Granite
JF-Expert Member
- Jul 6, 2016
- 268
- 624
Nakuja kwenu kwa Mara nyengine nikiwa na maombi ya kupata fursa ya kushiriki katika tasnia ya Ujenzi nikiwa ni kama Mhandisi wa Ujenzi, matamanio yangu ni kutumia ujuzi na Elimu yangu katika kuongeza thamani ya Kazi za Kampuni au taasisi, kushiriki katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa na kampuni au taasisi yanafikiwa kwa wakati uliopangwa, gharama nafuu na kwa ubora unaotakiwa.
Maeneo ninayotamani kupata nafasi ni katika ujenzi wa barabara, madaraja na mradi wowote ambao utanisaidia kuongeza ujuzi na mimi kunisaidia kampuni. Kwa walio na nafasi katika Miradi baadhi kama ifuatayo Naomba msaada wenu ipo baadhi nilipeleka CV sijafanikiwa kuitwa.
Mradi wa Barabara ya Kasulu-Kigoma
Mradi wa Bwawa la Nyerere - Mto Rufiji
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Salenda
Mradi wa Daraja la Busisi
Mradi wa Barabara za Mwendokasi
Ni Mingine Mingi, sijafanikiwa kupata mtu wa kunishika mkono naamini hapa naweza kupata msaada kwa mtu yeyote mwenye uwezo na nia ya kutoa msaada natanguliza shukrani. Lakini pia nipo tayari kushiriki hata katika Miradi ya kati na midogo.
Asanteni Wakuu