Kwenu ndugu wanajamii na wana maendeleo

Kwenu ndugu wanajamii na wana maendeleo

Joined
Oct 24, 2019
Posts
34
Reaction score
32
Habari zenu wanajamii.

Utambulisho,


Mimi ni mwanachuo nipo Dar, nachukua shahada ya teknolojia nipo mwaka wa mwisho wa masomo hadi sasa.Hivo kutokana na mihangaiko ya hapa na pale na changamoto za maisha mwaka jana sikua na budi kusimamisha masomo ili kutafuta namna ya kujikim pamoja pindi nikiwa chuo, maamuzi hayo niliyachukua kutokana na hali niliyokua naipitia na baada ya aliyekua mfadhili wangu kusimamisha ufadhili kutokana na matatizo ya kiuchumi hivo basi ilinilazimu kusimama masomo mwaka mmoja ulokua umebaki ili nipambane namna ya kukidhi mahitaj binafsi ikiwemo ada

Nilifanikiwa katika struggle zangu kwa kiasi baada ya mjasiliamali baada ya kuuza asset zangu baadhi nilizokua nazo kwa mda huo,, nilianza kuuza genge na mkaa maeneo ya mabibo na Mwenyezi mungu akanisimamia nikaweza kupata kile nilichokipambania pia niliweza kufanya Saving ambayo imenisaidia mwaka jana ku resume studies nikiwa kama mwaka wa tatu sasa, ila changamoto bado napambana nazo mana nina genge langu ambalo binafsi naliendesha kwa mda ambao sina vipindi na ndilo limenisaidia wakati wote tangu semester imeanza hadi sasa inaisha.

Lengo Kuu.

Natamani kutumia taaluma yangu ili inisaidia kutoka katika changamoto hii niliyonayo ila mazingira ya kuanzia yanakua magumu kutokana na ukosefu wa vitendea kazi hivo basi naomba kibarua(kazi yeyote ile) ili mradi haidharirishi utu wangu.

Nina kiu ya kufanya kazi ya muda(tempo) pahala popote ndani ya mazingira yangu katika fani ya IT na kazi yeyote ile inayoendana na field hii ili kujipatia chochote kitu pia kupata mda wa jioni ziada kwa ajili ya kuhudhuria vipindi pale napohitajika, mwisho kuongeza ufanisi ndani ya taaluma yangu kwa muda huu hivo naomba msaada wowote ule.

Mtaji wa genge umeshuka kutokana na kua nategemea kila kitu na pia msingi(mtaji) ulikua mdogo.

Hivo basi mimi ni Mpambanaji sibagui kazi ili mradi niingize kitu pia kama nilivyotanguliza ombi langu hapo juu kua natamani sana angalau kibarua kitakachonisaidia kupata ufanisi ndani ya taaluma yangu mana kazi yoyote inayohusiana na mifumo(system) nazimudu pia kama ikitokea.

Shukrani
Mawasiliano:

Simu: 0787357219
 
Mkuu kwanza hongera kwa kujiongeza ,hongera sana
Hebu tuma maombi
Raha.com
Greenline technologies
Cats net
Wia
(Cheki zoom haya makampuni na mengine mengi
Tuma bila kuchoka)
Angalia uandishi mpya wa cv
Google ina kila kitu ila usiache mmbachao kwa msala upitao
Genge lilikubeba
Genge lilikurudisha shule
Usiliache kabisa
Liiimarishe kisha ukipata hicho kingine mweke mtu
(Hapa nitakupa msaada wa chanya wa mawazo)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza hongera kwa kujiongeza ,hongera sana
Hebu tuma maombi
Raha.com
Greenline technologies
Cats net
Wia
(Cheki zoom haya makampuni na mengine mengi
Tuma bila kuchoka)
Angalia uandishi mpya wa cv
Google ina kila kitu ila usiache mmbachao kwa msala upitao
Genge lilikubeba
Genge lilikurudisha shule
Usiliache kabisa
Liiimarishe kisha ukipata hicho kingine mweke mtu
(Hapa nitakupa msaada wa chanya wa mawazo)

Sent using Jamii Forums mobile app
asante mkuu!! nafanyia kazi ushauli wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom