Kwenu ITV badilikeni habari zenu za michezo hazivutii hata watangazaji hamuwapi uhuru wa kuvaa nguo za michezo

Kwenu ITV badilikeni habari zenu za michezo hazivutii hata watangazaji hamuwapi uhuru wa kuvaa nguo za michezo

KAMA MSEMAJI WA IPP MEDIA PAMOJA NA ITV, NAPENDA KUSEMA HUYO MWENYE SHATI NA TAI NI MWANACHUO YUPO FIIELD. KUHUSU HABARI HUA TUNAJARIBU KIGUSIA TU MAANA MUDA HAUTOSHI UKISEMA UCHAMBUE HABARI KWA KINA UNAWEZA KUJIKUTA SAA ZIMA LIMEISHA UPO HABARI ZA BIASHARA. NI KUHUSA TU HIGHLIGHT TUSIJE KUHARIBU RATIBA YA VIPINDI VINGINE, NDO MAANA KUNA KIPINDI CHA MICHEZO TU AMBAPO MICHEZO HUJADILIWA KWA KINA
Umewahi kuangalia habari kupitia star tv..?, wao wanahabari zote hata kama ni juu juu ila wana cover kila sehemu
Kitaifa, kimataifa, bishara, michezo na burudani hapa naongelea michezo yote ndani na nje ya Africa
 
Umewahi kuangalia habari kupitia star tv..?, wao wanahabari zote hata kama ni juu juu ila wana cover kila sehemu
Kitaifa, kimataifa, bishara, michezo na burudani hapa naongelea michezo yote ndani na nje ya Africa
Star tv wana habari chache na zinazoelezewa kwa kina. ITV kuna habari nyingi zenye maelezo ya juujuu

Ni kitendo chs kupunguza habari ziwe chache na zenye maelezo ya kina au nyingi kwa kugusigusia wati wajue kinachoendelea
 
Ila tusema tu bongo vyombo vya habari bado sana,ukisikiliza bbc swahili au VOA, lisaa limoja tu inapangwa ikapangika,Habari zote kwa undani dunia nzima,vipindi vingine kama mijadala ya kisiasa ,kiuchumi, afyana mambo ya kijamii, maoni ya wasikilizaji,dondoo za kwenye mitandao ya kijamii na burudani ya mziki kwa kama sekunde 30 humo ndani.
Kwenye michezo utapata matokeo ya ligi mbali mbali kubwa na michezo inayofuata ndani ya dk kama 5 na inaeleweka.
 
Mbona PEDRO PINTO alikuwa anavaa suti lakini bado FIFA walimuona na kumchukua toka CNN na kumuajiri?
 
Yote ni sawa.

Ila hili la mavazi naona mnafanya mambo yawe magumu.
Kwani mtangazaji anaenda kusoma habari au kucheza mpira mpaka avae jezi.

Halafu jezi sio vazi la kazini.
Hata CNN na BBC sijawahi kuona mtangaxaji kavaa jezi wachen ushamba hv mbavotaka itakuwa kila habari inayosomwa mtangazaji akabadilishe vazi so siku nzima itakua kusikiliza habari na pendant na picha yenyew mfano habari za afya avae stethoscope na koti jeupe haaa patient habar za dunia mjue
 
Azam Media waliona hili gap la ITV wakalitumia. ITV kwenye michezo ni zero kabisa
 
Hivi kwanini mkisoma habari za michezo watangazaji wanakuwa na haraka sana. Habari za michezo kama mpira wa miguu hasa ligii kuu ya Tz mnaipa air time kwa dakika chache ama sekunde kadhaa.

Ila habari za michezo ya bao mnatowa muda wa kutosha hadi kuwa hoji wahusika.

Pia ligi ya ujerumani mmetenga hadi kipindi kizima kukielezea. Badilikeni habari zenu za michezo hazivutii hata watangazaji hamuwapi uhuru wa kuvaa nguo za michezo ni kuchomekea mwanzo mwisho kama vile wana soma habari za kitaifa na kimataifa.
Bongo mwenye mali akifa ndio basi tena hizo kampuni hazina muda
 
Back
Top Bottom