Kwenu wanaume

Kwenu wanaume

Jolie Jolie

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
7,406
Reaction score
13,806
RATIBA YA WANAUME WA DAR W/KEND
1.Asubuhi-Chai na soseji moja na yai la kuchemsha
Baada ya chai anaangalia tamthiliya ya kifilipino[emoji2][emoji2][emoji2]
2.Mchana-Chips mayai na mayonaiza na mshikaki mmoja.
Jioni jioni anaenda kufanya pedcure[emoji4][emoji4] pale mwenge. Baada ya hapo dili za kutafuta hela zinaendelea......(usiulize anatafutaje, wengi wanajua kuzisaka hata fake)

3.Usiku-Mchemsho wa maini[emoji13][emoji13]. Halafu anakazia na castle light au redbul

RATIBA YA MWANAUME WA MKOANI

1.Asubuhi- Kaamka saa 11 kaanza kukata majani ya ng'ombe then saa moja asubuhi CHAI MAGIMBI,MIHOGO YA KUCHEMSHA NA KARANGA MBICHI.
baada ya hapo analimia limia majani yanayozunguka nyumba.......

2.Mchana-Ugali wa Ulezi,Muhogo au dona na Mchicha+Maharage+Mapapai+ mtindi wa maana.
Baada ya hapo mishe zingine zinaendelea......

3.USIKU-Kabla ya kurudi home anakazia safari,au castle Lager, au BALIMI....then anaenda kula chakula chepesi cha kulalali a DONA NA MLENDA!

Sasa hapo angalia tofauti. Ndo mana wake zenu wakitoka dar kuja kusalimia kwa wazazi wao mkoani hawataki kurudi dar! Mana huko hawapati wanachostaili....Niwape siri huyo akikutana na EX wake wa mkoa mwenye ratiba kama hiyo anakuona wewe kama mdada mwenzie.......HUJIULIZI KILA MGANGA DAR ANAJIDAI KUTIBU NGUVU ZA KIUME?Mkoani hakuna waganga wa hivyo. "Usimwache mkeo aje likizo peke yake mkoani"


#wanaume_wa_dar_povu_ruksa
#mi_nipo_nyumbani_njoo_unipige
 
Acha zako basii mbona mimi siishi ivo?
Asubuhi chapati 2-4 mchana nusu kilo yangu ya dona na kibua..
Nikikosa chapata maandazi 8!

Labda kwakua natokea mkoani
 
Acha zako basii mbona mimi siishi ivo?
Asubuhi chapati 2-4 mchana nusu kilo yangu ya dona na kibua..
Nikikosa chapata maandazi 8!

Labda kwakua natokea mkoani
We ni mwanaume wa dar au wa mkoani?
 
Ndiyomaana wanaume wa mikoani wakifika Dar wanasababisha vyoo vi block. Akikaa hotelini mwenye hoteli kesho yake anaita vijana wa kuzibua vyoo.

Usipime wawe ni shemeji zako wawili wamekutembelea. Mkate mmoja na mayai sita wanaonja breakfast wakisubiri chapati na mchemsho.
 
Nadhani hawa ni kwa wale ambao umekua na kucheza nao toka utotoni.ila wengine kwa asili ya tutokako tume-copy life la kule tukaja kuliishi ndani ya town hii hii,sikumbuki ni lini nimeangalia Tv asubuhi au mchana labda jpili achilia mbali kuangalia hizo Philippine series.
 
Back
Top Bottom