Kwenu Wanaume: Vitu vichache wanavyoangalia Wanawake kabla hajaruhusu umuoe ama kujenga uchumba wa kudumu

Ukimuambia mwanamke ataje sifa za mwanaume anayemtaka ,matokeo yake anataja sifa za viumbe ambao hawapo duniani
 
Namba moja ni upendo, hayo mengine ni ziada tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo siku hizi kila mtu anahitaji mwenza mkamilifu, utampata wapi wewe.
Ila ukiwa hujao au kuolewa unaona hakuna mwanamke wa kuoa wala mwanaume wa kuolewa naye, ila ukishaoa au kuolewa hii mentality ni mfu, hii ni kwa uzoefu wangu. Wanawake wa kuoa tena wenye maadili wapo tena wengi tu na wanaume wenye maadili wapo wengi tu.
 
Hapo kwenye akili mbona hujaleta kifungu na inayosemwa ni akili ya aina gani huwa hiki kipengele sikielewi kabisa
 
Hapo kwenye akili mbona hujaleta kifungu na inayosemwa ni akili ya aina gani huwa hiki kipengele sikielewi kabisa
1Petro 3:7
Kadhalika ninyi waume,kaeni na wake zenu kwa akili na kumpa mke heshima,kama chombo kisicho na nguvu na kama warithi pamoja wa Neema ya uzima,kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.


*Akili gani hiyo sasa inahitajika?

Waefeso5:25
Enyi waume,wapendeni wake zenu,Kama Kristo Naye alivyolipenda kanisa,akajitoa kwa ajili yake.


*Kumbe akili inayohitajika ni kuwapenda.
Nampendaje sasa?


1kor 13:4-7
Upendo;
•Huvumilia
•Hufadhili
•Hauhusudu
•Hautakabari
•haujivuni
•Haukosi kuwa na adabu
•Hautafuti mambo yake
•Hauoni uchungu
•Hauhesabu mabaya
•Haufurahii udhalimu
•Bali hufurahi pamoja na kweli
•Huvumilia yote
•Huamini yote
•Hutumaini yote
•Hustahimili yote

AKILI=UPENDO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…