Kwenda Mpirani au kutembelea mafuriko?

Mkulu Mzee Mwanakijiji,

Unajua kila jambo linaenda na mahali husika. Hili unaweza kuliona jambo la ajabu kwa USA lakini kwa Afrika wala sio jambo la kushangaa. Watu wengi wako concerned na mafanikio ya timu ya taifa kuliko watu kwenye mafuriko huko Kilosa. Priorities zetu ziko mrama mno.

Hivi sisi hapa JF tumefanya nini kuwasaidia hao ndugu zetu wa Kilosa zaidi ya kukosoa tu serikali?

Ifike mahali sisi tuonyeshe kwa matendo kwamba tuko tofauti na serikali, kwa kufanya kwa vitendo yale ambayo tunailaumu serikali kushindwa kufanya.
 
hivi ninyi mnaona huyu jamaa zimetimia?!

anapenda sana kuonekana wala hajali mambo muhimu
 
unaweza kuwa sahihi kwa wakati lakini si mara zote.
Inashangaza kuona rais anaendelea na burudani zake wakati taifa lipo kwenye maafa ya msiba Mzito wa Mzee Kawawa, wakati huo Kilosa , Dodoma, sehemu za Lindi ni maafa mtindo mmoja. nilikua maeneo hayo hasa kilosa siku za karibuni, wee acha tu, mwache mkuu akamshangae Drogba maana watu kuangamia sio kipaumbele cha urais wake ila atawasili kule kutoa rambirambi na salaamu nyingi za huzuni.
 
Hivi sisi hapa JF tumefanya nini kuwasaidia hao ndugu zetu wa Kilosa zaidi ya kukosoa tu serikali?

Ifike mahali sisi tuonyeshe kwa matendo kwamba tuko tofauti na serikali, kwa kufanya kwa vitendo yale ambayo tunailaumu serikali kushindwa kufanya.
tunailaumu serikali ya Kikwete kwa kushindwa kutupatia maisha bora waliyo ahidi, tunaona wenzetu wanatenda ndivyo sivyo wakati waliomba kura wakijinadi wao ni suruhu ya matatizo ya kijamii na kiuchumi hapa TZ, SASA tunashangaa wenzetu wanaenda kushangaa Drogba wakati raia wanaendelea kuangamia na maji Kilosa na Dodoma, jamanii JK AMEZIDI .
 
Mkuu Mwanakijiji, kwa taarifa yako wapenzi wa kandanda tupo wengi sana humo na ajenda ya kumsakama mkulu kuhusu kabumbu haitaungwa mkono.

Mbona skandali ziko nyingi tu, si mtafute hoja nyingine?

Nadhani issue sio kwenda au kutokwenda mpirani. Issue ni kipaumbele (Priority). Rais ageweza kwenda asubui hadi mchana kwenye majanga ya kitaifa na jioni kuangalia kabumbu haina tataizo. Tatizo hasa ni kwmba Rais ana washauri wa kinajimu najimu kama Sheik Yahya ambao wanasema akienda na Helicopter uenda hasirudi. Kama Rais angekubali kupanda Helicopter kazi hii ingekwa rahisi mno na angeweza kurudi DAR na kujimwaga Uwanja wa Taifa. Bila helicopter ziara kama hizi ni ngumu kufanyika na siku zote Rais wetu ataonekana kupwaya.
 

Teh teh M.M
Muache muungwana ale vya mwisho mwisho
 

Celebrity president...
 
Uongozi wa nchi sio rais ni mlolongo mrefu hadi shinani .wananchi wanataka matatizo yao yatatuliwe kwa muda muafaka hawataki hotuba ya raisi kuhusu matatizo yao na mikono mitupu. Hata kama rais hajafika huko wakati huo huo wa maafa wateuzi wake wameshafika huko . Vile vile rais huyo lazima ataenda kutoa pole kama alivyofanya kule same haya mambo ya siasa za kuvizia(political sniping) hayajengi nchi upizani sio kufurahia uzaifu au kuomba makosa ya upande mmoja haumaanishi usahihi na umakini wa upande mwingine bali unatoa kibali cha upande mwingine kuboronga.
 
Labda anakumbukia enzi zile za foreign affairs!!
 
Mzee Mwkjj, haiingi akilini kwamba kweliwapo watu hapa JF ambao wanaweza kutetea vitendo vya rais bila kuwa na riziki fulani na Mheshimiwa (paid spin doctors, hanger on, opportunist etc).
Ingawa tunajaribu kutumia kila mbinu kumtetea lakini alichokifanya hakiwezi kutetewa. Ni kwamba ameonyesha wazi - HE DOES NOT CARE! He cares about his image and his pleasures... mi naamini kama tutampa kura (not collectively but individually) na hatumo katika kundi nililolitaja hapo juu basi ni wazi watz ni mabwege... sorry!!
 
Nadhani mjadala juu ya strengths na weaknesses za 'Muungwana' so far zimejadiliwa kwa mapana na marefu yote humu jamvini, naona kumekuwa na marudirudio mengi tu kiasi inaleta monotony sasa. Mimi nashauri (kama bado haijapendekezwa huko nyuma) sisi wana JF tuwe na position inayoeleweka kwa kutumia countable opinion polls........ so mods wetu waendeshe hiyo poll yenye motion "'Muungwana' anafaa kugombea 2010 au hafai" miongoni mwa wana-JF wote na jibu liwe 'Y' or 'N'. Polls ziwahusishe wana-JF ambao wamejiandikisha hadi kufikia muda pendekezo hili linatolewa tu (for obvious reasons!). Tusisubiri sijui REDET, etc tu. What about that??
 
Unaelekea kwenye ukweli (red)
 
..nchi haiwezi kufikwa na majanga kama yaliyotokea Kilombero na Same halafu mkamuona Raisi wake akiwa nje ya nchi akiruka kwenye mabembea au akihudhuria mechi za mpira.

..kwenye nchi za wenzetu ambako wanaheshimu UTU na MAISHA, mwenendo kama huu wa Raisi wetu wakati wa majanga ya kitaifa huwa hauvumiliwi hata kidogo.

..ni kweli Raisi anao wasaidizi. ni bora angewatuma wasaidizi wake kwenda kupanda mabembea Jamaica, au kubadilishana jezi na kina Drogba, na yeye asimamie relief efforts za Kilombero, na Kilosa.
 
How pitty, amakweli rais tuliye naye ni comedian!
 
Wadau, hivi tunamfanya Rais wetu kuwa ni Mzimu au Malaika (kuwa hana mwili)? Yaani kunapotokea jambo lazima awepo eneo la tukio? Nadhani tunakosea, yeye pia ana utashi na mapenzi yake binafsi na sil lazima aende kwenye kila tukio kwa wakati ambao tunadhani kwenye fikra zetu kuwa ni sahihi. Anaweza kuagiza Wasaidizi wake naye akatembelea eneo hilo siku atakapopata nafasi.

Naomba kuuliza, ni watu wangapi wamepoteza maisha huko Kilosa? Je, ni lazima Rais mwenyewe aende ndiyo tutaamini kuwa tatizo limeshughulikiwa?
 

Kuna mambo yanapotokea taifa linamhitaji Rais wake kuonesha uongozi; wakati watu zaidi ya 25,000 Kilosa peke yake hawana makazi tunahitaji kusikia Rais akilihamasisha Taifa; Hivi kweli wameshindwa kuhamasisha misaada kutoka sehemu mbalimbali za Watanzania tuchangie nguo, vyakula, n.k?

Naomba kuuliza, ni watu wangapi wamepoteza maisha huko Kilosa? Je, ni lazima Rais mwenyewe aende ndiyo tutaamini kuwa tatizo limeshughulikiwa?

siyo kwenda tu; ni kuonesha uongozi wa kutatua matatizo ya wahusika. hivi unafikiri wale watu wa Kongwa na Kilosa au kule Lindi walikuwa wanafikiria mechi ya Ivory Coast?
 
jamani JK is doing fine. kazi ya urais ni ngumu. tuwe na subira tu. tutafanikiwa.tunawaombea viongozi wetu kila la heri.
 
Inasikitisha sana kuona watu wamekufa na H.E hata salamu.Kweli hapo kuna utu?Huyo anayezungumzia kuwa wapenzi wa mpira ni wengi..-kweli umefikiria kwa makini na kutathmini kuwa mpira ni bora kuliko maisha ya Watanzania,tena hao 'wafuata upepo'??Hauoni kuwa kwenye maneno yaliyopo kwenye wimbo wa taifa "...dumisha uhuri na umoja..." yanapotea/kupoteza maana?Tuwe realistic,mechi haikuwa na ulazima sana na it was a wrong idea ya kuonekana kwenye hiyo mechi.Atoe basi hata salamu za rambirambi kwa walioathirika.Railway track nimesoma leo haitapitika for at least 3months,kweli bado tu kuna kumwonea hapa?Ukweli ni kwamba mambo kama haya ya vifo vya kitaifa,natural disasters, Mheshimiwa alitakiwa aonyeshe kuwajali hao waliompigia kura kufika hapo alipo.Sio kuzungumzia ushabiki wa kipuuzi,hili linabeba na linahusu utu kwa Mtanzania.

Inasikitisha na kutia hasira!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…