Kweli nimeamini shujaa hukunjwa na mkewe

ligera

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
2,646
Reaction score
1,171
kila siku nilikuwa nikisikia watu wakisema kwamba hakuna mwanaume aliyejasiri mbele ya mwanamke ,leo nimejionea mwenyewe kwa macho yangu kamanda mmoja ambaye anasifiwa na kugopwa mno kazini na walio chini yake kutokana na misimamo yake ya kikazi ,lakini leo tulipoenda kumsabahi asubuhi alichimbwa mkwara na mkewe kwamba marafuku kuongea na sisi na aliambiwa aende ndani mara moja na alirudi ndani akatuacha nje tukistaajabu yaliyotokea.mwisho kila mmoja wetu alijikuta akitamka hakuna jasiri mbele ya mwnamke,kwenye mapenzi hata kamanda awe na misimamo vipi inayeyuka tu kama barafu iliyokutana na joto kali .nawauliza wana jf hivi ni kweli shujaa anakunjwa na mkewe au ni msemo tu
 
nyie ndo wagombanishi sasa.....wenyewe wanaongea lugha moja na kuelewena....
Hilo swali pia jirudishie wewe ukiwa pande zako unakuwaje???
 
ninachouliza hivi ni kweli wanaume wote ni dhaifu mbele ya wake zao

Wengi wao mkuu. Labda hata mimi. Si unajua nyani haoni kundule? mpaka mtu aliyepembeni ndo aseme.......LOL
 
samson mbele ya delilah ndo ilikuwa vile,sembuse mjeda....kina delilah wapo wengi sana bado..
 
nyie ndo wagombanishi sasa.....wenyewe wanaongea lugha moja na kuelewena....
Hilo swali pia jirudishie wewe ukiwa pande zako unakuwaje???
Vai mambo... Hivi uliyenaye naye huwa unamshusha ujasiri kama hivyoo..???
 
Umetafsiri visvyo mkuu, hayo ni sehemu ya mahaba yao,wala huyo bwana sio dhaifu!

Rugaijamu, nikwo abashaija bagila kweli! nolwo zilaba zili ngonzi? ( Rugaijamu, wanaume kweli wanakuwaga hivyo hata kama ni mapenzi!)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…