Kweli wanaume wa Dar mnatia aibu

ndugaseli

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Posts
869
Reaction score
2,405
Habari zenu wakuu? Mi sitaki kusema mengi naandka uzi huu nikiwa nimejaa na huzuni kutokana na kitendo kilichotokea.

Ilikuwa majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi nilikuwa nasafiri naelekea Congo na rafiki yangu na gari za IT nikiwa kama dereva pamoja na rafiki yangu tuliamua kuchagua sehemu ya kuweka mafuta tukitoka bandarini itakuwa tabata sheli ya puma wengine wanapaita Alhamza.

Baada ya kufika pale tukapata huduma nzuri tu ya mafuta mimi pamoja na rafiki yangu tukasema usiku huu ngoja tukacheki chochote ili kuweka tumbo sawa tukavuka barabara upande wa pili kama unarudi G/mboto kuna kituo cha daladala pembeni yake wanauza chipsi tkaketi pale tukaanza kula chips.

Akata zoezi la kula chips linaendelea akaj kijana mmoja mvuta bangi akiwa kalegea legea kavaa na hereni sikio la kushoto alivyokuja alikuja kwa heshima na kusema bro mi sijala toka jana tafadhali nisaidien ata buku ili nile yule mwenzangu akamwambia yule dogo kwa ukali bhana sisi hatuna pesa siku nyingne Mungu akipenda tutacheki tu.

Dogo akaondoka akaenda kwa washikaji zake mara wakaja watu kama watatu hivi nao walikuwa wakidai kua hawajala yule rafiki yangu niliyekua naye akasema mkuu twende fasta linaweza tokea lolote akati tunavuka barabara kikaja kile kidogo cha mara ya kwanza kikasema bro haiwezekeni nipeni hata buku yule rafikii yangu akatoa buku akampa kosa likaanzia hapo dogo akataka pesa zote alizorudishiwa chenchi jamaa wakati ananua chips apewe yeye tena akisema maneno ya ukali acheni usenge toeni hiyo pesa fasta.


Yule rafiki akakabwa na yule dogo ndipo asira ziliponishika na kupiga ngumi moja hadi yule dogo akanguka chini baada ya kuanguka chini wenzake wakaja kwahiyo tukawa tunapambana na watu kama wanne kwa mtu mbili huku tukisema wezi, wezi, cha ajabu nilichokiona mpaka naandka uzi huu ni kwamba wakaja wanaume kama kumi nikajua yes nimepata kampani ila walipofika wakaanza kushangaa tunavyopigana na wezi kwa kweli nilihuzunika sana na ni tukio ambalo sitakuja kulisahau katika maisha yangu lakini mpaka sahivi najiuliza wanaume wa Dar wanamatatzo gani jamani hata kutoa msaada wa kumkamata mwizi inakua shida.

Nikarudisha akili nyuma juu ya tukio la Panya road lilivyoshndwa kudhibitiwa tamko kali lilitoka dhidi ya wanaume wa mikoan tena wale wa mara.

Namalizia kwa kutoa wito kwenu wadau mtoe maoni yenu nini kifanyike kuhusu wenzetu wa Dar.
 
1) Dawa yao kageuza wake na mabeki 3 mikoani, hakuna namna Mkuu

Halafu nirudi kwako

Mjini shule mkuu, Wanaume wa mjini watasaidia vipi matumbo matupu? Wakikusaidia unawaongezea njaa tu, sio sawa na mikoani chakula bure tu unavamia hata shamba la mihogo unaji sevia
 
wengi wao wamewahi kukabwa na hao vibaka, so wanajua mziki wake sometimes hao hao vibaka huwa wanatembea na visu, nyembe, mapanga n.k
 
wengi wao wamewahi kukabwa na hao vibaka, so wanajua mziki wake sometimes hao hao vibaka huwa wanatembea na visu, nyembe, mapanga n.k
ni kweli mkuu lakn kwa sisi wanaume wa mikoani hatutembei na matakataka hayo tunajihamin na nguvu zetu we fikiria pamoja sisi na kuwa tulikua hatuna ki2 ila tuliwazid nguvu wale vibaka uchwara
 
Mimi kama mwanaume wa Dar.

Hao jamaa kama kumi waliokuja hawakuingilia kwa sababu hao waliokua wanawakaba ni watoto wa nyumbani hivyo kuwazuia inakua tabu.
Wangekua hawajulikani mngepata ushirikiano wa kutosha.

Dar kuna kuoneana aibu ya macho kwingi mno.
 
Wala

Hao wanawajua wa hapohapo ila wangekuwa wageni wangechomwa moto

Hao ni wa kitaa hapohapo hivyo vigumu kuwazuia
ni kweli mkuu mana mlinz wa sheli alitoka na gobore akati tunapgana na wafanyakaz wengne wa sheli wakasema wale sio wezi wanawajua vzuri
 
apo nimekuelewa mkuu ni kweli kabisa
 
Mkuu wameanza kukulisha Chips aisee... Wanaume wa Dar hatari, mkuu nikushauri, rudi tu kijiji, ukikaa mwezi huko, hilo jina halitokuacha salama
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Eti ninakula chips

Bila hata aibu

We wa mikoani siku nyingine utatafunwa siyo siri, chips waachie wenyewe na mamiregezo yao

Sasa ukianza na kupaka poda si ndo umekwisha tena, utaanzaje kurudi tarime
 
Stor Ni Yakutunga Hii, Labda Kwakua Unawacmulia Wanakjj Wenzio Lkn Saa 5 Usiku Ni Mapema Sana Kwa Dar Hasa Tabata. Watu Wanatoka Harucn Na Sendoff Saa 6 Had 7 Ucku Hiyo Ndo Junction Kipenz Ya Watu Wa Ubungo, Tabata Na Wanaoenda Buguruni. Af Unasema Kaja Kjana Mvuta Bangi Kalegea, Wavuta Bangi Wanalegeaga? Ww Wa Kjj Gan? Wala Ucje Ukasema Mateja, Pale Hapana Kambi Ya Mateja. Km Alivaa Hereni Moja Ckio La Kushoto Huyo Kwa Town Ni Punga Au Choko. Ss Mtapgana Na machoko Watu C Watadhan Mmewala Viboga Af Mmekataa Kuwalipa! Maranyingi Waharifu Wa Maeneo Flan Hawatokag Mbali Na Ukute Wazaz Wao Ndo Viongoz Wa Mitaa, Mf.Magomen, Manzese, Tandika Likikukuta Hlo Lako. Madanguro Ya Mwananyamara Yapo Karibu Na Ofc Za Serikali Za Mtaa Na Hosptal Ya Mwananyamala, Na Kwingine Vibanda Vya Gongo Vpo Karibu Na Vituo Vya Police Na Maisha Yanaenda. Ndo Maana Ya Mjini Kila Mtu Anakufa Kvyake Hakuna Kuzoeana, Ujamaa Wa Nyerere Umebaki Mikoani. Mngetangaza Dau Watu Wangekuja Kuwasaidia.
 
sasa wewe
mporipori unashindwaje kuwapiga watu waliolegea
mtu kutembea hawezi unampiga vipi ??
kwanza hawasikii maumivu utawau upate kesi
 
Muulize JWTZ wa Matejoo Arusha kilichompata akisaidia jamaa asibiwe simu yake toka kwa mateja!!

R.I.P Afande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…