Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

Umejuaje mkuu
Computer engineering analamba karibu kila kazi ya IT, Computer science, ict, n.k. hap computer science na IT kuna kazi kama za kufunga mitambo ya simu upande wa hardware hawatii mguu hapo

Computer engineering anapiga electonics, hardware, software lakini computer science na IT wapo sanasana kwenye software tu ila computer science imeizidi IT
 
swali ni kwamba umejuaje mkuu😅
Because ninajua mkuu.

Computer engineering = Hardware & Electronics + Software + Math

Computer science = software + math

IT = kujua tu namna ya kutumia computer ili kusaidia makampuni mambo kama maintanance, kuwachagulia software nzuri, kupiga window, n.k.

Kwa hio hapo King ni computer engineering, Queen ni Computer science, mtoto ni IT
 
Watoto wasome wanachopenda na wawe na skills. Kozi zote ni sawa iwe HR, ACCOUNT, ENGINEERING, SCIENCE, IWE BEE KEEPING, IWE KILIMO, IWE SHERIA. Kozi zote ni sawa. Kuhusu board, board ni kichaka cha kupiga pesa zetu tu. Watu wanaajiriwa bila hata kupitia board.
 
Computer science ndio yenye ajira nyingi na ndio nzuri zaidi
 
Sio bee keeping ni book keeping.

Tunachoangalia ni Probability yani makadirio ya uwezekano kama yanaridhisha.

Hata mtoto wako akisema anaacha shule awe kama Diamond platnumz ni kwamba haelewi chochote kuhusu probability, kaa nae chini kwanza mwambie Diamond ni msanii moja tu, wasanii wengine hali zao vipi ?

Na ndivyo ilivyo hata kwenye hizi kozi, kuna kozi zingine zina probability angalau yenye nafuu kupata ajira ama kujiajiri lakini kozi zingine zina probability ndogo
 
Bachelor of Science in BEE KEEPING. BSc in Beekeeping Science and Technology is Undergraduate Programme which is pursued within the duration of 3 Years. This program is initially provided at College Of Agricultural Sciences And Food Technology found at University of Dar Es Salaam.
 
Waambieni ukweli kazi hakuna serikalini wala sekta binafsi


Ewe mzazi kama hukujipanga kimaisha na huna cha kuwarithisha wanao na hawana muelekeo mzuri wa maisha imekula kwako na kwa wanao.

Sisitizeni wazazi waandae urithi mzuri kwa vizazi vyao, urithi mzuri ni mali na sio elimu, elimu ni wajibu wa mzazi kutimiza kwa watoto lkn urithi wa kweli ni mali na sio porojo.

Waandaeni watoto wenu kiakili na kisaikolojia, mtoto wako anapofel shule usimlazimishe, muulize anataka jambo gan nje ya shule ndilo umuhangaikie, huo udactar sijui madudu gan kama mtoto wa kayumba huna connection basi sahau labda uweke mategemeo kwenye ndumba uchawi na bahat nasibu za waganga wakina mwamposa na wale walozi wapiga ramli chonganishi na matunguri.

Narudia tena, ewe mzazi na unaetegemea kuja kuwa mzazi, urithi wa kweli kwa mtoto/watoto ni MALI na sio porojo za shule na upumbavu mwingine, maendeleo yako wewe mzaz ndiyo yatakayo amua dira ya kizazi chako na watoto wako na familia zao na koo zao hapo mbeleni, elimu is nothing bila ya maendeleo yako mzazi, elimu haina maana kama huna dira ya urithi kwa wanao.

Tafuten pesa, tajiri na mtu mwenye maendeleo hana hizi mindset za kuwafanyia bahati nasibu watoto wake kuwabahatishia ama kuwabetisha ktk suala la elimu ili wapate ajira.

Mwanao akijua kusoma na kuandika achisha shule pekela short-coz za lugha za kichina, kihindi, kifaransa, kirusi na lugha zinazomatter ktk soko la kibiashara, achana na mambo ya shule, huko mnapoteza muda, kidooogo kama mtoto anapenda shule peleka akasomee Computer maana huku ndiko dunia iendako, tofaut na hapo usipoteze pesa zako na muda wako kumsomesha hizo takataka mashuleni ambazo zitamtesa akili na ajira hatopata ng'oooo

Ukweli mchungu...
 
Hebu kwanza niambie ni lini mara ya mwisho serikali imetoa hizo ajira za ufugaji wa nyuki ?

Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba hapa tunzazungumzia kozi amabazo zina probability nzuri ya kuajiria ama kujiajiri na kipato walau cha kumweka mtu vizuri.

Mtu hata akiitwa engineer flani, Dokta flani, Lawyer flani, Cpa flani, hata picha inakujia tu kwamba angalau uchumi wake si haba.
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Peleka chuo, hizo five&six ziliwekwa kuwapotezea watoto muda wakakue huko wachanganyikane na raia wa jamii tofauti kuondoa ukabila pia kuwafanya wapate wachumba huko, tofauti na hili level ya Advanced schools haina faida yoyote zaid ya kupoteza muda..peleka chuo
 
Hata hizo kozi Sio garantii ya soko la ajira.
Muhimu wasome huku ukiwaandalia mazingira pia ya kesho Yao.
Mfano kuwapandia miti,kuwashikia maeneo wakimaliza chuo yanakuwa ni marketable wanapata msingi wa kuanzisha ujasiliamali wa kile walichosomea.
Pia wapate hata mtaji wa kujaribu kwenda kujaribu hata nje ya nchi maisha
 
Naona hujasoma post umekurupuka ku comment baada ya kusoma kichwa tu.

Kasome post nzima maana hujasoma vipengere muhimu kama Probability na kujiajiri
 
Ndio muwashawishi ndugu zenu wasome vitu vya maana kama hivi, leo hii tupo tunaojuta kwenda kusoma vyuo coz ambazo kimsingi tuliona zina heshima kuliko wale waliokwenda VETA na Ufundi kumbe wao ndio wana nafuu kuliko sisi.

Tuendako huko kuna baadhi ya coz na masomo kama sio kufutwa basi yatatakiwa kuwekewa wasomaji wachache sana ambao watashikilia ajira za wachache wanaong'atuka serikalin na kwenye Mashirika.
 
Tafadhalini muwe mnasoma post nzima na kuelewa kabla hamjacomment

Nimeelezea sana ishu ya Probability kwenye post rudi kasome upya.

Hakuna guarantee kwenye probability.
 
Naona hujasoma post umekurupuka ku comment baada ya kusoma kichwa tu.

Kasome post nzima maana hujasoma vipengere muhimu kama Probability na kujiajiri
Hakuna cha probability wala nini ungesoma andiko langu ungeelewa zaidi maana nimesisitiza, nje ya mataraijio yenu ya kipumbavu kwanini kama wazazi msikazane kutafute hela ili hao watoto wenu msiwafanyie bahati nasibu kuwasomesha mambo ambayo hata hamna uhakika kama yatawasaidia, mara nyingi mimi hutoa maoni ambayo ni BEYOND YA UELEWA WA WATU WAJINGA NA WAJUAJI, ukiusoma ujumbe wangu utapata picha ya kitu kitakachosolve tatizo la ajira kwa watoto wa masikini wasio na uelekeo wa maisha.

Siku zote watoto wa ninyi masikini ndio huangaika kubahatisha muelekeo wa ajira badala ya kuhangaika kuijenga future ya watoto wenu nje ya bahati nasibu za elimu, mtu mwenye maendeleo hachagui la kusoma maana anajua by any means lolote atakaolosoma litamsaidia ktk kazi zake, nje na hapo mpo masikini ambao mnasoma ili mpate kazi muendekeze cycle ya umasikin ktk familia kwa kutegemea ajira.

sasa kukwepana na hayo kwanini usiufuate ushauri wangu ambao uko Juu ya uelewa wako na wajinga wengine kwa kutafuta sana pesa na maendeleo yatakayozifanya familia zenu zijiepushe na matatizo ya kufanya betting ktk maisha ya watoto?

Ni masikini tu ndio mnaosoma ili mpate ajira, shika ushauri wangu japo masikini huu ushauri hawaupendi maana unauma sana, matajiri tu na wenye maendeleo ndio hutumia huu ushauri.
 
Mkuu si useme ulikua hujui kuna course ya BEE KEEPING...unazuga hadi unachekesha hahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…