Kweli nchi inaibiwa lakini maendeleo tunayaona kwa watu

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,298
Hii bora iende... Ndio, sababu hatuna namna.
Toka mama ameingia kumekuwa na mabadiliko mengi sana. Tofauti na mtangulizi wake JPM. Magufuli alibinya pesa mikononi kwa wananchi lakini tukaona maendeleo ya serikali kupitia miradi mingi(sina haja ya kutaja sababu inaonekana).

Mama amekuja amefungua nchi, nchi imefunguka kweli wanachi nao tumefunguka hatujalala. Kwa sasa hakuna miradi mipya ya kimkakati lakini watu wameendelea sana. Nimejuaje? Angalia maeneo mengi watu wanajenga na kufungua biashara mpya, watu wanapiga hela sana. Majumba makali yanazidi kujengwa magari, na ujenzi kila kona ya nchi. Hiki ndio kipindi cha fursa hakuna kuzubaa tena.

Changamoto iliyopo matajiri wanazidi kupaa huku wanyonge wakizidi kunyonywa. Hongera sana mama etu Samia.
 


Tunapigwa Kama Ngoma ​

Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na Masikioni
 
Hiyo kusema watu wanajenga majumba kwa sababu mama amefungua nchi nadhani ni uwongo unaoenda kuwa ukweli maana kila mtu anasema hivyo!

Hakuna kitu kama hicho still wapo walioshindwa kujenga wakati wa Kikwete wakaja kujenga wakati wa Magufuli na wapo walioshindwa kujenga wakati wa Magufuli watajenga wakati huu na utashangaa zaidi hata baada ya huyu wapo watakaokuwa hawakujenga so mama has nothing to do kuhusu hili.
 
Kwani wakati wa magu matajiri na masikini walikuwa sawa? Kuna majina haya tajiri masikini lazima makundi haya yawepo tu
 
Mama anaupiga mwingi.
 
Waliojenga wakati wa magufuli hawa walijenga kihalali kabisa hawakuwa na kasoro kwenye mishe zao
 
Kwani wakati wa magu matajiri na masikini walikuwa sawa? Kuna majina haya tajiri masikini lazima makundi haya yawepo tu
Tajiri alikuwa anaishi kwa wasiwasi kuliko masikini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…