Nimekuwa nikijiuliza kwanini watanzania wengi wanapenda kushabikia na kushangilia timu za ulaya..utakuta mtu mweusi kutoka kule Musoma amevaa jezi imeandikwa Chacharito,Rooney nk...katika moja ya policy ya kuingiza ukoloni mamboleo ni kuwafanya watu weusi wadharau mambo yao..ni watu wachache sana wanaovaa jezi za timu kama Simba,Yanga,Azam FC,Mtibwa nk.....Tuacheni utumwa huo jamani turudini nyumbani tuone namna ya kukuza soka letu.....

sidhani kama ni vibaya kuvaa jezi hizo za timu ya kizungu. Sio kuwa hatutaki kuzipenda timu zetu za nyumbani, lakini kuna raha gani kuitukuza timu ambayo kila siku inakupa homa kwa migogoro isiyoisha? Ndani ya mwaka mmoja timu inakuwa haijafanya chochote cha maana, zaidi ya uongozi kuvurugana na kutuhumiana mambo mbalimbali. hata hizo jezi za wachezaji wa kibongo zipo kwani? maana wenzetu kila mchezaji ana namba yake, hata timu ikiwa na wachezaji 40, huku timu ina wachezaji 30, jezi 18, jezi za kubadilishana.
tunachohitaji ni kujitambua kuwa sisi watanzania na nchi nyingine za kiafrika hatuitendei haki sekta ya michezo. hatuna mipango madhubuti ya kuiimarisha, ambapo ingekuwa ni moja ya sehemu ya kutengenezea ajira kwa vijana mbalimbali