ipo kwa ajili ya watu wote lakini si kwa kila mtu " sijakuelewa! " Kwa ajili ya watu wote " kivipi ?! Hadi wapagani ?! Halafu si kwa kila mtu kivipi wakati ni kwa ajili ya watu wote ?! Kitu kikiishakuwa ni kwa ajili ya watu wote si tayari kinakuwa ni kwa kila mtu ?! Watu wote ndiyo kila mtu !
 
Jumamos ya jumuiya

Masomo jumuiya ya leo
Isaya 58:9-14
Luka 5:27- 32
Zaburi 86:1-6
 
Back
Top Bottom