KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Asalaam alyeikum ndugu wana jamii ya jamiiforum..?
Awali ya yote poleni kwa maswahibu mnayopata sehemu mbalimbali na wale mnaokula raha shikilieni hapohapo.
Mwenzenu juzi kati nimeyakanyaga!,mwisho wa mwaka huu nikaamua niende zangu kijijini kusalimu ndugu na jamaa pamoja na majirani.. siku ya kwanza ikapita salama ya pili nayo haikuwa na zimwi lolote.
Zengwe likaanza siku ya tatu naamka tu kichwani unapiga ule wimbo wa "furaha Kulewa na marafiki" nikawa naupotezea baadae kiu cha malt malt fulani kikawa Kikali sana!,moyo wa kikomamanga ukaniambia "yanini kujinyima..?".
Haikuchukua muda tayari nikawa kwenye grocery moja hivi inayopatikana kijijini.. galagaza sana serengeti lager nikaona haitoshi nikaona local gin yetu itatatua tatizo la kutokulewa!.
Mezani akatua jibapa size ya kati nikachezanae kiperesopereso mpk akakatika! Nikanyanyuka kama naenda uani ili nipime hali nikajiona hali bado ni muhali japo sio sana!.
Ungwe ya pili ikawadia jibapa ndogo ikatua mezani sasa huyu nikaona nisimpige kimperesopereso! Mara hii nilimpiga knock out!.
Nikacheki muda ndo kwanza ilikuwa mida ya saa kumi hapo kijasho fulani hivi cha kidowezi kikawa kinatoka.
Kunyanyuka hatua ya kwanza nikayumba ya pili nikataka kuanguka lkn maulana akasaidia sikuanguka.
Nilipoona hiyo hali nikajua kabisa leo kazi ipo ikabidi nifungulie ufahamu wa pili ili niweke mambo sawa. Kwanza sikutaka kuonekana nimelewa pili nikajiambia lazima nitembee mwendo wa ndoige! Yani hata ikitokea nimeangua basi iwe kama sijaanguka.
Safari ikaanza kuelekea nyumbani jambo lakufurahisha hatua kumi za awali nilipiga fresh hata ungekuja na kipimo cha Ulevi kwa kutumia mwendo ungefeli!. Labda ungenipatia kwenye macho na kuongea.
Mwendo ukakolea mpk nikajiona Niko fit nikaongeza na hatua zikapita dakika kama kumi hivi nikatokeza kwenye kisima cha kijiji sasa hapo ndo nilipoharibu akili yangu iliponiambia hebu nenda kachungulie uone maji yapo kina gani.
Mbovu mbaya hakukuwa na mtu karibu na kile kisima kimejengewa kina ngazi mbili ile nakaribia ngazi ya kwanza tu mlevi nikajikwaa.
Mzimamzima kama gunia la mihogo nikashangaa naenda kulilaki tundu la kisima na kibovu zaidi kichwa ndio kikawa kimetangulia. Niliingia kama mshale ambao ulipatia target mpk mlengaji akasema kazi nzuri.
Bahati nzuri nilikwamia njiani yani almanusra nifikie maji hapo huku juu miguu ipo juujuu na kichwa kipo ndani ya kisima natizamana na maji. Tena maji yale yalivyomakatili yakawa yananionyesha taswira yangu nilivyomlevi kupindukia.
Nilipotaka kujiinua nirudi juu ndo nikagundua sina pa kushika na nikileta vurugu zaidi basi natumbukia kisimani! Nikaanza kutukana matusi hovyo tena mazito mazito,nikaukumbuka na ule usemi wa "sungura mjanja hunasa kwenye tundu bovu. "Nikajiona huyo sungura ndio mimi kiberenge.
Zikapita dakika kama tatu hivi bila masada wowote hakuna mtu aliepita wala mwenye shida na maji. Nikajiona taabani nitakufa kijinga nikaanza kupiga kelele za kuomba msaada. Hapo nimebakiza kama dakika mbili tu za kuamua liwalo na liwe nitopee kwenye kisima cha nzengo au niokolewe!
Nilipiga kelele mpk tumachozi fulani hivi twa majuto tukawa tunarengarenga! Ule wimbo wa furaha kulewa na marafiki ukageuka kuwa wimbo wa kamanda.
Nikaona haitoshi nilipiga kelele tena mpk kwenye taswira ya maji niliona Kidaka tonge changu kilivyosimama nacho kikiomba msaada maana kiliona kabisa huyu kenge anatuua sasa hivi.
Lile jasho ushenzi likakosa pa kujificha isitoshe nikikumbuka ninahistoria mbaya na maji ndo nikajiona kabisa zimefika kama sio kuwadia.
Kelele nyengine kali na ya kilevi ikanitoka nafikiri hiyo ndio ilikuwa kelele kali niliyowahi kupiga toka kuzaliwa wala haikuchukua muda nikasikia vishindo vikikaribia kisimani! Punde nikavutwa na njemba mbili hivi za pale kijijini.
Hapo nipo chakali hoi bin hoi na pombe ikawa imenikolea kushinda hata ile awali. Nafikiri ile kelele ya mwisho niliyopiga haikuwa kelele ilikuwa ni mbiu! Maana takribani nusu kijiji ilikuwa imeshafika.
Hapo nipo chini mwanaume tisheti wamenivua sendoz moja ipo nyengine sijui iko wapi! Nahema kama Kambale nje ya tope.
Sasa hapo ndo ukaanza utambuzi mara mwanakijiji mmoja akasema huyu si mjukuu wa fulani huyu. Picha likaanza kuungua hapo na mbaya zaidi wale walioniokoa nao wakatoa ushuhuda wa namna walivyonikuta nikikinajisi kisima cha kijiji. Haikutosha wakakandia na hapa mnapomuona kalewa nzwiiiiii.
Wakuu hiyo nzwiiii ioneni hivyohivyo heri mtu aseme mtu kalewa tu kuliko kuweka na hiyo Nzwii, hata ambao hawajawahi kulewa hapo wanajua huyu mlevi sio kwamba tu kalewa bali hapo alipo anaona nyotanyota.
Sasa waliponichosha zaidi si wakaanza kunisema pale kwamba watu wa mjini sijui tuna tabia mbovu ndo tunakuja kuharibu na watoto wao kijijini! (Kumbukeni nikiwa kijijini kwetu mimi ndio asali ya warembo).
Walinisema sana mpaka kwa kiruga ulifika hatua hasira zikanikamata nikaona niwatolee uvivu hawa wataniona mi boya especially wananisema mbele ya totoz za kijijini kweli.
Sasa akili ya pombe ikaanza kujibu mara nijitape mi sterling kwanza wangeniacha ningetoka mwenyewe! Matusi yakaanza kunitoka. Halooo wanakijiji wenye hasira kali wakataka kunichakaza pale wengine wakawa wanazuia nisipigwe wengine wamecharuka wanasema kijana lazima nifunzwe adabu.
Nilipoona upande wa watetezi wangu unakaribia kushindwa nikaona nitumie mbinu yangu ya kiinteljensia. Nikavunga kuzimia. Purukushani la wao kutaka kunidunda ikabidi life wa focus kumtibia mzimiaji! Sio kwa ndoo zile za maji nilizomwagiwa.
Nilipozinduka nikapelekwa nyumbani kesho yake mjadala kumbe ulifika kwa mwenyekiti wakaafikiana na sungusungu wake kuwa nishikwe nikapigwe mboko! Baada ya kupata hiyo taarifa tu sikusubiri haraka sana nikarudi town wabaki na mboko zao.
Ujumbe pombe sio chai wakuu, lingekufa jitu walai kumbukeni kijijini nina deni.