Kwenu ma-Legendary Utafanyaje umeenda ukweni na ukawadanganya kuwa umeokoka hivyo pombe hutumii?

Kwenu ma-Legendary Utafanyaje umeenda ukweni na ukawadanganya kuwa umeokoka hivyo pombe hutumii?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Wapo watu huwa wanapenda kuficha tabia zao hadi kwa wake zao.

Wapo hata humu ni walevi wanakunywa pombe ila wake zao hawajui kabisa wameshawadanganya wameokoka.

Niliwahi msindikiza rafiki yangu ukweni kwakwe ambae huwa tunapiga nae vyombo kama kawaida
Mke wake alikuwa amemwambia huwa hanywi.

Mimi aliponiambia kuwa hakikisha usikubali kuwa kama nawewe unakunywa pombe.

Nikamwambia mkuu mimi hua sijifichi nika muuliza kwani hata huko ukweni ni walokole? akasema mama ndo mlokole ila baba mkwe anakunywa. Nika mwambia basi utatuacha sisi na baba mkwe tule vitu wewe utavunga hivyohivyo.

Tulifika kama kawaida mke wake akasema hawanywi pombe na mimi nikaungamishwa humo kwa walokole nilichukia sana.

Basi mzee akatuletea vijana wa makamo kwa ajiri ya kutupa kampan then yeye naye akaleta wazee wenzake 4 hivi. Baba mkwe hakuwa mkubwa sana kwenye miaka55 hivi.

Tukiwa tunapiga story mara creti mbili za bia hizi hapa zikashushwa kwa wazee asee.sisi tukaletewa soda nikamwambia jamaa mambo gani tena haya kuongezeana sukari mwilini ?

Jamaa akaanza kucheka. Ukweli sikuvunga nikamwambia mmoja wa wenyeji wetu lete mzigo mkuu hizi soda hapana.

Jamaa nae kumbe alikuwa mdau asee mara akasema tuagize kabisa konyagi2 😂😂 Nikajibu nikweli.

Huyu jamaa yangu nilikuwa nikinywa hivi namuona kabisa anaitaka kwa hamu zote lakini ndo hivyo kashasema hanywi na ameokoka.

Alienda kulala saa3 tu kama kuku sisi tulipiga hadi saa5 ikabidi twende hukohuko kwenye Bar sisi na wale wazee pamoja na baba mkwe tulirudi usiku umeenda sana.

Picha hii chini imenikumbusha hilo tukio.

FB_IMG_1742070509017.jpg
 
Umenikumbusha kuna ndugu yangu (R.I.P) alikuwa akigombana na mke wake hali iliyokuwa inafanya mke kurudi kwao mara kwa mara. Jamaa alikuwa mlevi. Kuna siku kaenda ukweni yuko na best yake wamelewa wanapepesuka. Siku nyingine wameenda kama vile wako wazima kumbe wamejikaza mara ghafla wakaanza kutapika na kuishia kutia aibu. Cha ajabu jamaa aliishi na mke wake zaidi ya miaka 20 ndoani hadi pale kifo kilipowatenganisha
 
Wadau huwq wanaogopa kuwaambia lakini pombe haiwezi haribu ndoa kama unakunywa kama starehe. Ikizidi sasa ndo shida huwa inaanzia hapo
 
Back
Top Bottom