Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
Niliwahi kuleta kesi hizi hapa awali, ndipo akatokea jamaa mmoja nikaweza kuwapa namba zake na kuwaunganisha na mwanasheria wa humu. Jamaa huyo aliwasaidia sana hadi wakafanikiwa kushinda kesi zao. Hivi sasa mhusika huyo yuko nje ya nchi na atakuwa huko kwa muda mfupi.
Watoto wa familia hiyo walikuwa wanne: wawili ni wa mama wa nje na wawili ni wa ndoa halali. Baba yao alipofariki, msimamizi wa mirathi aliteuliwa, ambaye ni mdogo wa marehemu. Msimamizi aliwaita watoto wote na wakakubaliana kwa maandishi kuwa mali zote zigawanywe kwa usawa.
Hata hivyo, kabla ya kwenda mahakamani, watoto wa ndoa walikimbilia mahakamani kufungua kesi. Msimamizi alikwepa kufika mahakamani na akaenda mkoani. Baada ya miaka minne, alifungua kesi ya mirathi lakini aligoma kuwaalika watoto wa ndoa. Watoto hao baadaye walipata nyaraka za mirathi zenye muhuri wa mahakama na saini ya mhakimu.
Watoto wa ndoa walirudi mahakamani kuomba mahakama imwite msimamizi ili kufahamu kinachoendelea. Badala yake, msimamizi alipeleka suala hilo kwenye mahakama nyingine tofauti na ile aliyofungulia awali.
Walipoomba na kusoma nyaraka hizo, waligundua kuwa sehemu ya mali msimamizi aliwapa watoto wa nje, huku mali nyingine zikigawanywa kwa usawa.
Hapo ndipo mambo yalipoanza kuchukua mwelekeo mwingine. Watoto walirudi katika mahakama aliyofungulia msimamizi na kuomba aondolewe. Mahakama iliamua wachaguliwe watoto wawili kufungua kesi: mmoja akiwakilisha upande wa ndoa na mwingine upande wa watoto wa nje.
Ilibainika kuwa msimamizi tayari alikuwa na makubaliano ya maandishi na watoto wote, yaliyosainiwa mbele ya mwanasheria, yakieleza wazi kuwa mali zote zigawanywe kwa usawa.
Watoto wa kambo waliombwa kuwasilisha nyaraka zozote zilizoonesha kuwa marehemu aliwaandikia mali hiyo kuwa ni yao. Ilibidi niwaombe tena wale jamaa wawasaidie, na kwa kweli mmoja wao alitoa msaada mkubwa hadi walipofika walipofikia.
Baadaye, watoto wa kambo waliwasilisha nyaraka bandia wakidai ziliandikwa na kusainiwa na baba yao. Mahakama ilipochunguza, ilibaini nyaraka hizo zilikuwa zimeghushiwa.
Mahakama ikaamuru mali zote zigawanywe kwa usawa. Hata hivyo, watoto wa kambo walirudi tena mahakamani na kuwasilisha mkataba wakidai baba yao aliwauzia ile ardhi miaka ya nyuma alipokuwa anahitaji shilingi milioni saba kwa ajili ya matibabu. Uchunguzi ulifanyika tena na madai hayo yakakataliwa.
Kwa sasa, serikali imechukua kiwanja hicho na italipa fidia. Fedha hizo zinapaswa kulipwa kwa wale watoto wawili walioteuliwa kutoka kila upande, lakini mmoja wao yuko nje ya nchi
Tatizo linalojitokeza sasa ni kwamba mmoja anadai hawezi kusaini chochote kinachohusu mgawanyo wa fedha hizo. Pia, niliwashauri wafungue akaunti ya benki, lakini hilo linahitaji ushiriki wa wasimamizi wote wa mirathi.
Hapo ndipo changamoto ilipo, kwani msimamizi hatoi ushirikiano, na yule mwingine anayehitajika si msimamizi halali wa mirathi.
Mawakili na wasomi, tunaomba ushauri wenu. Hawa ni vijana yatima wanaohitaji msaada na mwongozo wa kisheria.