KWELI? Dunia imeanza kuzunguka haraka zaidi, sekunde moja kufutwa mwaka 2029

Ibilisi Mjalaana

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2019
Posts
8,297
Reaction score
16,529
Shalom shalom

Wanasayansi wanasema Dunia yetu imeanza kuzunguka kwa kasi zaidi kuliko kawaida. Kwa kawaida, Dunia huchukua sekunde 86,400 kumaliza mzunguko mmoja (siku moja kamili). Lakini hivi sasa, kasi hiyo imeongezeka kidogo sana, kiasi kwamba siku moja inaweza kuwa sekunde chache fupi kuliko kawaida.

Hali hii imefanya wataalamu wa muda (timekeepers) kupendekeza kuondoa sekunde moja kwenye saa za dunia ifikapo mwaka 2029 – jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia!

Kwa kawaida, tumekuwa tukiweka "leap second" (sekunde ya ziada) kila baada ya muda fulani kulinganisha saa za atomu na mzunguko halisi wa Dunia. Sasa, kwa mara ya kwanza, sekunde itaondolewa badala ya kuongezwa!

Hii inamaanisha siku hiyo moja saa itaruka moja kwa moja kutoka 23:59:58 hadi 00:00:00, bila kupitia 23:59:59.

Swali ni: Hili linaweza kuathiri vipi mifumo yetu ya teknolojia? Na kuna athari yoyote kwa maisha ya kila siku?

Karibuni tujadili.
 
Weka chanzo Cha hii taharifa
 
Back
Top Bottom