Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

Nimegundua wewe una elimu ya kuungaunga , yani unafundisha watu uoga wa maisha wasomee ma udaktari eti mshahara sio haba. Akili za kimaskini. Alafu national aviation board inahusiana vipi na bodi ya uhasibu?
 
Ndio unavyojidanganya? Umahiri kwenye kesi ni kopaji ukiachana na kukariri ,Bora nisome psychology naweza kujiajiri fasta kuliko hiyo Sheria
Naweka facts tu hapa.

Hio psychology kwa wabongo mwamko bado mdogo, mtu hadi anyanyue mguu aende kwa mwanasaikolojia bado sana, wengi wanaenda kwa marafiki, ila mtu akipata kesi ni fasta tu anatafuta wakili.
 
Mwanangu nataka acheze kandanda awe Kama Cristiano Ronaldo, au Lionel messi πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mwanangu nataka acheze kandanda awe Kama Cristiano Ronaldo, au Lionel messi πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
probability ndogo sana, hapa tz nzima wachezaji wapo kibao ila waliofanikiwa kuwa na mishahara ya kuwatunza vizuri hata wakistaafu hawazidi kumi
 
Unaongelea hawa madaktari waliofanyiwa figisu ya kunyimwa leseni ya kufanya kazi? bongo fitna zishakuwa nyingi.
Probability hainaga guarantee, kinyume cha probability ni uhakika

wapo wanaosugua benchi kitaa pia
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Kama ni wa kike ni rahisi kutiwa mimba maana akishatoka nje ya NECTA na ana miaka 18 halindwi tena na ile sheria ya kutomtia mimba mwanafunzi.
 
Vyuo vya Clinical Officers, Nursing, Pharmacy ni vingi kama utiriri. Nawapa miaka 10 baadaye watarudi palepale kama vyuo vya HR na Community Development

Mtoa mada angeshauri Vijana waziweke Akili zao kwenye kujiajiri kuliko kufikiri hicho alichokishauri.

Kwa sasa Madaktari ni wengi, CO, manesi, na wafamasia, Watu wa maabara.
 
Kweli gone are the days mtu kufanya kile anachopenda, ndio maana tuma madaktari lakini hatuna healers (watu wamekuwa kama mashine) Kazi kama ualimu na udaktari ni wito...; Binafsi ushauri wangu chochote utakachosoma soma (don't let schooling interfere with your education) ila ikiwezekana fanya kile unachopenda hata ukikosa ujira mkubwa bado utakuwa una-enjoy the ride...

By the way Uhasibu ni kama obsolete kwa sasa chochote unachoweza kunifanyia naweza kukifanya instantly kwa kutumia software tena kinatoa reports zote...

Kama dunia tumepotea watu hatufanyi kile kinachotakiwa kufanyika bali tunafanya kile ambacho tutapata ujira hata kama tunachofanya hakina tija (ndio maana kuna utapeli mwingi unaingia kama Ponzi schemes n.k.) au kutengeneza vijikazi unnecessary ili tu watu wapate kuwanyonya wenzao - Ukiangalia huu Mfumo wa Pesa wa Mabenki ni Desi Iliyochangamka
 
By the way Uhasibu ni kama obsolete kwa sasa chochote unachoweza kunifanyia naweza kukifanya instantly kwa kutumia software tena kinatoa reports zote...
Huwezi kuwa muhasibu bila kuwa na cpa.

hata uwe na phd au masters bila cpa huwezi kutambulika kama muhasibu.

kazi za uhasibu zinafanywa na wahasibu chini ya bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu.

Cpa wa kwanza nchini alikuwa marehemu Reginald Mengi.
 
probability ndogo sana, hapa tz nzima wachezaji wapo kibao ila waliofanikiwa kuwa na mishahara ya kuwatunza vizuri hata wakistaafu hawazidi kumi
Binadamu ameumbwa kutumia akili. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Hii nzuri zaidi ila awe na marks nzuri yaani credit sio wale waliofaulu kwa mbinde na kubahatisha kupata D za masomo manne..
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Form five na six hakumuongezei chochote zaid ya umri labda na namna ya kuchangamana na watu tofauti napo akisoma hizi shule za serikali kwa hyo advance
 
Huwezi kuwa muhasibu bila kuwa na cpa.

hata uwe na masters bila cpa huwezi kutambulika kama muhasibu.

kazi za uhasibu zinafanywa na wahasibu chini ya bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu inayoongozwa na cag
Ndio hayo nayosema..., Mtu anakula ili apate nishati aweze kuishi; kwahio chakula kipo pale ili mtu apate nishati watu hawali sababu wamekuwa wakila tangia enzi na enzi; na mkulima ana-fulfill hio need ya watu kula (kwahio watu wakipata pills ambazo haziihitaji tena chakula hicho basi mkulima atakuwa hana kazi)

Tukija kwenye uhasibu mambo yamekuwa simplified unakuta Kampuni ambayo hapo awali ingebidi ichukue siku kupata information inachukua second..., Hayo ya CPA, UHASIBU na Requirement kwamba lazima uwe na mtu Certified ndio hayo nimeweka hapo juu (red tapes ili watu wapate pesa) kwa sasa ambacho agefanya mtu kinaweza kuwa streamlined hapo hapo kila transaction inapofanyika
 
Achana na masuala ya elimu hasa nyakati hizi. Nawashauri vijana mkimaliza form 4 ingienj mtaani muanze kutafuta pesa huko vyuoni ni kupoteza muda na pesa ambazo pengine zingekuwa mtaji wako wa biashara.

Mimi ni diploma na degree ya Accounting (uhasibu) but now nafanya umachinga, najilaumu sana kwanini nimepoteza muda na gharama huko vyuoni. Najuta sana tena sana

Elimu kwa miaka ya sasa hivi ni kama laana tu wasomi tunaonekana kama tumelaaniwa kuna haja ya kufanya maboresho kwenye huu mfumo wa elimu kukaririsha vitu visivyo na msaada wowote kijamii ni upumbavu. Narudia tena elimu ya sasa ni upumbavu
 
Kiwango cha elimu ya mtoa hoja ni kipi? #AkilizaBandia
 
Connection
Bahati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…