Kwenu TARURA; Vijana mliowapa mashine za tozo za parking wanazitumia vibaya

Kwenu TARURA; Vijana mliowapa mashine za tozo za parking wanazitumia vibaya

... ifike mahali akili itumike badala ya kufanya mambo kienyeji. Kwa mfano, mfumo wao ubadilishwe iwe ni 2-factor authentication; iwe combination ya namba ya gari na driving license. Ni rahisi tu.
Unaweza ukaandikiwa hata kama unamshusha mtu na kuendeleza safari sasa aisee
 
Na apart from 2-factor authentication; iwe combination ya namba ya gari na driving license. Waunganishe no za magari na mobile no zetu tupate sms alert.
Hii pia itapunguza matukio ya kihalifu,mtu akikufanyia uhalifu akateleza plate no,mobile no, NIDA ID,umemkamata mmiliki, simple
 
... another innovative idea! Ingawa by mobile no unamaanisha namba ya mmiliki? Maana sio mara zote gari inaendeshwa na mmiliki; inaweza ikaendeshwa na mke/mume, mtoto, dereva, mfanyakazi, n.k. ambao hao kila mmoja ana driving license yake.
 
Parking wangeziondoa kwenye hospitali ,inauma sana.unamsubiria dactari au upo upasuaji mdogo unakuta bei kubwa ya Parking. Kwanini wabunge msitusaidie wananchi.
Hadi hospitalini wanatoza parking....?Duh hii nchi ngumu kweli.
 
Parking wangeziondoa kwenye hospitali ,inauma sana.unamsubiria dactari au upo upasuaji mdogo unakuta bei kubwa ya Parking. Kwanini wabunge msitusaidie wananchi.
Yaani ndugu umeongelea point ya msingi sana.Mtu umepata dharula mgonjwa unampeleka hospitali hata hela ya matibabu hujui utatoa wapi unaanza waza nani umpigie simu akusaidie unatoka unakuta kashapiga vipicha vyake.Ifike wakati wajipange sehemu za huduma muhimu kwa jamii iwe free .tena kinachokera zaidi hata kutengeneza maegesho hawatengenezi ila ngoja wakute watu wamepaki mbio na vizibao vyao.jengeni maegesho ndiyo mfikirie tozo siyo nimepaki kwenye majani na miba halafu unakuja kunilipisha
 
Habarini ndugu zangu, huu mfumo mpya wa Parking ni mzuri sana ila hawa watu mliowapa hizo mashine wanazitumia vibaya.

Ipo hivi, kuna kijana anaitwa Anthony yupo mtaa wa Swahili(Kariakoo) yeye likija gari haijalishi litakaa mda gani, yeye uscan ya siku nzima na tiketi haweki na wala hamwambii mwenye gari kama kali scan gari, kwa kifupi jamaa wakati wa kuli scan gari anaakikisha dereva hamuoni.
Usiwaze,kuanzia July Halmashauri watafanya hiyo kazi
 
Mnalillia parking fees hii sasa hatari, ukiona unamiliki gari na bado parking fee inakuuma elewa kwamba wewe maisha yako ni ya chini na ulimiliki chombo cha moto wakati bado hujafikia hiyo levo.
Yaani unalialia kisa 5000 ya siku nzima..
Ndo maana siku zote huwa nawambia vijana kama unajijua kuwa kipato chako ni chini ya laki moja kwa siku panda tu daladala ili upunguze foleni mjini.
 
Umeuelewa uzi vizuri?
 
Tarura bado wanafanya hii mpaka julai mosi ndivyo nilivyojibiwa. Ni kweli hawa vijana wanafanya kazi kwa kuvizia mno kuna mmoja juzi nilimwamboia wee ilikuwa bado dakika 2 ifike saa 12.00 jioni akadhani sipo ndani ya gari maana nilikuwa ndiyo napaki akakimbia . Kinachokera kuviziana na hakuna risiti yoyote kuonyesha unadaiwa yaani ni wizi wizi flani hivi.
Kabisa huu mfumo wa hovyo sana, niajabu eti kusema wataalamu wamekaa na kubuni huo ujinga.
 
Ni wezi kweli,tena wasumbufu hasa!! Tena saiz wamezidisha aysee,wanachukua hela ya parking mpaka kwenye vijiwe zinakopaki canter,townace na Kirikuu...wakiona tu kuna kakijiwe wanakuja ku scan!! Daah serikali inafosi sana mapato aysee,sisiem ndio wametufikisha hapa aysee
Huku Morogoro, kuna siku niko Wallet Pub Kihonda nikakuta wapo..
 
Habarini ndugu zangu, huu mfumo mpya wa Parking ni mzuri sana ila hawa watu mliowapa hizo mashine wanazitumia vibaya.

Ipo hivi, kuna kijana anaitwa Anthony yupo mtaa wa Swahili(Kariakoo) yeye likija gari haijalishi litakaa mda gani, yeye uscan ya siku nzima na tiketi haweki na wala hamwambii mwenye gari kama kali scan gari, kwa kifupi jamaa wakati wa kuli scan gari anaakikisha dereva hamuoni.
Yani huyo dawa yake ndogo ukimdaba unampga bao hilo hadi ajikojolee.
 
Back
Top Bottom