Kweli hali ni mbaya, majirani wamenichinjia baharini

Kweli hali ni mbaya, majirani wamenichinjia baharini

Tuna mazoea kila sikukuu kupelekeana chakula .ikiwa ya upande wa dini yangu basi lazima hotpot ziende kwa jirani wa kaskazini na nyingine kusini.sasa Leo nimesubiria kwa hamu nikajua lazima hotpot zitakuja nifaidi kwa hiyo mchana sikuhangaika kabisa na chakula
Kila nikiskia mlango unagongwa nawahi kwa bashasha ila kutoka nje hakuna msosi uliokuja.nimetumia mbinu kibao lakini wapi.nikasema labda wamenisahau ,nikamtuma dogo nikijidai nawapa taarifa za Kenya uchaguzi kurudiwa ili tu wanikumbuke.mbinu hiyo pia ikagonga mwamba.uzalendo ukanishinda mida ya sa kumi ikabidi nijipitishe labda watanikumbuka.pia hiyo nayo imegonga mwamba.sasa kama wamefuta mkataba kwa nini wasingeniambia .Dah mtaani kweli hali mbaya .Baba J legeza kidogo baba
Pole sana mkuu

Huku nilipo nililetewa hotpot tatu na hapa yaani hata moja sjaimaliza nyingine mbili zmejaaa

D.A "Mwanaume mashine"
 
Back
Top Bottom