round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Ninawajua watu kama kadhaa walioenda kusoma nje ya nchi miaka ya 2012 hadi 2015, Wamesumbuka sana kwenye soko la ajira imewabidi tu wakubaliane na matokeo kwa kujiendeleza na shughuli nyinginezo
Kwenye ajira degree huwa ina uzito sana hivyo inabidi uwe makini kwenye uchaguzi wa vyuo, Masters haikubani sana ndio maana watu wengi wanaenda kuzisomea hata kwenye vyuo vya kata vya India ilimradi cheti tu chetu tu, sehemu ulikosoma sio sana tofauti na degree.
Kusomesha au kusoma degree nje ya nchi ni muhimu sana kuchagua chuo chenye jina, yani hata ukirudi bongo ukitaja chuo ulichosoma hakuna haja ya kugoogle, Mifano ni Havard, Oxford, Satanford, MIT, Cambridge, Yale, London , etc, Nje ya hapo kama ni vyuo vingine basi viwe ni vina hadhi ya kitaifa mfano kwa Uganda kuna Makerere university , India kuna IIT, Japan kuna university of Tokyo, n.k.
Waajiri wengi wanapenda kuajiri mtu aliesoma vyuo wanavyovijua, Kwa hapa Tz uwe umesoma ndani ya nchi au umesoma vyuo maarufu duniani, hivi hata wewe una kampuni yako mtu anakuja kukuomba ajira lakini chuo alichosoma hujawahi kukisikia tangu uzaliwe, utapata mashaka, hata ukitaka kumsaidia utahitaji ushahidi wa kutosha, mahojiano ya kina, ufanye research, n.k.
Sasa unakurupuka kwenda kusoma katika vyuo visivyo na majina huko India, Malaysia, Thailand, China, n.k. umeingia kwenye mfumo kwasababu ya kuona ada nafuu au umepata scholarship, jiandae kwa stress ukirudi Bongo. Kwanza, baada ya kuhitimu, unalazimika kwenda TCU (Tume ya Vyuo Vikuu) wathibitisha cheti chako, Ikiwa chuo ulichosoma hakifikii viwango vyao utapigwa block kuomba kazi kwa kutumia hicho cheti, Tangazo la kazi linatoka unaanza mchakato wa kuomba ajira, kuna waajiri / mabosi wakiona hawajikui chuo ulichosoma chap chap wanakata jina lako hawataki kujichosha kuanza kukifanyia research, Ikitokea umeitwa interview unaweza kuambiwa urudi tena TCU upate barua nyingine ya uthibitisho, Hata baada ya kupewa barua bado wanakutilia shaka na utaulizwa maswali mengi. Wakati huo wenzako waliosoma hata vyuo vya kawaida hapa Bongo hawakutani na hizo bugudha.
Sio lazima kusoma nje, Kama chuo unachoenda hakina umaarufu ni bora ubaki Tz unless una connection