Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Status
Not open for further replies.

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Miezi michache iliyopita vyombo vya habari vilisheheni taarifa ya magaidi waliokuwa katika vijiji vya Handeni.

Taarifa zilifika Tanga kuwa kulikuwa na magaidi wanaishi katika mahandaki na operesheni maalum ilikuwa ikifanyika kuwateketeza.

Propaganda ikaenezwa kuwa walikuwa hawaitambui serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Habari zilivuja Tanga mjini na vitongiji vyake kuwa kuna vijiji vimeteketezwa.

Kwa hakika kuna watu waliletwa Hospitali ya Bombo wakiwa na majeraha ya risasi.

Kwa watu waliofika Hospitali ya Bombo kwa kweli waliwaona vijana waliokuwa wamefungwa pingu wakiwa katika vitanda vyao huku wakilindwa na askari.

Taarifa zikafika vilevile kuwa kuna watoto wadogo wamefikishwa Tanga baada ya kukutwa porini.

Watoto hawa walikuwa wamehifadhiwa katika moja ya shule za hapo mjini.

Katika hali kama hiyo vilevile zikafika taarifa tofauti kwa Waislam wa Tanga kuwa hao walioletwa Hosptali ya Bombo na watoto waliookotwa porini ni Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande walioshambuliwa na askari pasi na sababu.

Juhudi za Umoja wa Taasisi za Kiislam Tanga (SHITA) chini ya Mayor Omari Guledi na Katibu wake Ahmed Mustafa kukutana na Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa kupata ukweli zikagonga mwamba.

Hali ikawa tete baada ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso mmoja katika masheikh vijana mjini Tanga kukamatwa na kuwekwa rumande kisha kuhamishwa Handeni ambako alifunguliwa kesi ya ''kushawishi mauaji.''

Ikavuma kuwa patakuwa na maandamano kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Chanmbuso.

Askari wa FFU walizingira misikiti kadhaa Ijumaa hiyo lakini hapakuwa na maadamano yoyote.

Alipopata dhamana na kuachiwa Sheikh Chambuso alikuja Tanga na habari za kutisha kuhusu dhulma iliyopita katika vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande.

Habari hizi alielezwa na mahabusi wendake katika hivyo vijiji vilivyoshambuliwa.

Sheikh Chambuso katika hotba aliyotoa katika moja ya misikiti maarufu Tanga aliwafahamisha Waislam kuhusu misikiti iliyovujwa na kuchomwa moto, Qur'an zillizochoiwa moto na nyumba za Waislam zilizoteketezwa kwa kisingizo cha ugaidi.

Wananchi jioneeni wenyewe yote hayo katika hizi picha.

PS: Weka cursor kwenye picha click utapata na maelezo ya picha.
 

Attachments

  • Angalia mandhari zuri ya kijiji na nyumba.png
    Angalia mandhari zuri ya kijiji na nyumba.png
    183.2 KB · Views: 1,494
  • Msingi wa msikiti ulivyovunjwa na matofali kuondolewa kabisa.png
    Msingi wa msikiti ulivyovunjwa na matofali kuondolewa kabisa.png
    23 KB · Views: 3,465
  • haya ni baadhi ya matofali yaliyokuwa kwenye jengo la msikiti yakiwa tayari kupelekwa kwenye jen.png
    haya ni baadhi ya matofali yaliyokuwa kwenye jengo la msikiti yakiwa tayari kupelekwa kwenye jen.png
    217 KB · Views: 1,373
  • Nyumba iliyoezuliwa paa.png
    Nyumba iliyoezuliwa paa.png
    242.5 KB · Views: 1,302
  • Nyumba ya Imam.png
    Nyumba ya Imam.png
    22.6 KB · Views: 3,361
Kwa definition ya ugaid ilishindikana kupatikana labda dictionary mpya,

Kwa mantiki hiyo basi, hiyo ni vita dhidi ya Uislaam kwa kutumia jina hilo pahala popote pale Dunia kwa nembo ya eti UGAIDI.
 
Mnatuletea mambo yenu ya kujilipua hapa...dini zingine zinahubiri ushetani na mauaji..
 
kwa kweli nazichukia kupita maelezo hizi dini,hasa hizi dini za zilizoletwa na watu weupe na miafrika ilivyo mijinga ikaingia kichwa kichwa matokeo yake leo hii imekuwa kama mi-zombie vile..!!
 
Ni vigumu kutofautisha kati ya muislam na gaidi,maana ugaidi na uislam ni pande mbili za shiling moja,kwa hyo kupambana na ugaidi ni lazma kupambana na uislam.
 
Ipo siku yatawarudi wanaofanya uovu huu. Na ipo siku waislam wataishiwa na uvumilivu ndio itakuwa mwisho wa uonevu

Hii ni Vita Dhidi ya UGAIDI na MAGAIDI.Kama unaona ni Vita dhidi ya Uislamu Jaribu kulianzisha uone Moto wake.Mwenzio Shekh Ossama alitamani ardhi ipasuke.
 
Mataifa ya kikafiri yamejaribu kutafuta sababu za kuwashambulia waislamu kwa miaka mingi sana.
Na hii sababu hii inayoitwa ugaidi imekuwa inatumiwa kuua na kuingilia ardhi za watu kwa sababu za kuiba mali zao!

Ukiangalia ktk english dictionary maana halisi ya ugaidi utakuta hizo nchi wavamizi na hizo serikali zinazo wanyanyasa waislamu ZINA SIFA ZOTE ZA KIGAIDI!

sasa sijui toka lini GAIDI AKAPIGA VITA UGAIDI!!

Ukirudi hapa kwetu hali ndio mbaya zaidi.
Nadiriki kusema wale waanzilishi wa kuwavamia waislamu ktk nchi zao na miji yao HUJITAHIDI KUTAFUTA JAPO KI USHAHIDI CHA UONGO ILI WAFANIKISHE YAO!
Hizi serikali km ya kwetu dhulma yao iko WAAZI KABISA.
Na wasipojiregebisha nchi hii itakuja kumbwa na balaa kuliko yaliotokea rwanda na burundi.
Mungu isaidie nchi yangu TZ.
 
Hii ni Vita Dhidi ya UGAIDI na MAGAIDI.Kama unaona ni Vita dhidi ya Uislamu Jaribu kulianzisha uone Moto wake.Mwenzio Shekh Ossama alitamani ardhi ipasuke.

Haitwi ossama. Bali ni SHEIKH OSAMA MWANA WA LADEN!
Ametingisha mataifa zaidi ya 50 ya makafiri!
Kawarudisha makafiri kwenye body bags kwa maalfu!
Ni one man army! Wamepiga kila kona ya afghanistan na Pakistan kwa zaidi ya miaka zaidi ya 10 na ziada lkn wapi!
Kwa hio unapotaka jina lake MPE HESHIMA yake!
 
Ushenzi kama huu wakifanyiwa Waislam huwa hakuna tatizo, sasa hivi ukitaka kuwapiga Waislam wewe weka tag ya ugaidi unaruhusiwa hata kuwaua.

Waislamu wa wapi wanafanyiwa Ushenzi?.Kama ni Tanzania siamini kama Serikali ya CCM inaweza kuyafanya haya.Jengeni vyuo watu waelimike.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom