Kweli Ndoa yataka Moyo.....

Huyo mumeo anatakiwa aheshimu ndoa. Aliahidi kukupenda wewe tu kwenye shida na raha. Mkumbushe kwa kuangalia picha za harusi yenu na video kila mnapokuwa pamoja. Hata usipomwambia kwa maneno, hayo matendo ya kumwonyesha harusi yatamuuma kama kwelia anasaliti
 
Thanks snowwhite....
 
SUbiri tu uone..
Wewe si umeona mwenzio anavyolia hapa..
hata mimi x wangu ni rafiki yangu saaanaaaa........
mwanzo hakuamini kama sitaweza kumpa kitu baadae kakubali matokeo, maana nilimwambia kabisa siwezi kwenda beyond stories...... kama anataka zaidi ni bora tusiwasiliane kabisaaaa, kila mtu aishi kwa amani nyumbani kwake. akiangalia hawezi kunipoteza, maana namsaidia sana kwa maushauri na kila kitu..... in fact hata kwenye kuijenga ndoa yake ambayo ilikuwa inayumba mara kadhaa...... tumebaki kuwa marafiki na hakuna feelings zozote (to me)
 
Usivumilie kwa kukaa kimya, utakonda kwa mawazo wakati wenzio wanainjoi, pambana mdogowa wangu, kama umeongea na mumeo imeshindikana nenda kwa wasimamizi wa ndoa yenu watamwita na watawashauri vzr tu ikishindikana nenda kwa wazazi wake.

Mumeo nae, sijui kwanini anashindwa kujiheshimu, kama alimpenda huyo dada kwanini hakumuoa? amenikeraa

asante kwa ushauri najitahidi kuvumilia ila roho inaniuma sana
 
 
mummy, the best way ya kumtreat mume wa hivyo, endelea kumpenda, kumheshimu na kumuombea. usientertain any communication na huyo mke wa nje, atakuumiza tu, maana anafurahi kuona wewe unaumia. je yeye hajaolewa?
 
"An eye for an eye will make the whole world go blind." - M. Ghandi



Ukishaamua kuoa/kuolewa lazima uwe tayari kuachana na yote hayo! Ukiona huwezi basi hujafikia wakati wako..tatizo tunaoa/kuolewa kwa kuangalia umri.

vishawishi vingi plus kufosiwa kufunga ndoa ndo usiseme
usikute huyo mwanamke alilazimisha ndoa na si mapenzi ya mwanaume mwenyewe
 
 
Mkuu nakukubali kwa ushauri wako na naamini uko sahihi,nakiri kuwa nitaplay my part as a married wife na daima kuwa upande wa mume wangu but i wont allow tena huyo EX aitese ndoa yangu,naamini ntachukua hatua yakinifu katika kulitatua hili tatizo....
 
Reactions: Mbu
FP mambo!
Huyo wa kwako inawezekana ni muelewa, kwa bidada hapa kinachokera kwanini mwanaume anaruhusu huyo mwanamke wake amtukane mkewe, hata kama bado wanamahusiano na huyo ex wake basi wafanye kwa siri ili asimuumize mdada wa watu

 
mummy, the best way ya kumtreat mume wa hivyo, endelea kumpenda, kumheshimu na kumuombea. usientertain any communication na huyo mke wa nje, atakuumiza tu, maana anafurahi kuona wewe unaumia. je yeye hajaolewa?
ukweli ni kwamba yeye bado hajaolewa ila naskia anabwana...
 
Bi dada pole jamani,mmeo anaweza kuwa anafanya hivyo,
1.Ni mkakati waliousuka ili ukereke na uamue kukimbia halafu wao waoane.anataka wewe ndio uanze ili kujivua lawama kwa ndugu wa pande zote mbili.
2.inawezekana ikawa kweli manjonjo anayopata upande wa pili yakawa zaidi yako ila mmeo ni limbukeni hakupaswa kukufanya wewe ujue.usione ndoa zimesimama ukafikiri uko mwenyewe wee!nyumba ndogo ni nyingi kupita maelezo ila kinachofanyika ni kutomkera mke wa ndani hadi ajue kuwa kuna mwengine nje.
3.MLILIE MUNGU,MAOMBI NI SILAHA YAKO YA MWISHO washirikishe wadada, wamama mwekeni mwaume huyo mbele za Mungu usisahau maombi ya kufunga yana nguvu zaidi.
 
mumeo kuna kitu anakikosa kutoka kwako kaa chini uongee nae vizuri
 
Mshauri mume wako akate mawasiliano kabisa na huyo cd maana ni mwaribifu na huyo mumeo anamatatizo sana kama itashindikana wahushe wazazi wake huyo jamaa!
 
Hongera sana kwa kuwa imara na kudhibiti na kuweka mipaka ya mahusiano na mawasiliano na EX wako ambayo hayana athari zozote katika uhusiano wako...pia hongera kwa kuwa na ex mstaarabu...hapa tatioz ni kwamba ex wa mume wa mimi naona ustaarabu kwake ni kitendawili
 

I concur with you guys! Gfsonwin msaidie huy dada natumaini ukiwa naye kwa karibu atavuka mlima huu!! barikiwa gfsonwin
 
Pole sana dada,inaonekana huyo mumeo anshindwa kufanya uamuzi mgumu wa kumweleza huyo ex-wake juu ya kuheshimu ndoa yenu,pia huyo dada hana adabu,kwani kutembea na mume wa mtu ndo atoe siri,ina maana hata angekuwa na mume wake angekuwa anaanika yale yote wanayoyafanya kwenye mitandao?kwenye mitandao watu tunasaidiana tu kwa mawazo lkn huwezi anika siri za kitandani kwako kama wewe ni mtu una akili timamu.huyo mumeo angekuwa na akili nzuri leo leo angempiga chini kwani ipo siku atamdhalilisha kwa kumtoa picha za uchi ambazo atakuwa amempiga kwa kujua au kutokujua,kwani hapo anatembea na zuzu.
Wewe mpiganie mumeo kwa Mungu kwa maombi na kufunga hasa kipindi hiki cha kwaresma naye atakujibu.
 
FP mambo!
Huyo wa kwako inawezekana ni muelewa, kwa bidada hapa kinachokera kwanini mwanaume anaruhusu huyo mwanamke wake amtukane mkewe, hata kama bado wanamahusiano na huyo ex wake basi wafanye kwa siri ili asimuumize mdada wa watu
poa kabisa ram.....
mimi nilichoongelea ni kitendo cha kuwa na mawasiliano na x na si vinginevyo. na kama kitu napinga ni kuendelea na mahusiano na x, hiki sitakuja kukifanya na namwomba Mungu wangu azidi kunisaidia. hata pale ninapokuwa down, x haji kabisa katika akili yangu ingawa nipo naye karibu sana na najua angefurahi sana angepata hiyo nafasi.
hayo ya kutukana ni habari nyingine. kuna wadada wapo hivyo, sijui kwa nini wanafanya hivyo. kuna siku nilipokea simu usiku wa manane namba ni ya mkaka ninayemfahamu, niliogopa sana maana nilijua anaweza akawa na tatizo, siyo kawaida kupiga usiku ule. nilipopokea akaongea mdada na kuanza kunishushia matusi niachane na BF wake. kwa hasira nikakata simu nikalala. nikapanga asubuhi nimshushie moto wa haja huyo kaka. kabla sijaamka asubuhi nikapigiwa simu na rafiki yangu sana (mdada), mimi naye wote tulikuwa kwenye phonebook ya simu ya yule kaka, mdada kanipigia kunipa story ya yaliyonitokea usiku...... nikajua hapa kuna shida. nikasema sitampigia yule kaka, nilielewa yaliyompata. baadae akatutumia msg kutuomba msamaha. kumbe yule dada usiku aliiba simu ya BF wake, akapigia simu wadada woote waliokuwa kwenye ile simu kwa kutumia namba ya yule kaka..... hapo unaweza kupata picha huyo ni kichaa wa design gani....
 
Reactions: ram
soma post yangu # 119, huyo dada si mstaarabu kwa namna yoyote ile. na kama unataka amani acha kabisa kupoteza nguvu zako kwake, deal na mumeo, kama atakusikia poa. huyo dada ni kichaa kabisa wala usiumize kichwa chako kumuwazia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…