Kwenda kwa mumeo na vitu vyote au kwenda na begi?

@King'asti hujanielewa ..ngoja nikuulize binti yako akiwa anaolewa utamnunulia kila kitu ?

Whatever i can afford, inshaallah! Isipokuwa sitowapa nyumba, labda kiwanja tena siku ya harusi manake nawapa wote wawili. Na hata kama nna nyumba mia mjini, hawatakaa kwenye nyumba yangu na wala sitawapangisha! Lakini zawadi nitawaambia wajadili na mwenzie nijue what they want. Actually sikawii kuwapa chance ya kuchagua their style and taste.

Kwangu mie mama mkwe is my mother, na mume wa mwanangu is my son na nitam-treat like one of my own! Manake hata mwanangu hatokaa nyumba yangu, i hate mamaz boys.
 
so upo tayari kukaa kwenye nyumba ambayo kila kitu ni cha mke ..?

Mi nipo tayari kuhamia kwa wife na kukaa kwenye nyumba yake tukizinguana na beba malboro yangu begani huyoo uswazi
 
Mi nipo tayari kuhamia kwa wife na kukaa kwenye nyumba yake tukizinguana na beba malboro yangu begani huyoo uswazi

Hahaha! Kwanza wewe toka uondoe ile avatar nnayoipenda hata sikuchunuku tena ujue!
 
aya maaaa..i wish ungekuwa mamamkwe wangu
 
Inategemea kama mme hana kitu au kuna baadhi yavitu vinamiss then sio vibaya kwenda navyo, hata hivyo me nachojua NYUMBA NI MWANAMKE so ni wewe kama unataka nyumba yako ionekaneje ndio utaifanya so kwa mfano mie napenda myumba nzuri yenye vitu vizuri tena vya kisasa ivutie haswaaa.
MWANAMKE NYUMBA DIA KAMA UMEPEWA NENDA NA KILA KITU TENA UTAKAVYOKUTA GAWA UWEKE VIPYAAAAAAAAAAAAAAAA
 
mmmh wanaume wana kazi...mimi tutanunua wote
 
Kumpa nyumba mkweo ya kuishi na bintiyo ni ishara ya ukomavu wa makuzi na malezi ukiwa mzazi
mmmh wanaume wa sasa hivi kumbe ndo maana sipati mpenzi ..ngoja nianze kusema nina nyumba namalizia mbezi beach
 
Kumpa nyumba mkweo ya kuishi na bintiyo ni ishara ya ukomavu wa makuzi na malezi ukiwa mzazi

ofkozi,ikiwezekana wape,,,,,,wenyewe watajipanga watanunua tu kiwanja watajenga,,,,,,,
 

Lakini hii huwa haisaidii sana kwenye ndoa. binti anakuwa na kiburi cha pesa na kijana anakuwa na hofu ya pesa hizo ukweni,hakuna ndoa hapo!wazazi huwa tunaamini kuwapa kila kitu vijana au mabinti kunawapa push lakini kiukweli vitu vile huwa ni moja ya sababu kubwa sana zinakuja kuwavuruga baadae.though nia huwa ni nzuri lakini utekelezaji wake ni hovyo sana,maneno kama unaringia pesa ya kwenu,bila babako kukupa kiwanja ungejenga wewe,hunitishi lolote nilikuja hapa na kila kitu changu,and sort off!zawadi si lazima iwe in terms of tht mavitu,hebu tubadili namna ya kufikiri kidogo!
 
mmmh wanaume wa sasa hivi kumbe ndo maana sipati mpenzi ..ngoja nianze kusema nina nyumba namalizia mbezi beach

baada ya ndoa tuwakute TANDALE KWA BI NYAU,,,,,SI NDIO????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…