Kwenu Mawakili wasomi msaada na ushauri wenu wa Mirathi kwa vijana hawa yatima

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Niliwahi kuleta kesi hizi hapa awali, ndipo akatokea jamaa mmoja nikaweza kuwapa namba zake na kuwaunganisha na mwanasheria wa humu. Jamaa huyo aliwasaidia sana hadi wakafanikiwa kushinda kesi zao. Hivi sasa mhusika huyo yuko nje ya nchi na atakuwa huko kwa muda mfupi.

Watoto wa familia hiyo walikuwa wanne: wawili ni wa mama wa nje na wawili ni wa ndoa halali. Baba yao alipofariki, msimamizi wa mirathi aliteuliwa, ambaye ni mdogo wa marehemu. Msimamizi aliwaita watoto wote na wakakubaliana kwa maandishi kuwa mali zote zigawanywe kwa usawa.

Hata hivyo, kabla ya kwenda mahakamani, watoto wa ndoa walikimbilia mahakamani kufungua kesi. Msimamizi alikwepa kufika mahakamani na akaenda mkoani. Baada ya miaka minne, alifungua kesi ya mirathi lakini aligoma kuwaalika watoto wa ndoa. Watoto hao baadaye walipata nyaraka za mirathi zenye muhuri wa mahakama na saini ya mhakimu.

Watoto wa ndoa walirudi mahakamani kuomba mahakama imwite msimamizi ili kufahamu kinachoendelea. Badala yake, msimamizi alipeleka suala hilo kwenye mahakama nyingine tofauti na ile aliyofungulia awali.

Walipoomba na kusoma nyaraka hizo, waligundua kuwa sehemu ya mali msimamizi aliwapa watoto wa nje, huku mali nyingine zikigawanywa kwa usawa.

Hapo ndipo mambo yalipoanza kuchukua mwelekeo mwingine. Watoto walirudi katika mahakama aliyofungulia msimamizi na kuomba aondolewe. Mahakama iliamua wachaguliwe watoto wawili kufungua kesi: mmoja akiwakilisha upande wa ndoa na mwingine upande wa watoto wa nje.

Ilibainika kuwa msimamizi tayari alikuwa na makubaliano ya maandishi na watoto wote, yaliyosainiwa mbele ya mwanasheria, yakieleza wazi kuwa mali zote zigawanywe kwa usawa.

Watoto wa kambo waliombwa kuwasilisha nyaraka zozote zilizoonesha kuwa marehemu aliwaandikia mali hiyo kuwa ni yao. Ilibidi niwaombe tena wale jamaa wawasaidie, na kwa kweli mmoja wao alitoa msaada mkubwa hadi walipofika walipofikia.

Baadaye, watoto wa kambo waliwasilisha nyaraka bandia wakidai ziliandikwa na kusainiwa na baba yao. Mahakama ilipochunguza, ilibaini nyaraka hizo zilikuwa zimeghushiwa.

Mahakama ikaamuru mali zote zigawanywe kwa usawa. Hata hivyo, watoto wa kambo walirudi tena mahakamani na kuwasilisha mkataba wakidai baba yao aliwauzia ile ardhi miaka ya nyuma alipokuwa anahitaji shilingi milioni saba kwa ajili ya matibabu. Uchunguzi ulifanyika tena na madai hayo yakakataliwa.

Kwa sasa, serikali imechukua kiwanja hicho na italipa fidia. Fedha hizo zinapaswa kulipwa kwa wale watoto wawili walioteuliwa kutoka kila upande, lakini mmoja wao yuko nje ya nchi

Tatizo linalojitokeza sasa ni kwamba mmoja anadai hawezi kusaini chochote kinachohusu mgawanyo wa fedha hizo. Pia, niliwashauri wafungue akaunti ya benki, lakini hilo linahitaji ushiriki wa wasimamizi wote wa mirathi.

Hapo ndipo changamoto ilipo, kwani msimamizi hatoi ushirikiano, na yule mwingine anayehitajika si msimamizi halali wa mirathi.

Mawakili na wasomi, tunaomba ushauri wenu. Hawa ni vijana yatima wanaohitaji msaada na mwongozo wa kisheria.
 
Extensive narration, limited insight............
 
swali: huyu anaruhusiwa kufungua akaunti kama si msimamizi wa mirathi?

pili: je, ni lazima wafungue kesi katika ile mahakama waliyomwondoa msimamizi wao (mzee wao), au wanaweza kufungua katika mahakama ya chang’ombe?

maana waliambiwa na serikali waende kufungua akaunti ya benki, kisha wawapelekee namba ya akaunti yao ili fedha zitumwe huko.

baada ya kufungua akaunti, wameruhusiwa kurudi mahakamani kupata barua ya kuthibitisha kuwa akaunti ya marehemu tayari imefunguliwa, kisha barua hiyo ipelekwe serikalini.

baada ya hapo, serikali itaweka fedha (deposit) kwenye akaunti hiyo.

nafikiria pia kuwa watakaporudi mahakamani kutoa taarifa kuwa fedha tayari zimewekwa, mahakama itachukua hatua zake za kisheria kuhusu mgawanyo.

wazazi, wekeni sawa mambo haya kabla hamjaondoka huko. mtakuwa mmewasaidia sana watoto wenu na wengine wengi wenye changamoto kama hizi.
 
Unaposema msimamizi, ni nani? Na aliteuliwa na nani?
Anza hapo kwanza.
 
Unaposema msimamizi, ni nani? Na aliteuliwa na nani?
Anza hapo kwanza.
Wa mwanzo akuteuliwa na kikao ukisoma docs zao..walipomtoa watoto wakachagua makaka kusimamilq upande
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…