Nadhani inafaa tuwe na viongozi wa aina ya Pinda kwa maana ya watu waliokulia maisha ya kawaida (wanaozitambua kwa undani changamoto anazopambana nazo mtanzania wa kawaida) lakini waadilifu wanaotaka kuitoa nchi hii kutoka kwenye umasikini kwa kutumia rasilimali zetu vizuri, siyo kwenda tunajipendekeza na kujidhalilisha kwa wazungu kuomba misaada.
Mpaka pale tutakapoacha kulaumu vita vya ukombozi wa Afrika kwa umasikini wetu, ukosefu wa pesa za kuwasaidia watu wetu, na visingizio vingine tunavyo-manufacture ili mradi ku-justify umasikini wetu ndipo tutaondokana na umasikini.
Binafsi sioni umhimu wa rais wetu kuwa kila sehemu kila siku akihudhulia uzinduzi wa maabara (tuliyojengewa kwa msaada), akipokea zawadi ya kuku (sijui ya kufuga?) akihudhulia matamasha ya mziki na akina Boys II Men, akirandaranda huku na kule kututafutia misaada. Halafu kesho yake anatudanganya kuwa ahadi zote alizotoa wakati akiomba kura 2005 zitatekelezwa na kuwa ndani ya miaka miwili kila mwalimu wa Tanzania atakuwa na laptop, wakati hata mshahara wake tumeshindwa kuuongeza ili awe motivated zaidi.... no priority, no direction, no brains, no nothing, just smiles and empty words. Hatutaki!