Kwenu BAKITA, KISHIKWAMBI ikimaanisha Tablet imetoka wapi? IE The science of the origin of a word kishikwambi

Kwenu BAKITA, KISHIKWAMBI ikimaanisha Tablet imetoka wapi? IE The science of the origin of a word kishikwambi

It seems hujanielewa. Chimbuko la neno Kishikwambi ni lipi?
au mtu kwa vile uko BAKITA unaamua kuibatiza tablet jina la bibi yako! Kwamba bibi yangu anaitwa ekisitoroveti, basi tablet naibatiza jina la bibi yangu EKISITOROVETI 😀 😀 😀 😀 😀 Kukua kwa lugha hakuendi hivyo kwa dunia ya wasomi


Neno "lia" asili yake nini??
 
Kwanza nikuweke sawa tu neno KISHIKWAMBI/KISHKWAMBI halijaja na Sensa ni neno lipo siku nyingi sana... sisi walimu tunalo na tunatumia tangu ugawaji wa vishikwambi mashuleni enzi za Magu (mpaka posho ya mwl mkuu tunaita hela ya kishikwambi)

Halafu pili tuzungumze kuhusu neno lenyewe sasa ni kwamba maneno mengine yapo siku nyingi sana ila utumizi (mahitaji ya msamiati husika katika mazingira) ndo hakuna na mdomaana siku ikitokea mazingira ya kulitumia mtu akalitumia linaonekana kama geni/ajabu/kituko

Mifano hii hapa...
Neno MUBASHARA lipo siku nyingi sana lakini limekuja kupaishwa juzi tu kwenye ITV na kwenye michezo (mambo ya mpira)

Neno DEMKA Raisi ndo kalitia nguvu juzi pia likaonekana geni kwelikweli

Neno EXPANSION JOINT vilevile kwa upande wa Kiingereza

Neno ARAFA sikiliza redio wanavyolipaisha kama hujui unaweza kuona neno geni sana

Na kadhalika na kadhalika

Kama utataka kila neno uulize limetolewa wapi basi utakesha usikukucha... Uliza na haya basi

Kiswaswadu
Simujanja
Kimbaka
Au
Ua
 
Back
Top Bottom