Kweli Ndoa yataka Moyo.....

Kweli Ndoa yataka Moyo.....

Ndugu zanguni yamenikuta na naomba ushauri wenu,Mimi ninaishi na mume wangu yapata miaka miwili sasa,nina mpenda sana Mume wangu na ninaamini kuwa naye ananipenda pia.Ila kuna tatizo linanisumbua sana juu yake ambalo linanipa wasiwasi kiasi kwamba nashindwa kuelewa hatma ya mahusiano yetu ya ndoa kwa maana ya kwamba nahofia yasije yakaingia shubiri na ile imani nlionayo juu yake ikateteleka.Ni hivi kabla ya kunioa mimi aliwahi kuwa na mahusiano na wanawake wengine ila mwanamke wa mwisho ambaye aliachana nae amekua akiendelea kuwasiliana na mume wangu na kila ninapohoji juu ya hilo Mume wangu hunijibu kuwa hauna kitu kinachoendelea baina yetu ni rafiki yangu tu wakawaida na hana shida yoyote na sisi kwanza huwa anapiga simu na kutuma meseji za kutujulia hali,anyways nimejitahidi sana kuwa na mtizamo chanya na kuuambia moyo wangu uamini hivyo.Ila siku zinavyokwenda nikaona mazoea yanakua sio mazuri kwa maana wakati mwingine humpigia simu ana hutuma meseji humueleza mume wangu kuwa amemmiss sana na anataka kuonana nae na vitu kama hivyo.Nlimwambia mume wangu mawasiliano na huyo mpenzi wako wa zamani hayanibariki hata kidogo naomba uwe na mipaka na ikibidi uache kwa maana yananiumiza mimi zaidi,aliniahidi kufanya hivyo na kweli kwa kipindi fulani kazi ilipungua ila sasa leo ametuma tweets kuhusu mume wangu kwenye mtandao wa twitter kitu ambacho kimeniuma maana anaeleza jinsi anavyofurahia tendo la ndoa na mume wangu na baada ya kuliona hilo nkampigia mume waqngu kumweleza akaniambia atampigia simu kumsema juu ya hilo na kumuonya.Badala yake kilichotokea yule mwanamke alituma tweets za kunitukana na kunidhalilisha mimi kitu ambacho kinaniuma sana kwa maana mume wangu anasema yule mwanamke ni rafiki mzuri tu na hana shida hata kidogo.Nisaidieni ushauri ndugu zangu je niendelee kuvumilia hayo yote yanayojitokeza na kuamini maneno ya mume wangu kuwa huyo mwanamke hana shida na sisi ama nifanyenye?Naomba ushauri wenu katika hili.....

Kwa hatua iliofikia huenda umechelewa kiasi kuomba ushauri, kwa kuwa sasa utapaswa kutumia nguvu uweze kuweka mambo kwenye mstari.
1. Inapotokea swala kama hili la sms n.k unapaswa kuwa na msimamo, yaani onyeshwa kukerwa, na unapo uliza weka ule u dear kando; kuwa serious na usikubaliane na majibu mepesi. Ikibidi mwambie achague moja.
2. Lilipofikia nadhani unapaswa kuwahusisha wazee/viongozi wa dini unayoabudu, waeleze A-Z bila kuficha chochote.

Ukilichukulia mzaha swala hili mwisho wake litakuja kuleta athari kubwa sana kwako na familia yenu kwa ujumla.
 
im honored mpenzi!
mi hapa huwa pananishangaza kweli!ndo mana naumia sana mtu akibaki kujikunyata na kuamini kuwa uzinzi wa mume au wa mkewe ni kwa kuwa yeye mke au mume ana mapungufu mahali!
ushawahi kuwa na kila kitu kiasi cha kutamani the opposite? sasa ndo hii!

Unajua jamii hasa ya wanawake ndio inayowafanya wanawake wengi wajione wanyonge na ni fault yao kila wanaume wanavyocheat; it is so sad kwa kweli maana kwa mtazamo wangu mtu ana cheat kwakuwa ameamua kwani there is always another way out of any situation or problem.
BTW hata wanaume pia hunyong'onyea pale wake zao wanapowasaliti na kujiona wana mapungufu fulani. Which is wrong, kwa maana kwamba as long as umeamua kuwa na mimi na mapungufu yangu basi unapaswa kuwa na mimi, kama huwezi the door is always open. You cant eat your cake and still have it! If you arent ready for commitment then dont commit yourself; as mapungufu (iwe nguvu za kiume, au mvuto kupungua) are as sure as sunshine!
 
Huwa narefer story yako kila ninapokumbana na issue kama hizi; and l think, ilikutokea hiyo ili uweze kuwasaidia wengine wenye shida za namna hiyo.
Basi once again, nakuomba; nenda naye another stage further, akupe contacts zake uendelee kumjenga zaidi (simu etc). She seems to be somewhat naive and too nice (jinsi hata anavyojibu post "......nimekuelewa nitafanyiakazi...." sort of majibu) so she need a strong woman like you to mentor her.
sitaki kukwambia pole, ila nataka kukwambia kwamba hakuna maisha ambayo hayana milima. ingawa aina ya vilima hutofautiana kati ya mtu na mtu lakini vyote ni vilima na lazima muhusika apande tena atulize akili apande kwa busara asije akajajuta baadae.

tuje upande wa huu mlima wako, kwanza umenikumbusha mbali sana enzi hizo nikiwa MISRI hapa Kaunga atakumbuka vyema namaanisha nini. wakati huo ANNA alipokuwa ananitesa kwenye ndoa. Lakini namshukuru sana Mungu leo hii niko KANAANI nakula maziwa na asali.

Sasa mwali nikupe ushuhuda wangu kidogo, binafsi niliangalia nahitaji nini katika maisha yangu, je ndoa yangu bado naipenda?? nikapata jibu ndio, je mume wangu bado ni mzuri nikapata jibu ndio nikajiuliza tatizo ni nini?? nikapata jibu ni mwanamke mwenzangu hapa nikasema sitoruhusu mwanamke mwenzangu anitese maishani mwangu. sasa nitafanyeje??

nikasema nitafanya haya yafuatayo nitamwona mume wangu mzuri kuliko kwanza, kisha nitaanza kusali kuombea ndoa yangu. neno la Mungu linasema hivi ndoa na iheshimiwe na watu wote, istoshe Mungu anasema yyte alalaye na mwanamke asiyekuwa mke wake anazini na zinaa huaribu hekalu la Mungu so mume wangu kama kichwa cha familia ni hekalu la Mungu kuliharibu inamaana naharibu kichwa cha nyumba yangu.

nilitubu kwaajili ya Mume wangu, kisha nikamtenga na yule mwnamke kwa maombi ya moto wa RMT na damu ya Yesu. mfunike mumeo kwa damu ya Yesu, mzungushie moto wa roho mtakatifu mwekee utisho wa Mungu uwe ndio utukufu wake.

ukijifunza kusali maomabi haya usiku kabla ya saa 10 usiku basi utaona majibu ya Mungu muda mfupi tu. mwenzio mie hadii nilikua nampiga upofu Anna kwa maombi na ndio maana hata alipotolewa ndani hakuona aibu iliyokuwa mbele yake manake alitoka uchi na kitenge changu.

usilale ukalemaa ukategemea hurum ya mumeo, tegemea maombi ya vita na uwe mshindi kwenye maombi haya tena usiwe mpole sema na Mungu wako unataka nini na mwambie adui yako ambaye ni shetan kwamba hana uwezo wa kulipa kisasi juu yako wala familia yako.

hebu acha kulalamika anza leo tena unapoanza kuomba panda sadaka ya mbegu kwamba unaipanda ili Mungu akufanye uvune ndoa njema, mweleze mungu aikumbuke sadaka yako ya mbegu na weleze kabisa kwamba unataka kumpiga upofu huyo rafiki yenu asiione ndoa yako na wala mwanamke yyte yule kahaba asiione na unataka uavune ndoa yeney amani na furaha.

naamini utakuwa umenielewa vyema mpendwa wangu. nakutakia kwaresma njema na Mungu akutane na haja ya moyo wako.
 
hivi unajua kwanini nakupenda!nafkir sijawahi kukwambia
na hakika nakwambia hapa peupe namna hii!
UNA MOYO WA PEKEE SANA!kimsingi i envy you mi kuna watu wananiona strong lakini walahi sifungui gidamu za viatu vyako!NAKUPENDA SANA mwali!sana!
 
Unajua jamii hasa ya wanawake ndio inayowafanya wanawake wengi wajione wanyonge na ni fault yao kila wanaume wanavyocheat; it is so sad kwa kweli maana kwa mtazamo wangu mtu ana cheat kwakuwa ameamua kwani there is always another way out of any situation or problem.
BTW hata wanaume pia hunyong'onyea pale wake zao wanapowasaliti na kujiona wana mapungufu fulani. Which is wrong, kwa maana kwamba as long as umeamua kuwa na mimi na mapungufu yangu basi unapaswa kuwa na mimi, kama huwezi the door is always open. You cant eat your cake and still have it! If you arent ready for commitment then dont commit yourself; as mapungufu (iwe nguvu za kiume, au mvuto kupungua) are as sure as sunshine!
Nawashukuru wandugu kwa mawazo na michango yenu katika hili naamini in the end kila kitu kitaisha and i will be as much happy as I am
 
Mmeo kaingia na utoto kwenye ndoa usithubutu tena kumruhusu kuwa eti ni just a friend huyo X wake na kosa umechangia kwa kiasi kikubwa kuruhusu huo hayo mawasiliano yao.Wenzio huwa tunaomba kistaarabu mawasiliano yakatishwe tukiona hamna uelekeo kesho yake tunatoa amrri na kitisho juu kwa mume.Shenzy type mawasilano ya nn wakati mmeachana. kwani wamekuwa busness partners hao? Kama unataka upate bp au kisukari siku moja endelea kuruhusu huo ujinga kwenye ndoa yako.
 
hivi unajua kwanini nakupenda!nafkir sijawahi kukwambia
na hakika nakwambia hapa peupe namna hii!
UNA MOYO WA PEKEE SANA!kimsingi i envy you mi kuna watu wananiona strong lakini walahi sifungui gidamu za viatu vyako!NAKUPENDA SANA mwali!sana!
am dearly humbled ma dearest.
i love you snowhite na najua wajua kwann mamii huwa nakupenda.

btw nimejaribu kutuma pm kwako na mwaJ na FP na cacico naona imegoma kudeliver sijui nitafanyeje mamii kuhusu ule mpango wetu.
 
Last edited by a moderator:
Nazidi kumwomba Mungu azidi kunipa ujasiri na nguvu katika hili ili mwisho wa siku nifanye maamuzi ya busara na nisimwonee mtu

Mungu wa siku hizi anataka na nguvu zako angalau zitumike ndo atende kazi.You have to change....
 
am dearly humbled ma dearest.
i love you snowhite na najua wajua kwann mamii huwa nakupenda.

btw nimejaribu kutuma pm kwako na mwaJ na FP na cacico naona imegoma kudeliver sijui nitafanyeje mamii kuhusu ule mpango wetu.
FP will chek with her later najua pa kumpata,cacico nakuachia mwaJ pia naweza kumpata mahali! Kaunga anahusika hapa pia!ntambrief
 
Last edited by a moderator:
nashukuru sana snowhite nafikiri basi tukae nae sote mm na wewe mamii manake tunajijua jinsi tulivyoshibishwa ile roho ya umama.

yup!anytime mwali . true_diva huwa hatushushi mikono kirahisi hivo!
bidae tutafte chemba tufanye mpango! hakuna kulia lia hapa!
funga kanga chini ya tumbo twende kazi!
 
Kama madam gfsonwin umeliingilia hili swala natumaini majibu ya ukweli yenye busara kwa mpendwa wetu juu ya tatizo lake yanaenda kuisha.MUNGU AKUBARIKI DADA UKAENDE KUINUSURU NDOA YA MWENZETU.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni mkristo, kumbuka kiapo "kifo ndo kitawatenganisha"..... Muombe Mungu atafungua njia.
 
FP will chek with her later najua pa kumpata,cacico nakuachia mwaJ pia naweza kumpata mahali! Kaunga anahusika hapa pia!ntambrief

thats why i love you mamii. basi wewe fanya yako na mm nifanye yangu ili mwisho wa siku tuwe kama tulivyotaka kuwa.

unakumbuka ahadi yetu ya kwaresma hii?? napenda sana kuona sasa tumekuwa wamama wenye tija.
 
Ndugu zanguni yamenikuta na naomba ushauri wenu,Mimi ninaishi na mume wangu yapata miaka miwili sasa,nina mpenda sana Mume wangu na ninaamini kuwa naye ananipenda pia.Ila kuna tatizo linanisumbua sana juu yake ambalo linanipa wasiwasi kiasi kwamba nashindwa kuelewa hatma ya mahusiano yetu ya ndoa kwa maana ya kwamba nahofia yasije yakaingia shubiri na ile imani nlionayo juu yake ikateteleka.Ni hivi kabla ya kunioa mimi aliwahi kuwa na mahusiano na wanawake wengine ila mwanamke wa mwisho ambaye aliachana nae amekua akiendelea kuwasiliana na mume wangu na kila ninapohoji juu ya hilo Mume wangu hunijibu kuwa hauna kitu kinachoendelea baina yetu ni rafiki yangu tu wakawaida na hana shida yoyote na sisi kwanza huwa anapiga simu na kutuma meseji za kutujulia hali,anyways nimejitahidi sana kuwa na mtizamo chanya na kuuambia moyo wangu uamini hivyo.Ila siku zinavyokwenda nikaona mazoea yanakua sio mazuri kwa maana wakati mwingine humpigia simu ana hutuma meseji humueleza mume wangu kuwa amemmiss sana na anataka kuonana nae na vitu kama hivyo.Nlimwambia mume wangu mawasiliano na huyo mpenzi wako wa zamani hayanibariki hata kidogo naomba uwe na mipaka na ikibidi uache kwa maana yananiumiza mimi zaidi,aliniahidi kufanya hivyo na kweli kwa kipindi fulani kazi ilipungua ila sasa leo ametuma tweets kuhusu mume wangu kwenye mtandao wa twitter kitu ambacho kimeniuma maana anaeleza jinsi anavyofurahia tendo la ndoa na mume wangu na baada ya kuliona hilo nkampigia mume waqngu kumweleza akaniambia atampigia simu kumsema juu ya hilo na kumuonya.Badala yake kilichotokea yule mwanamke alituma tweets za kunitukana na kunidhalilisha mimi kitu ambacho kinaniuma sana kwa maana mume wangu anasema yule mwanamke ni rafiki mzuri tu na hana shida hata kidogo.Nisaidieni ushauri ndugu zangu je niendelee kuvumilia hayo yote yanayojitokeza na kuamini maneno ya mume wangu kuwa huyo mwanamke hana shida na sisi ama nifanyenye?Naomba ushauri wenu katika hili.....
Kwanza amini wewe ni wa thamani sana mbele ya Mungu na Mumeo.alipokuoa wewe alikuwa Anajua vzr kuwa kuna mwingine kabla yako ila akaona wewe ndo unayefaa kupewa heshima ya mke.huyo anayetukana hajielewi hata yuko wapi!kwanza ame simama jalalani kila mtu anatupa uchafu yeye anaona yuko kwenye bustani Nzuri sana.usijibizane nae hata kidogo kwani atakushusha heshima yako.Mumeo mwambie unashukuru sana kwa namna anavyokudhalilisha then nyama za kimya na usimfuatilie tena mauzauza yake.ila huduma zote umpe Kama vile hakuna kitu kilichotokea.ukigombana nae unamvimbisha kichwa.matokeo ya Haya uyalete tena hapa jamvini utapata ushauri mwingine.
 
yup!anytime mwali . true_diva huwa hatushushi mikono kirahisi hivo!
bidae tutafte chemba tufanye mpango! hakuna kulia lia hapa!
funga kanga chini ya tumbo twende kazi!

imeandikwa nimeweka jambo jipya chini ya mbingu ya kwamba mwanaume atalindwa na mwanamke. sasa hatulindi kwa mapanga na bastola jamani bali kwa maombi na sadaka.

na pia dada true_diva biblia inasema ukizimia siku ya taabu yako nguvu zako ni chache. na mtu akishindana kweye machezo hapewi taji hadi ameshindana kwa halali. na mwisho wa siku vita ikimalizika utavalishwa taji. taji ya nini?? ya furaha, upendo, ndoa njema, watoto wenye siha njema, mume mwenye heshima umeona??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom