Mkuu
Ulimakafu unamkumbuka Said Swed Scud wewe?Scud yule wa enzi za Abas Gulamali?unakumbuka alivyokua anaifunga Simba anavyotaka?unakumbuka ndio mchezaji wa kwanza wa ligi ya ndani kumiliki gari dogo la kuendea mazoezini?unakumbuka Gulamal aliwahi kutoa chozi kutokana na burudani ya mshikaji uwanjani?lakini kilichofatia ni kuiringia Yanga?akisema mazoezi hayana hadhi na sasa yeye na mazoezi sasa basi isipokua atakua anacheza mechi tuu?unakumbuka nini kilifuatia baada ya hapo?alifukuzwa jangwani zikiwa zimebaki dk chache kuumana na Simba na Yanga akaua mtu,baada ya kutimliwa akarudi zake Mirambo FC na mpira ukafa.
Kiiza anajiona star na hadhi yake sii ya $35,000 ambazo Yanga walikua tayari kumpa na ambazo wachezaji karibu wote wa Yanga wamepewa.Lakini pia kwa ushauri wa coach kasema kwamba kama hataki kusaini kwa pesa hiyo wamwache maana kuna Ngasa,Nizar,Kabange na Msuva wanaoweza kucheza vizuri zaidi.
Hapa Yanga wanabaki kwenye falsafa yao kwamba hawana desturi ya kumbembeleza mchezaji!!