Kweli wakati umefika kubadiri jina la timu ya soka ya nchi yetu

Kweli wakati umefika kubadiri jina la timu ya soka ya nchi yetu

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Kwa kuzingatia matokeo mabovu ya timu yetu ya soka ya taifa ni aibu sasa kuendelea kuiita "TAIFA STARS". Nashauri kabla ya kuanza kubadiri benchi la ufundi la timu hiyo ni bora kulibadiri jina na kutafuta jina la kutangaza utalii wetu tuliobarikiwa na Mwenyezi Mungu. Narejea tena ni AIBU kuendelea kutumia jina la "Taifa Stars" kwa muendelezo huu wa kudidimia kwa soka letu.
NB:- Timu ikiwa na kocha wa kigeni ikifanya vizuri (Maximo) kelele na ikifanya vibaya (Martinooj) kelele. Sasa ina kocha (benchi la ufundi) mzawa na haijafanya vizuri si katika michezo ya kirafiki lakini wapiga kelele wamekaa kimya kabisaaaa. Unafiki huu.
 
Kwa kuzingatia matokeo mabovu ya timu yetu ya soka ya taifa ni aibu sasa kuendelea kuiita "TAIFA STARS". Nashauri kabla ya kuanza kubadiri benchi la ufundi la timu hiyo ni bora kulibadiri jina na kutafuta jina la kutangaza utalii wetu tuliobarikiwa na Mwenyezi Mungu. Narejea tena ni AIBU kuendelea kutumia jina la "Taifa Stars" kwa muendelezo huu wa kudidimia kwa soka letu.

= kubadili
= kulibadili
 
Mbona lishabadilishwa muda tu sahivi inaitwa "stars rojorojo"
 
Ajabu hujatoa pendekezo la jina unalotaka. Jezi zirudi kama zamani au zitokane na bendera ya taifa letu. Hii rangi ya sasa sio rangi iliyopo kwenye bendera. Kama rangi za bendera hazitakuwa ndiyo msingi wa kuchagua jezi, basi upatikane msingi mwingine muafaka.
 
Mkuu nimependekeza jina la mbadala liwe la KITALII zaidi ili kuitangaza nchi yetu kiutalii na si soka. Kuhusu rangi ni vema na ni kawaida timu ya soka ya nchi huvaa jezi zinazoakisi rangi za bendera za nchi husika lakini hapa kwetu yaonekana rangi NYEUSI haitakiwi na baadhi ya waliozowea aina fulani ya rangi hasa za timu za Yanga na Simba.
 
Mbona lishabadilishwa muda tu sahivi inaitwa "stars rojorojo"
Mkuu hilo neno STARS lisiwepo asilan kwani linatufanya tuwe mastar wa kufungwa fungwa hovyo hovyo.
 
Jina halisaidii kitu.

Malinzi alikuja na idea ya kubadili jezi lakini ni shida
Mkuu, jina lina mchango wake kwa kila kitu. Hii mialiko tunayoipata ni kutokana na jina hilo sasa tunapofungwa hubadilika na kuwa Stars wa kufungwa wakati nchi hii pana watu wanaoweza kubadilisha soka na kuwa la mafanikio zaidi.
 
Sio wachezaji wale wanaocheza, ni majini yale. Kila mchezaji ana mganga wake, anaenda kuloga ili acheze mpira vizuri baada ya juhudi zake binafsi, sasa apo akishapandikizwa majini lazima acheze fyongo.
 
Mkuu nimependekeza jina la mbadala liwe la KITALII zaidi ili kuitangaza nchi yetu kiutalii na si soka. Kuhusu rangi ni vema na ni kawaida timu ya soka ya nchi huvaa jezi zinazoakisi rangi za bendera za nchi husika lakini hapa kwetu yaonekana rangi NYEUSI haitakiwi na baadhi ya waliozowea aina fulani ya rangi hasa za timu za Yanga na Simba.

Hilo la kitalii lipi mkuu?

Suala la jezi limeingiliwa na unazi wa timu. Bendera ya Taifa haina timu.
Brazil kuna timu zina jezi zenye rangi ya timu yao ya Taifa lkn haijazuia kuakisi bendera yao.
 
Duh, dada mkubwa usiingie kwenye siasa tufanye yetu humu jf tu. Sasa una shule hazina madawati, hazina maabara, hazina hata umeme na vyoo na maji. Waalimu hawana nyumba. Mahospitali hayana dawa wala vitanda. Halafu utawekeza kwenye viwanja vya kisasa? Kama tumeshindwa the basics, when you are poor sports is a luxury.

TFF wanafanya nini? si kazi yao madawati wala maabara za mashuleni, tusiende huko: wawe na maabara za mpira.

Tazama Somalia ambapo nchi ipo kwenye matatizo miaka na miaka sasa, lakini:

Ni upunguani tu Tanzania kuanza kufikiria Taifa Stras itafanya maajabu bila ya kuanza kuwatayarisha kwenye roots.

Tusidhangae miaka michache kuanzia sasa hata Somalia wakitulamba magoli.
 
Wangeanza kubadili viwanja vya mazoezi ili viwe na mvuto kwa watoto na vijana kwenda kufanya mazoezi.

Inatakiwa kila Kata kuwe na kiwanja cha mpira kwa ajili ya watoto, chenye hadhi na vifaa na kocha na walezi wa soka.

Unaanza kubadili juu? Waswahili tunasema samaki mkunje angali mbichi. Bila kuanzia kubadilika ngazi ya chini, tusahau kubadili soka la Tanzania.

Ni nani anataka mtoto wake akajichubuwe?:

Umenena, lakini tutaweza kweli hivyo viwanja??? maana hata madawati huko mashuleni ni shidaaaaaaa. Tuangalie wapi mzizi wa hili tatizo. Hii Taifa Stars inajaribu tu kutuonyesha jinsi tulivyo wabovu Taifa kwa ujumla. Lesoto, Swaziland, Madagascar!!! hii sasa imezidi hata mwendawazimu hawezi kukubali kujifunzia kunyoa, hiki kichwa hakifai.
 
Suluhisho la muda mfupi ni TFF kuwekeza kupitia umitashumta na umiseta, ikiwa ni pamoja kuwapatia. Walimu wa michezo mafunzo Ya ukocha...
Mbali na Hilo Huyu kocha atufai apewe kocha mzawa na wachezaji achague kocha mwenyewe. Eti anaitwa Bocco anaachwa kina Rashid Mandawa,
 
Hilo la kitalii lipi mkuu?

Suala la jezi limeingiliwa na unazi wa timu. Bendera ya Taifa haina timu.
Brazil kuna timu zina jezi zenye rangi ya timu yao ya Taifa lkn haijazuia kuakisi bendera yao.
Ngome Kongwe, Katavi, Manyara, Selous, Ruaha, Mikumi n.k. Mbona vivutio nchi hii ni vingi tuuuuuu. Wenzetu wana The Cranes (Uganda), Indomitable Lions (Cameroon) n.k.
 
Back
Top Bottom