Kwani umemuoa? Mwanamke unaeweza kutembea nae wewe nje ya ndoa anaweza akatembea na mwanamme yoyote yule, huna hati miliki.
Halafu nawapa nasaha vijana, mwanamke wa maana haswa, si yule ambae anahitaji matumizi yake ya kila siku kutoka kwako. Mwanamke anaehitaji kutoka kwako huyo yupo katika biashara na mfanya biashara huwa na wateja wengi na tofauti.
Astahili yenu yawapate na mtaendelea kupatikana hivyo hivyo kwa uzinzi wenu.
Nawashangaa sana kuona kuwa kuwa na mwanamke au mwanamke kuwa na mwanamme (boy friend/girl friend) mnaona kuwa ni sifa au uhodari. Sifa ya mwanamme au mwanamke ni kuwa na mume/mke wa ndoa.
Hivi haya maadili huwa mnafundishwa wapi? Taifa omba omba huanzia kwa hawa wazinzi wa kike na wa kiume. Zinaa huongeza ufukara, si wa mali tu, bali hata wa mawazo. Jiulize, hivi mwanamke anaeweza kukuvulia nguo kabla hujamuoa anaweza kukushauri nini cha maana? Wakati wana falsafa wanasema kuwa "kuna mwanamke mwenye nguvu nyuma ya kila mwanamme mwenye mafanikio". Sasa mwanamke nguvu za nini? Nguvu za mawazo na si misuli. Anaeweza kukuvulia chupi nje ya ndoa hana nguvu za mawazo au ni mfanya biashara ya kuuza mwili wake. Hivi mkivuliwa nguo mnajiona mahodari na mmepata? Mnanchekesha! Wenzenu huwa wanaona "lione jinga hili limepatikana".