Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

Doctor, engineer au Lawyer ikishindikana angalau somea uhasibu.

Niseme tu ya kwamba wapo wanaosomea hata degree ya kifaransa wanapata ajira hapahapa Tanzania lakini Probability (makadirio ya uwezekano) ya kupata hizo kazi ni ndogo.

Lakini hizi kozi tajwa angalau zina Probability (makadirio ya uwezekano) nzuri ya kuajiriwa sambamba na malipo mazuri, vijana wengi tu wapo makazini kwenye hizi kazi na hali zao kiuchumi si haba. Haimaanishi kwamba wooooote wanaajiriwa ama kujiajiri, LA HASHA!! wengine wanasugua benchi mtaani lakini kozi hizi angalau zina nafuu kwenye Probability (makadirio ya uwezekano) ya kuajiriwa ama kujiajiri, Mambo hayana formula lakini ni vema kufanya kitu walau kina Probability (makadirio ya uwezekano) nzuri, hata kwenye muziki yupo Diamond platnumz lakini probability ya mtu aliemaliza form 4 aanze kuimba ategemee muziki pekee kuendesha maisha ni ndogo sana, ni heri adungue mgahawa wake angalau kuna Probability nzuri ya uhakika wa kuendesha maisha yake.

Madaktari wana bodi yao Medical Council of Tanganyika, jina la daktari linaanza kwa Md flani. Afya ndio mtaji jamani, Uhitaji wao ni mkubwa, mishahara yao si haba, na mtu akiweza kujiajiri afungue hata sehemu yake kama zahahanati ni jambo la neema kwa jamii maana huduma za afya bado zipo chache.

Engineers wana bodi yao, Engineers Registration Board, jina la daktari linaanza kwa Eng, flani. hawa ndio mafundi mitambo, wahandisi wa barabara, wanaojenga majengo, wahandisi wa computer, n.k. huku waliojaa wengi ni wanaume tofauti na kwengine, kwa wanawake nadhani huwa wanapata upendeleo maalum kwenya ajira.

wanasheria wana bodi yao, Tanganyika law society, jina la daktari linaanza kwa wakili flani. hapa wapo wale mapilato wanaotembelea gari zimeandikwa J, wapo washauri wa sheria wa kulipwa, wapo mawakili, wapo wenye law firms zao, n.k. asikwambie mtu yani watu wapo tayari kutoa chochote kukwepa maisha nyuma ya nondo, kudai haki zao, kujitetea, n.k. wanasheria ndio wanufaika hapa.

wahasibu wana bodi yao, National Business Aviation Association, jina la daktari linaanza kwa Cpa flani. ndio wanaohusika na usimamizi wa fedha kuanzia mapato, matumizi, faida , n.k. wapo kwa wingi karibu kila shirika maana pesa bila usimamizi ni hatari, kwa cpa kima cha chini cha mshahara inasemekana ni milioni 1.3, kwenye kujiajiri kuna accounting firms hawa ndio wanahusika na kusimamia hesabu za makampuni, kusaidia watu kupeleka tax returns TRA, n.k. pesa ipo.

Ni kipimo cha kuonyesha uzito wa haya mambo, bodi hizi zipo tangu zamani na ili uwe mwanachama inabidi ufanye mitihani yao.

Pia ni inapendeza kuanza kusomea taaluma mapema vyuoni baada ya kuhitimu form 4, diploma miaka mitatu kisha unaingia degree pamoja na wale waliotokea sekondari form 6, kumbuka form 6 ni elimu ya sekondari wala sio elimu ya taaluma ndio maana mtu aliesoma form hawezi kuajiriwa bila degree lakini mwenye Diploma anaweza kupata ajira bila degree, Pia kazi za degree ni za wote waliotokea form 6 kwenda degree na wale form 4>diploma>degree lakini kazi za diploma ni maalum kwajili ya walioanza kusoma chuo baada ya form 4, nchi zilizoendelea kama Kenya walishafuta form 5 na 6 ni moja kwa moja kuanza kusomea taaluma chuoni.

Wanaijeria ndio jamii ya waafrika walioelimika zaidi wanasisistiza watoto wao wasomee Doctor, Lawyer ama Engineer, waisrael na wahindi ndio makundi yenye wasomi zaidi wanasisitiza watoto wao wasomee Doctor, engineer ama Lawyer, hio accountant.
Nimegundua wewe una elimu ya kuungaunga , yani unafundisha watu uoga wa maisha wasomee ma udaktari eti mshahara sio haba. Akili za kimaskini. Alafu national aviation board inahusiana vipi na bodi ya uhasibu?
 
Ndio unavyojidanganya? Umahiri kwenye kesi ni kopaji ukiachana na kukariri ,Bora nisome psychology naweza kujiajiri fasta kuliko hiyo Sheria
Naweka facts tu hapa.

Hio psychology kwa wabongo mwamko bado mdogo, mtu hadi anyanyue mguu aende kwa mwanasaikolojia bado sana, wengi wanaenda kwa marafiki, ila mtu akipata kesi ni fasta tu anatafuta wakili.
 
Mwanangu nataka acheze kandanda awe Kama Cristiano Ronaldo, au Lionel messi 😀😀😀😀
 
Mwanangu nataka acheze kandanda awe Kama Cristiano Ronaldo, au Lionel messi 😀😀😀😀
probability ndogo sana, hapa tz nzima wachezaji wapo kibao ila waliofanikiwa kuwa na mishahara ya kuwatunza vizuri hata wakistaafu hawazidi kumi
 
Unaongelea hawa madaktari waliofanyiwa figisu ya kunyimwa leseni ya kufanya kazi? bongo fitna zishakuwa nyingi.
Probability hainaga guarantee, kinyume cha probability ni uhakika

wapo wanaosugua benchi kitaa pia
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Kama ni wa kike ni rahisi kutiwa mimba maana akishatoka nje ya NECTA na ana miaka 18 halindwi tena na ile sheria ya kutomtia mimba mwanafunzi.
 
Vyuo vya Clinical Officers, Nursing, Pharmacy ni vingi kama utiriri. Nawapa miaka 10 baadaye watarudi palepale kama vyuo vya HR na Community Development

Mtoa mada angeshauri Vijana waziweke Akili zao kwenye kujiajiri kuliko kufikiri hicho alichokishauri.

Kwa sasa Madaktari ni wengi, CO, manesi, na wafamasia, Watu wa maabara.
 
Kweli gone are the days mtu kufanya kile anachopenda, ndio maana tuma madaktari lakini hatuna healers (watu wamekuwa kama mashine) Kazi kama ualimu na udaktari ni wito...; Binafsi ushauri wangu chochote utakachosoma soma (don't let schooling interfere with your education) ila ikiwezekana fanya kile unachopenda hata ukikosa ujira mkubwa bado utakuwa una-enjoy the ride...

By the way Uhasibu ni kama obsolete kwa sasa chochote unachoweza kunifanyia naweza kukifanya instantly kwa kutumia software tena kinatoa reports zote...

Kama dunia tumepotea watu hatufanyi kile kinachotakiwa kufanyika bali tunafanya kile ambacho tutapata ujira hata kama tunachofanya hakina tija (ndio maana kuna utapeli mwingi unaingia kama Ponzi schemes n.k.) au kutengeneza vijikazi unnecessary ili tu watu wapate kuwanyonya wenzao - Ukiangalia huu Mfumo wa Pesa wa Mabenki ni Desi Iliyochangamka
 
By the way Uhasibu ni kama obsolete kwa sasa chochote unachoweza kunifanyia naweza kukifanya instantly kwa kutumia software tena kinatoa reports zote...
Huwezi kuwa muhasibu bila kuwa na cpa.

hata uwe na phd au masters bila cpa huwezi kutambulika kama muhasibu.

kazi za uhasibu zinafanywa na wahasibu chini ya bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu.

Cpa wa kwanza nchini alikuwa marehemu Reginald Mengi.
 
probability ndogo sana, hapa tz nzima wachezaji wapo kibao ila waliofanikiwa kuwa na mishahara ya kuwatunza vizuri hata wakistaafu hawazidi kumi
Binadamu ameumbwa kutumia akili. 😀😀😀
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Hii nzuri zaidi ila awe na marks nzuri yaani credit sio wale waliofaulu kwa mbinde na kubahatisha kupata D za masomo manne..
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Form five na six hakumuongezei chochote zaid ya umri labda na namna ya kuchangamana na watu tofauti napo akisoma hizi shule za serikali kwa hyo advance
 
Huwezi kuwa muhasibu bila kuwa na cpa.

hata uwe na masters bila cpa huwezi kutambulika kama muhasibu.

kazi za uhasibu zinafanywa na wahasibu chini ya bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu inayoongozwa na cag
Ndio hayo nayosema..., Mtu anakula ili apate nishati aweze kuishi; kwahio chakula kipo pale ili mtu apate nishati watu hawali sababu wamekuwa wakila tangia enzi na enzi; na mkulima ana-fulfill hio need ya watu kula (kwahio watu wakipata pills ambazo haziihitaji tena chakula hicho basi mkulima atakuwa hana kazi)

Tukija kwenye uhasibu mambo yamekuwa simplified unakuta Kampuni ambayo hapo awali ingebidi ichukue siku kupata information inachukua second..., Hayo ya CPA, UHASIBU na Requirement kwamba lazima uwe na mtu Certified ndio hayo nimeweka hapo juu (red tapes ili watu wapate pesa) kwa sasa ambacho agefanya mtu kinaweza kuwa streamlined hapo hapo kila transaction inapofanyika
 
Achana na masuala ya elimu hasa nyakati hizi. Nawashauri vijana mkimaliza form 4 ingienj mtaani muanze kutafuta pesa huko vyuoni ni kupoteza muda na pesa ambazo pengine zingekuwa mtaji wako wa biashara.

Mimi ni diploma na degree ya Accounting (uhasibu) but now nafanya umachinga, najilaumu sana kwanini nimepoteza muda na gharama huko vyuoni. Najuta sana tena sana

Elimu kwa miaka ya sasa hivi ni kama laana tu wasomi tunaonekana kama tumelaaniwa kuna haja ya kufanya maboresho kwenye huu mfumo wa elimu kukaririsha vitu visivyo na msaada wowote kijamii ni upumbavu. Narudia tena elimu ya sasa ni upumbavu
 
Kiwango cha elimu ya mtoa hoja ni kipi? #AkilizaBandia
 
Doctor, engineer au Lawyer ikishindikana angalau somea uhasibu.

Niseme tu ya kwamba wapo wanaosomea hata degree ya kichina wanapata ajira hapahapa Tanzania lakini Probability (makadirio ya uwezekano) ya kupata hizo kazi ni ndogo.

Lakini hizi kozi tajwa angalau zina Probability (makadirio ya uwezekano) nzuri ya kuajiriwa sambamba na malipo mazuri, vijana wengi tu wapo makazini kwenye hizi kazi na hali zao kiuchumi si haba. Haimaanishi kwamba wooooote wanaajiriwa ama kujiajiri, LA HASHA!! wengine wanasugua benchi mtaani lakini kozi hizi angalau zina nafuu kwenye Probability (makadirio ya uwezekano) ya kuajiriwa ama kujiajiri, Mambo hayana formula lakini ni vema kufanya kitu walau kina Probability (makadirio ya uwezekano) nzuri, hata kwenye muziki yupo Diamond platnumz lakini probability ya mtu aliemaliza form 4 aanze kuimba ategemee muziki pekee kuendesha maisha ni ndogo sana, ni heri adungue mgahawa wake angalau kuna Probability nzuri ya uhakika wa kuendesha maisha yake.

Madaktari wana bodi yao Medical Council of Tanganyika, jina la daktari linaanza kwa Md flani. Afya ndio mtaji jamani, Uhitaji wao ni mkubwa, mishahara yao si haba, na mtu akiweza kujiajiri afungue hata sehemu yake kama zahahanati ni jambo la neema kwa jamii maana huduma za afya bado zipo chache.

Engineers wana bodi yao, Engineers Registration Board, jina la daktari linaanza kwa Eng, flani. hawa ndio mafundi mitambo, wahandisi wa barabara, wanaojenga majengo, wahandisi wa computer, n.k. huku waliojaa wengi ni wanaume tofauti na kwengine, kwa wanawake nadhani huwa wanapata upendeleo maalum kwenya ajira.

wanasheria wana bodi yao, Tanganyika law society, jina linaanza kwa wakili flani. hapa wapo wale mapilato wanaotembelea gari zimeandikwa J, wapo washauri wa sheria wa kulipwa, wapo mawakili, wapo wenye law firms zao, n.k. asikwambie mtu yani watu wapo tayari kutoa chochote kukwepa maisha nyuma ya nondo, kudai haki zao, kujitetea, n.k. wanasheria ndio wanufaika hapa.

wahasibu wana bodi yao, National board of accountants and auditors jina la mhasibu linaanza kwa Cpa flani. ndio wanaohusika na usimamizi wa fedha kuanzia mapato, matumizi, faida , n.k. wapo kwa wingi karibu kila shirika maana pesa bila usimamizi ni hatari, kwa cpa kima cha chini cha mshahara inasemekana ni milioni 1.3, kwenye kujiajiri kuna accounting firms hawa ndio wanahusika na kusimamia hesabu za makampuni, kusaidia watu kupeleka tax returns TRA, n.k. pesa ipo.

Ni kipimo cha kuonyesha uzito wa haya mambo, bodi hizi zipo tangu zamani na ili uwe mwanachama inabidi ufanye mitihani yao.

Pia ni inapendeza kuanza kusomea taaluma mapema vyuoni baada ya kuhitimu form 4, diploma miaka mitatu kisha unaingia degree pamoja na wale waliotokea sekondari form 6, kumbuka form 6 ni elimu ya sekondari wala sio elimu ya taaluma ndio maana mtu aliesoma form hawezi kuajiriwa bila degree lakini mwenye Diploma anaweza kupata ajira bila degree, Pia kazi za degree ni za wote waliotokea form 6 kwenda degree na wale form 4>diploma>degree lakini kazi za diploma ni maalum kwajili ya walioanza kusoma chuo baada ya form 4, nchi zilizoendelea kama Kenya walishafuta form 5 na 6 ni moja kwa moja kuanza kusomea taaluma chuoni.

Wanaijeria ndio jamii ya waafrika walioelimika zaidi wanasisistiza watoto wao wasomee Doctor, Lawyer ama Engineer, waisrael na wahindi ndio makundi yenye wasomi zaidi wanasisitiza watoto wao wasomee Doctor, engineer ama Lawyer,
Connection
Bahati
 
Back
Top Bottom