Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Katika vitu ambavyo alifeli Diamond ni kwenda huu mkoa uliojaa washirikina ,watu wenye vijicho na wasiopenda maendeleo ya watu.
Tangu Diamond aende Sumbawanga amekuwa mtu mwenye mikosi tele kila kukicha kuanzia siku ya kwanza alipotaka kufanya show ambayo waliahirisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na vilevile kuanguka jukwaani siku ya pili yake.
Mpaka sasa hivi bado hatuamini kama kuanguka kule kulikuwa kwa kawaida kutokana na uimara wa lile jukwaa.
Hilo halijatulia mara likajitokeza tatizo jingine la kuingia mgogoro na shirika la ndege ,
sakata hili bado halijapoa mara limejitokeza tatizo la kuzuiliwa kufanya show ndani na nje ya nchi kwa muda usijulikana sambamba na kuzuiwa kwa muendelezo wa Wasafi Festival kwa mikoa iliyobaki.
Diamond Platnums inabidi hili suala asilichukulie kirahisi rahisi ,hakuna namna inabidi atafute wataalam wamuangalizie nyota yake kiundani zaidi pamoja na kuing'arisha upya kwa maana watu wa Sumbawanga wasiopenda maendeleo yake watakuwa wameshaifunika nyota yake kwa njia za kijadi.
Siku zote dawa ya mshirikina ni kuwa mshirikina zaidi yake, hakuna namna Diamond inabidi atumie njia za kijadi haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi japo nina amini Diamond ni mkubwa kuliko hata BASATA YENYEWE.
Vilevile kufeli kwa Diamond kutaathiri vijana wengi sana haswa wafanya biashara na wasanii wengi ambao kwa kiasi kikubwa walitarajia kuingiza pesa kupitia Wasafi Festival .
Kila la heri Simbaaaaa tupo pamoja katika wakati huu mgumu unaopitia