Kwenu Wajumbe wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari, chukueni pointi 8 hizi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Tasnia ya habari imevamiwa na magugu maji. MNA JUKUMU LA KUNG'OA MAGUGU

Na N'yadikwa - Milima ya Umalila

Hongereni kwa kuteuliwa.

Kwa kuzingatia changamoto za uandishi wa habari na utangazaji nchini Tanzania, Bodi ya Ithibati kwa Waandishi wa Habari ina majukumu muhimu ya kuhakikisha sekta ya habari inasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.

Nayatafakari yafuatayo kama baadhi ya mapendekezo ya kazi zenu za kipaumbele ambazo chini ya uongozi mahiri wa Tido Mhando wanabodi mtaweza kuanza kufanyia kazi na kuipa heshima tasnia ya habari kwa mara nyingine baada ya heshima hiyo kupokwa na wavamizi kwa kigezo cha eti "usupastaa".

Yafuatayo:-

1. Kusimamia Mchakato wa Kuwathibitisha Waandishi, Watangazaji, maafisa habari, wahadhiri wa vyuo vya habari, na yeyote anaejuhusisha na masuala ya habari kama taaluma rasmi.
- Kipaumbele cha Kwanza
Kuhakikisha kwamba waandishi wa habari na watangazaji wote wana taaluma wanapata ithibati na kuthibitishwa na Bodi kwa mujibu wa sifa na viwango vilivyowekwa na Sheria ya Huduma za Habari, 2016.

- Hatua za Kuchukua:
- Kuandaa utaratibu rasmi wa kupokea maombi ya ithibati kwa waandishi wa habari na watangazaji.

- Kushirikiana na taasisi za elimu ili kuhakikisha wahitimu wa vyuo vya uandishi wa habari wanakidhi vigezo vya ithibati.

2. Kuweka Vigezo na Masharti kwa Watangazaji Wote

- Kipaumbele cha Pili
Kushughulikia tatizo la watangazaji wasiokuwa na taaluma kwa kuweka vigezo maalumu vya kitaaluma na maadili kwa watangazaji wanaopaswa kuajiriwa kwenye vyombo vya habari.

- Hatua za Kuchukua:
- Kufanya ukaguzi wa watangazaji waliopo na kutoa mwongozo kuhusu mafunzo ya lazima kwa wale wanaohitaji kuboresha ujuzi wao hasa wasiokuwa na taaluma.

- Kuanzisha taratibu za utoaji wa leseni za utangazaji kwa watangazaji wenye vigezo maalumu vya kitaaluma.

3. Utoaji wa Leseni kwa Maafisa Habari

- Kipaumbele cha Tatu

Kuhakikisha maafisa habari katika taasisi za umma na binafsi wanapata leseni ya kuthibitishwa kama wataalamu wa habari.

- Hatua za Kuchukua
- Kuanzisha utaratibu wa maafisa habari kusajiliwa na Bodi na kutoa leseni kwa wale waliopitia mafunzo rasmi kv waliosoma kozi relevant kwa kazi za PR mf Mass Communication, Journalism, PR na Marketing, Communication Science etc.

- Kushirikiana na taasisi za mafunzo ya uhusiano wa umma na mawasiliano ili kuhakikisha maafisa habari wanaendana na viwango vya kitaaluma vinavyohitajika. Au kushirikiana na NACTVET na TCU kuhakikisha vigezo husika vinazingatiwa kwa PROs

4. Kufuatilia na Kusimamia Uzingatiaji wa Maadili ya Uandishi wa Habari

- Kipaumbele cha Nne
Kuweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha waandishi wa habari na watangazaji wanazingatia maadili ya kitaaluma na mwongozo wa maadili uliowekwa na Sheria ya Huduma za Habari, 2016, Sheria ya EPOCA, nk

- Hatua za Kuchukua
- Kutengeneza mpango wa ukaguzi wa vyombo vya habari ili kuhakikisha wanafuata kanuni na maadili ya uandishi wa habari.

- Kutoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa maadili na sheria zinazowasimamia.

5. Kuhamasisha Mafunzo Endelevu kwa Waandishi na Watangazaji
- Kipaumbele cha Tano
Kuanzisha programu za mafunzo endelevu kwa waandishi wa habari na watangazaji ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia na kitaaluma.

- Hatua za Kuchukua
- Kuandaa warsha na semina za mara kwa mara kwa waandishi wa habari kuhusu mabadiliko ya kidigitali, matumizi ya teknolojia za habari na usalama wa mitandaoni. Pia, uandaaji wa maudhui bora yanayoifaa jamii ya Tanzania.

- Kutoa motisha kwa vyombo vya habari vya ndani vya Tanzania kushirikiana na Bodi ili kusaidia waandishi wa habari na watangazaji kupata mafunzo ya mara kwa mara.

6. Kushughulikia Malalamiko na Nidhamu
- Kipaumbele cha Sita
Kuanzisha utaratibu rasmi wa kushughulikia malalamiko yanayohusu waandishi wa habari na watangazaji kuhusu ukiukwaji wa maadili au viwango vya taaluma.

- Hatua za Kuchukua-
Kuweka mfumo wa kuripoti ukiukwaji wa maadili na sheria za habari kwa umma na wadau wa sekta ya habari.

- Kutekeleza hatua za kinidhamu kwa waandishi wa habari na watangazaji watakaopatikana na makosa ya kitaaluma.

7. Kuhamasisha Ushirikiano na Wadau wa Sekta ya Habari

- Kipaumbele cha Saba
Kupanua wigo wa ushirikiano kati ya Bodi na wadau wengine wa sekta ya habari kama vile vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, na taasisi za elimu.

- Hatua za Kuchukua
- Kuandaa mikutano ya mara kwa mara na wadau ili kupata maoni na ushauri kuhusu mwelekeo wa sekta ya habari na utangazaji.

- Kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha viwango vya uandishi wa habari nchini.

Soma Pia: Tido Mhando Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari

8. Kuboresha Mazingira ya Kazi kwa Waandishi wa Habari

- Kipaumbele cha Nane
Kutoa mapendekezo kwa serikali na vyombo vya habari kuhusu kuboresha maslahi na mazingira ya kazi kwa waandishi wa habari, ikiwemo afya, usalama, na uhuru wa kufanya kazi.

- Hatua za Kuchukua

- Kupendekeza sheria au sera zinazohusu ulinzi wa waandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao, hususani wanaposhughulikia habari zenye maslahi kwa umma.

Na;

- Kutoa mwongozo kuhusu usalama wa waandishi wa habari katika mazingira ya hatari na kutilia mkazo utoaji wa bima kwa waandishi.

Kwa leo chukueni hizo pointi nane.

Kwa kuzingatia mapendekezo haya, Bodi ya Ithibati kwa Waandishi wa Habari inaweza kusaidia kuboresha taaluma na maadili katika sekta ya habari na utangazaji nchini Tanzania.
 
Ukichunguza kwa umakini Sana kuhusiana na madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo ya Waandishi wa Habari hasa ni Serikali kutaka kuwadhibiti Waandishi wa Habari ili kusudi Waandishi wote kabisa wawe Machawa na Waimba Mapambio ya Kusifu na Kuabudu Watawala pamoja na Vibaraka wao. Nothing good!

Waandishi wa Habari watakaokataa Kusifu na Kuwaabudu Watawala na Vibaraka wao basi watakumbana na Visa na majanga ya Kufungiwa Leseni zao, Kunyang'anywa pamoja na Kufutiwa Usajili wa kufanya kazi za Uandishi wa Habari hapa Tanzania.

Kwa hiyo Waandishi wa Habari wajiandae Kisaikolojia kukabiliana na janga hili jipya linalowanyemelea.
Wakumbuke kisa Cha Fatma Karume kufungiwa Leseni ya Uwakili hapa Tanganyika.

Waandishi wa Habari wa Tanzania sasa watakuwa na kazi moja tu ya :
Kusifu na Kuabudu Watawala!
 
Mtazamo wako
 
Back
Top Bottom