Kwenu ITV badilikeni habari zenu za michezo hazivutii hata watangazaji hamuwapi uhuru wa kuvaa nguo za michezo

Kwenu ITV badilikeni habari zenu za michezo hazivutii hata watangazaji hamuwapi uhuru wa kuvaa nguo za michezo

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Hivi kwanini mkisoma habari za michezo watangazaji wanakuwa na haraka sana. Habari za michezo kama mpira wa miguu hasa ligii kuu ya Tz mnaipa air time kwa dakika chache ama sekunde kadhaa.

Ila habari za michezo ya bao mnatowa muda wa kutosha hadi kuwa hoji wahusika.

Pia ligi ya ujerumani mmetenga hadi kipindi kizima kukielezea. Badilikeni habari zenu za michezo hazivutii hata watangazaji hamuwapi uhuru wa kuvaa nguo za michezo ni kuchomekea mwanzo mwisho kama vile wana soma habari za kitaifa na kimataifa.
 
Yote ni sawa.

Ila hili la mavazi naona mnafanya mambo yawe magumu.
Kwani mtangazaji anaenda kusoma habari au kucheza mpira mpaka avae jezi.

Halafu jezi sio vazi la kazini.
Apige suti huoni wachambuzi wa azam ?
 
KAMA MSEMAJI WA IPP MEDIA PAMOJA NA ITV, NAPENDA KUSEMA HUYO MWENYE SHATI NA TAI NI MWANACHUO YUPO FIIELD. KUHUSU HABARI HUA TUNAJARIBU KIGUSIA TU MAANA MUDA HAUTOSHI UKISEMA UCHAMBUE HABARI KWA KINA UNAWEZA KUJIKUTA SAA ZIMA LIMEISHA UPO HABARI ZA BIASHARA. NI KUHUSA TU HIGHLIGHT TUSIJE KUHARIBU RATIBA YA VIPINDI VINGINE, NDO MAANA KUNA KIPINDI CHA MICHEZO TU AMBAPO MICHEZO HUJADILIWA KWA KINA
 
Back
Top Bottom