kila siku nilikuwa nikisikia watu wakisema kwamba hakuna mwanaume aliyejasiri mbele ya mwanamke ,leo nimejionea mwenyewe kwa macho yangu kamanda mmoja ambaye anasifiwa na kugopwa mno kazini na walio chini yake kutokana na misimamo yake ya kikazi ,lakini leo tulipoenda kumsabahi asubuhi alichimbwa mkwara na mkewe kwamba marafuku kuongea na sisi na aliambiwa aende ndani mara moja na alirudi ndani akatuacha nje tukistaajabu yaliyotokea.mwisho kila mmoja wetu alijikuta akitamka hakuna jasiri mbele ya mwnamke,kwenye mapenzi hata kamanda awe na misimamo vipi inayeyuka tu kama barafu iliyokutana na joto kali .nawauliza wana jf hivi ni kweli shujaa anakunjwa na mkewe au ni msemo tu