Dah! ulimwengu umebadilika sana na mambo yanaenda kutoka stage moja kwenda nyingine ni kama vile kutoka homo sapians to homo erectus etc... na kuendelea...
Kwa mtazamo wangu tangu nimeanza kupata ufahamu kwenye akili yangu zamani ili mwanaume aoe au apewe mke alikuwa anatakiwa awe na uwezo wa kulisha familia yaani mke na watoto watakao zaliwa. Awe na mahali pa kuishi either amejenga au amepanga ila sio nyumba ya familia au wanayokaa wazazi wa mume. Pia mume huyo alitakiwa awe na vitu kadhaa vya ndani ya nyumba ambavyo ni godoro, kitanda, angalau stuli au kigoda kwa wageni na mwanamke ili aweze kuolewa alikuwa anaangaliwa kwanza anauwezo wa kuzaa?, kulea watoto?, anajua kupika kwa njia zote yaani kuni, mkaa, jiko la mchina, anajua kufua, kuhudumia wagonjwa na usafi kwa ujumla. Na suala la mwanamke kuwa na kitu au kwenda na kitu kwa mume halikuwepo. Mtaji wa mwanamke kwenye ndoa ilikuwa ni uchapa kazi, usafi, kulea familia n.k. na mwanaume mtaji wake kwenye ndoa ilikuwa ni ujasiri, mtafutaji wa chakula na vitu vya familia.
Matatizo yanayotokea kwenye ndoa mengine yanafikia wenye ndoa kuachana na hapo kwenye kuachana baada ya miaka kadhaa ya kuishi kwenye ndoa ndipo ikaonekana mwanamke anafukuzwa na kirago cha nguo zake tu kama alivokuja wakati anaolewa. Hii imeipa shida jamii na kuifanya jamii ijihami au itengeneza njia za kumnusuru mwanamke ili ikitokea wanaachana au anafukuzwa basi mwanamke huyo awe na kitu cha kutoka nacho kwenye ndoa na si kufukuzwa na kirago cha nguo. Isingekuwa shida na matatizo yaliyowahi kutokea kwenye ndoa ambazo nimeshuhidia au wewe umezisikia basi hadi leo mwanamke angekuwa anatoka kwao na nguo tuu na khanga kibao na jukumu la nyumba na vitu vyake na kula likabaki kwa mwanaume. Ila kwa sababu ya matatizo hayo hata pale mume anapofariki ndugu wa mume kumnyanyasa mwanamke na kumfukuza mwanamke na nguo zake tuu wakati mali walizochuma mwamamke aliwekeza nguvu zake za uchapakazi, usafi, kulea n.k
Mabadiliko haya ndo yameleta leo wamama au wazazi kwa ujumla kuwafungasha mabinti zao wanapoenda kwa waume zao na vitu vyote vya ndani japo hapa uwezo unazingatiwa. Kwasababu wale ambao wanatoka kwenye familia duni bado wanaenda kwa waume zao na nguo tuu. Tatizo ni pale binti anapojishebedua kabla hata hajateswa na mume au ndugu wa mume, utasikia, ''eeeh usinibabaishe kama umenichoka naita fuso sasa hivi na ninasepa na kilakitu changu cha kichen party''. Hapo mwanaume akisikia hivi na akiangalia nyumba ibaki wazi anaona bora soo liishe na binti hapa anakuwa anakosea kwani unamfanya mwanaume kuwa mdogo na kutojiamini.
Ni vizuri kuwafungasha mabinti na vyombo vya ndani kwani jiko linaaminika ni sehemu ya mama na si baba ndo maana wanaume wachache sana hata waliojenga wanakuwa na vyombo vingi vya ndani. Utakuta hata kama anajipikia atakuwa na sahani moja au kikombe kimoja na sufuria moja. Kumpa binti sofa, dining table, coffe table, makabati ya ndani, godoro vitanda n.k vya ndani ili kuwasaidia wanandoa hawa kujikwamua kimaisha na si kwenda kunyanyasana.
Nimeongea kwa kireeefu but hope nimeeleweka, wanaume msiwanyanyase wake zenu waliokuja na nguo tuu na kuwakuta nyie wanaume na kilakitu ndani. Na nyie mabinti mnaoolewa na mmefungashiwa kila kitu na wazazi wenu yaani mmejaza fuso kwenda kwa waume zenu msijishebedue kwa kujiona nyumba nzima umeijaza wewe.
ZINGATIA: mwanaume na ampende mke wake, mwanamke na amtii mume wake, for sure ukiweza kuitimiza hii rule in all ur marriage life hutapata shida. Kila mtu atimize wajibu wake na kufanya yanayompasa. Play ur part in ur marriage and enjoy....!
Ni mtazamo wangu tuu.
Ever remaining,
Sakapal.