kufuga kuku wa kienyeji si kigezo cha Ukulima
wazee wa kuigwa tanzania!
Uko right mkuu I salute you....siku moja tulipita nyumbani kwa wazazi wake kigogo fulani akatuambia 'mnaiona ile nyumba ya udongo pale' tukasema naam. akasema yaani baba yangu amefia katika nyumba ile hata baada ya mimi kumjengea hii mpya ya kisasa aligoma kuhamia.. mmh mmh tukabaki hoi
Kuna wazazi watata sana hapa tz
mix with yours
Nadhani inafaa tuwe na viongozi wa aina ya Pinda kwa maana ya watu waliokulia maisha ya kawaida (wanaozitambua kwa undani changamoto anazopambana nazo mtanzania wa kawaida) lakini waadilifu wanaotaka kuitoa nchi hii kutoka kwenye umasikini kwa kutumia rasilimali zetu vizuri, siyo kwenda tunajipendekeza na kujidhalilisha kwa wazungu kuomba misaada.
Mpaka pale tutakapoacha kulaumu vita vya ukombozi wa Afrika kwa umasikini wetu, ukosefu wa pesa za kuwasaidia watu wetu, na visingizio vingine tunavyo-manufacture ili mradi ku-justify umasikini wetu ndipo tutaondokana na umasikini.
Binafsi sioni umhimu wa rais wetu kuwa kila sehemu kila siku akihudhulia uzinduzi wa maabara (tuliyojengewa kwa msaada), akipokea zawadi ya kuku (sijui ya kufuga?) akihudhulia matamasha ya mziki na akina Boys II Men, akirandaranda huku na kule kututafutia misaada. Halafu kesho yake anatudanganya kuwa ahadi zote alizotoa wakati akiomba kura 2005 zitatekelezwa na kuwa ndani ya miaka miwili kila mwalimu wa Tanzania atakuwa na laptop, wakati hata mshahara wake tumeshindwa kuuongeza ili awe motivated zaidi.... no priority, no direction, no brains, no nothing, just smiles and empty words. Hatutaki!
Yeye ni mtoto wa mkulima, mimi ni mkulima mwenyewe
Hawezi kumla huyo kuku kabla wataalam hawajampigia kisomo !!
Pinda na yeye aache kupindisha mambo. Amekuwa serikalini akilipwa mshahara kwa zaidi ya miaka thelathini.Mshahara wake kwa kujinyima tu anasa angeweza kuwajengea wazazi wake nyumba nzuri tu na ambayo ni sawa na hadhi ya mshahara wake. ...
Sasa kama amefanya kazi muda wote huo, mshahara alikuwa anaupeleka wapi japo ni mdogo. Au kajenga maeneo mengine kwa kuhofia Usumbawanga?
Kwanza, nikichukulia kama picha hiyo ni halisi lazima nikubali kwamba PM huyu ni Mtanzania wa kawaida (anaweza kujiita mtoto wa mkulima). Tunalazimika kuipongeza hali hiyo kwa vile nchi imegeuka sana: wizi wa kutisha na hujuma mbalimbali za kiuchumi vimekuwa vitu vya kawaida kabisa kwa viongozi wetu na tunajua kuwa wapo wenye utajiri usiomithilika kwa viwango vyetu.
Pili, kwa sisi tuliofanya kazi serikalini miaka ya kutosha, ukitegemea kuishi kwa mapato halali ya kazi yako peke yake na usipokuwa na harakati nyingine nje ya kazi (kitu ambacho utalazimika kutokuwa makini au kuiba muda wa kazi) basi hiyo nyumba tunayoiona hapo ni mafanikio ya kutosha. Halafu, hata kwa hao wakubwa kama PM, vipato vyao miaka ya nyuma havikuwa chochote. Ni siku hizi tu vimeinuliwa kiasi cha kufanywa siri.
Tatu, hii sasa ni nje kidogo ya mada, hali hiyo si sifa tosha ya u-PM. Anatakiwa pia awe na sauti ya kukemea na kuchukua hatua za dhati kudhibiti mafisadi na hujuma za kiuchumi serikalini. Pamoja na yote, basi angalau kwanza tukubali kuwa huyu mheshimiwa ni zao tofauti kidogo na walafi wanaotishia hatma ya taifa. (Hata Mrema alitamba kumzidi utajiri!). Anachotakiwa kufanya ni kuchangamka na kuonyesha uongozi thabiti wa kisiasa. Amepoa sana kuweza kuimudu nafasi hiyo.
Tanzania kuna usumbawanga,ukala ,usukuma etc.Mpaka leo watu wengi hawajengi vijijini kwao hasa toka mikoa hiyo kuogopa kulogwa.Hii ni fact!Kuna watu wako mijini ,na pesa kibao ,but never will build a decent house for his parents.
CREDIT kwa wachaga ,pamoja na kuwa na nyumba walipo popote,bado wanajenga migombani.It highly likely kupata nyumba nzuri self contain uchagani vijijini kuliko USUKUMANI,UKALA ,UFIPANI na kadhalika.
Watu wengi wamelowea DAR ,vijijini kwa wazazi wao kunatisha
tunadanganyana tuu hapa kama ufisadi kila mtanzania ni fisadi sema tuu hamjapata nafasi ukweli ni kwamba tofauti na viongozi wengine wengi Pinda ni MKULIMA

Picha nzuri inafurahisha sana.
Nakubaliana nawe moja kwa moja kwa yote uliyosema. Watumishi wa Serikali wa aina ya akina Pinda walikuwa wazalendo waliotumikia nchi yao kwa moyo na si kwa kuiibia.
Mie nadhani kupoa kwa Pinda kuna sababu nyingine zaidi ya yeye kuwa dhaifu. PM makini anatakiwa awe chini ya Rais makini ndipo kwa pamoja wanaweza kuchapa kazi inavyostahili. Mfano mzuri ni ule wa Rais wa awamu ya kwanza na mawaziri wakuu wake. Angalia Sokoine alivyokuwa anafanyakazi usiku na mchana na kuchukua hatua kali na thabiti kwa manufaa ya taifa bila hofu yoyote kwa sababu Mwalimu Nyerere alimpa ruksa ya kufanya yale yote. Vivyo hivyo kwa Salim, Msuya na Kawawa. Wote hao kazi zao za kizalendo ziliweza kuonekana na kuthaminiwa kwa sababu Rais wao alikuwa akishirikiana nao bega kwa bega bila usanii wala unafiki wowote.
kitu ambacho watu hawajaelewa ni kwamba raisi hakwenda huko kupokea huyo kuku. alikuwa na ziara ya kikazi akapitia kusabahi wazee. pia umiliki wa kuku sio kigezo cha ukulima kwani hata aziz anaweza kutoa kutoa kuku kwa raisi.