Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Kuna daktari mmoja hapa mtaani ana ka pharmacy kake kadogo ka mchongo ambako hutumia muda wa jioni kusogezea siku. Basi bhana, ikabidi nikaonane naye kutokana na masuala mazima ya ushauri nasaha kuhusu matumizi ya pombe yaliyokithiri yaliyosababishwa na homa ya mapenzi
Wakati nilikuwa nikipata mawili matatu, ndipo mteja kuingia, akazungumza na daktari kuwa anahitaji PrEP, baada ya kuondoka ndipo nikamuuliza daktari kuwa PrEP ndo PEP maake naona mteja kataja ndivyo sivyo. Daktari ndipo kunielewesha kuwa PrEP ni opposite ya PEP, na PrEP ni vidonge anavyomeza mtu ndani ya masaa 2 kabla ya kufanya mapenzi na mpenzi anayekisiwa huenda akawa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI
Itoshe tu kusema watanzania tuna mioyo migumu sana, unaanzaje kufanya mapenzi na mtu mwenye VVU bila kinga kwa kigezo cha eti unatumia PrEP?