Kweli wanaume wengine kazi ipo ......


Daaaaaaah maisha yanamajaribu kweli mungu amsimaie huyo mama wa watu juu ya uwamuzi wowote alio uchukua, hope watoto wake hawatokuwa majambazi kama baba yao ili atleast wata mfuta mama yao machozi
 

Honestly, ana thamani gani kwangu mtu kama huyo? Hata kama ingekuwa aliniacha na pesa kipindi anaondoka, nakuapia ningemfukuzilia mbali arudi alikotoka or ende kokote anakokujua yeye!!! Unaweza dhani labda angerudi ana pesa ningempokea, Never........haijalishi nina shida kiasi gani baby gal!!!
 

vipi kama bado ungekuwa na hisia za kumpenda? Ungepingana na hisia zako?
 
Kama shetani alimdanganya the first time, what makes him think hatadanganyika tena? Shetani si bado yuko kwenye ajira,ama?
 
Ktk maandiko ya dini tunafundishwa kusamehe, basi na huyo mama amsamehe mumewe kwani ni binadamu, na kama ameona alimkosea mkewe kaamua kurudi basi ni jambo la kumshukuru Mungu. IMPORTANT:Mama ahakikishe usalama wake kiafya kabla hajarudiana nae mana inawezekna mzee keshalivaa gonjwa letu lile, so awe makini kama mzee keshaumia basi amlee tu na atapata thawabu kwa Mungu wake
 
vipi kama bado ungekuwa na hisia za kumpenda? Ungepingana na hisia zako?

Haiwezekani niendelee kuwa na hisia za kumpenda kama mume/mpenzi labda itokee miujiza dunia ianze upya!! Ila kwakuwa umeuliza ngoja tuassume iko hivyo, pamoja na kuwa na hisia nae, nina uhakika akili itakuwa imeshatia adabu kwa adhabu alonipa so ningekubali kufa na tai shingoni my dear!! Sitaweza kurudiana nae aisee....
 
mi ningemvuta chumbani ningempa ilekitu kaimiss for 7 years afu ndo maongezi yaanze baadaye
 
mi ningemvuta chumbani ningempa ilekitu kaimiss for 7 years afu ndo maongezi yaanze baadaye

my friend... usidanganyike na kelele za chumbani, kucha na maneno yote matamu ya kitandani (yanakuja standard pre-packaged na kila mwanamke). Wanawake hawakumbuki namna hiyo hasa kama katikati hapo wamekuja watu wengine. Halafu kama ndio waliumizwa hisia namna hiyo basi hata ila hisia ya ukaribu wa mapenzi haipo wanakuwa kama wanamsaidia mgeni aliyeumba mahali pa kupumzikia. Mwanamme basi anakuwa na jukumu kubwa sana la kuuvuta upendo ule wa awali. Kumvutia chumbani na kumpa unachofikiria alikuwa anakimiss kuna jina jingine kinaitwa kitendo hicho.....

Na ukimpata mwanamke kichaa kweli unaweza kujikuta unaamkia lupango kesho yake.
 
Mie ningemwambia mlango alioingilia ndo huo huo autumie kutoka..samehe ,samehe maradhi..No thank you:embarassed2:
 
Huyo mwanamke amsamehe lakini Angaza au marie stopes kwanza ndo mpango mzima! Lakini zaidi mwanaume kurejea anakuwa amejifunza jambo sio rahisi kurejea hivi hivi ujue alikwama akaona mama yoyoo ndo mwenzi wake wa ukweli..wanaume ndo tulivyo na mnaosema asisamehewe nadhani HAMJAINGIA ndoani mkajionee benyewe... Sema mwanamke anatakiwa aishi kwa tahadhari sana maana wanaume wengine hawatabiriki...
 
vipi kama bado ungekuwa na hisia za kumpenda? Ungepingana na hisia zako?

Husninyo miaka saba hisia gani hizo,
Yaani mie hiyo miaka ilikuwa tosha kabisa kuhamishia mapenzi yangu yote kwa katoto alikoniachia tumboni..
Big NO!
 
FL1
Inaumiza sana, lakini Mwisho wa Siku tunabaki kuwa Binadamu tu, kusamehe ni muhimu sana katika maisha na ni AFYA pia, Lakini lazima mama ajue kwanini mume aliondoka?, Na kilichomfanya arudi tena ni kitu gani?Halafu mengine yaanzie hapo, isije kuwa amerudi baada ya kushindwa na kuona kuwa hana mahali pengine pa kwenda!! Na isije kuwa mambo yakimnyookea anarudi kule kule, manake kuna sehemu nyingine unakaa kwa sababu ya Pesa zako, Hakuna Upendo, zikiisha Huna chako, Ukizipata Mapenzi motomoto.
 
Ha ha ha yaani hata nafasi ya kumuona nisingekuwa nayo

kumsamehe utamsamehe tu nakwambia labda hamkuoana lakini kuishi nae hilo uamuzi inategemea na mtu....upande mwingine wa shillingi hivi mwanamke katoka mbio miezi hata mitatu hujui yuko wapi akirudi anasamehewa na mumewe? Wapi? Tena utamkuta mwingne kashaolewa fasta! Hapo ndo huwa sielewi double standard imekaaje!
 
Nyie,jifunzeni kusamehe,mwee!!....
 
Hakuna cha msamaha hapo, huyoshetani anasingiziwa sana tatizo hajitetei... Hakuna cha msamaha akampige maweshetani aliye mpitia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…